Ummy Mwalimu: Wachangiaji damu, kupewa kipaumbele wanapohitaji damu hospitalini. Watapewa kadi Maalum

Ndugu Kilatha, mimi nadhani unasumbuliwa na chuki tu. Kiuhalisia hata huyo aliyejitolea damu akipatwa na tatizo ambalo litahitaji kuongezewa damu, ndugu na jamaa wanaweza kumchangia damu. Na sidhani kama kuna mtu anajitolea damu ili akipata tatizo apewe kipaumbele. Huko ni kujiombea matatizo, kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza kufanya hivyo.

Naamini unasoma michango mbali mbali inayotumwa hapa kujaribu kukuelewesha. Tatizo lako ni kwamba unajifanya unajua kuliko watu wengine. Lakini bahati mbaya huelekei kama unajua kama ambavyo unavyotaka watu wakuchukuliye. Ndugu yangu hata maneno tu ya kitaalamu yanakushinda kuandika! Na bado umeng'ang'ana hapa kutuaminisha kuwa u mjuzi. Au unataka cheo?

Nakushauri pumzika ndugu yangu maana unazidi "kujivua nguo".
 
Hivi huyu mtu anafahamu hata Medical Ethics?

Waziri wa afya jifunze ‘medical ethics’ under the concept of ‘non malificence’ you can’t do harm to a patience.

Hakuna priority kwenye afya who deserve the resources than another. It’s either first come first served or who needs it the most based on their poor medical condition.

Lakini hakuna sera ya kuchangia, upendelewe. Ni jukumu la wizara ya afya kukusanya damu na watu wana mbinu za kufanya hiyo shughuli.

Wanakupenda huko kwa sababu siyo mtaalamu unaeongea ujinga mtupu na aliekupa hayo mapendekezo ni mjinga vile vile.

=====

Na. WAF - Dar Es Salaam
View attachment 2131495
Serikali kupitia wizara ya Afya imejipanga kutoa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu wanaojitolea mara kwa mara angalau mara tatu kwa mwaka.

Hayo yamesemwa leo Februari 25, 2022 na Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika ziara ya kutembelea makao kuu ya mpango wa taifa wa damu salama jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Kadi za kieletroniki zitaepusha usumbufu kwa wachangia damu endapo watahitaji huduma ya damu kwani kadi hizo zitaonesha jina la mchangiaji damu, kundi la damu yake na namba ya kadi, na mchangiaji huyu atapewa kipaumbele akiwa na mgonjwa hata yeye mwenyewe.

"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu salama pamoja na vifaa vya ukusanyaji kwa Halmashauri zote nchini 184 ili kwenda kumaliza changamoto ya ukusanyaji ambayo imejitokeza nchini hivi sasa na kusababisha uhaba wa damu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Nitoe wito kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea vifaa hivyo vya kuchangia damu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji damu kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji". Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema vifo vingi vya kina mama wajawazito hutokana na ukosefu wa damu salama na hivyo kuitaka jamii iweze kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji huku akieleza kuhamasisha vikundi mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya uchangiaji.

Nae, Meneja mpango wa Taifa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo ameishukuru Serikali kwa hatua inayochukua juu ya upatikanaji damu salama kwa urahisi.

"Sasa kazi ni kwetu kuhakikisha damu salama inapatikana kwa kuungana na wananchi juu ya uchangiaji damu na naamini tukishirikiana tutaokoa vifo vingi". Amesema Dkt. Lyimo.

Akili za mwendo Kasi,kila mtu atabeba makadi mangapi?ajari huwa haisemi,ikitokea wakati hiyo kadi hajaibeba na ni mchangia damu mzuri,hatahudumiwa? Mtu afikishwe hospitari,badala ya kumuhudumia,unaanza kucheki data base kama amekuwa akichangia damu,kwa mtandao gani!!huu huu wa TRA,NIDA?
Toeni Elimu umuhimu wa kuchangia damu,au iwekwe sheria kila mwanaume juu ya miaka 18 achangie damu mara mbili kwa mwaka
 
Elimu na campaign endelevu ndio suluhisho.
 
Hatari sana
but na nyinyi mnamvizia akosee ili mumseme!! Kuonesha kwamba hatoshi!
wabongo noma sana......
Hapa duniani Kuna watu muda wote huishi kwa kujali shida za wengine. Imagine mtu kama Malisa kule Facebook kwa mengi anayofanya, chukulia watu ambao wakisikia tuu Kuna wiki ya kuchangia damu, au jirani ana uhitaji wa damu anaacha shughuli zote na kwenda faster kusaidia, wakati wengine tena majority ndiyo kwanza anakuambia nawahi Bar kupata Serengeti baridi au kuangalia mpira... Sasa unatarajia nini hapoo?
 
Ndugu Kilatha, mimi nadhani unasumbuliwa na chuki tu. Kiuhalisia hata huyo aliyejitolea damu akipatwa na tatizo ambalo litahitaji kuongezewa damu, ndugu na jamaa wanaweza kumchangia damu. Na sidhani kama kuna mtu anajitolea damu ili akipata tatizo apewe kipaumbele. Huko ni kujiombea matatizo, kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza kufanya hivyo.

Naamini unasoma michango mbali mbali inayotumwa hapa kujaribu kukuelewesha. Tatizo lako ni kwamba unajifanya unajua kuliko watu wengine. Lakini bahati mbaya huelekei kama unajua kama ambavyo unavyotaka watu wakuchukuliye. Ndugu yangu hata maneno tu ya kitaalamu yanakushinda kuandika! Na bado umeng'ang'ana hapa kutuaminisha kuwa u mjuzi. Au unataka cheo?

Nakushauri pumzika ndugu yangu maana unazidi "kujivua nguo".
6882ADB2-B875-46A5-AD97-CDD218F46F0E.jpeg

Huna tofauti na huyo waziri zaidi ya kuandika ujinga. Kuna units kama 30 za degree mtu anaesoma degree za health and social care management amalizi zote ndani ya miaka mitatu. Mie nishaandikia report zote mara kadhaa with different scenario.

3D1D9A1E-6616-4E1C-8CA0-41D2159CF89D.jpeg

532427F3-4960-43D4-ADCD-4012D188ADEA.jpeg

Unaelewa hiyo learning outcome 3 ya hii module ya quality management wanaposema preventing problems and controlling processes wanalenga nini?

Jibu hoja sio kuandika ujinga wakati una ata clue jinsi mambo yanavyosimamiwa.

Utaki kujua upande wa afya pekee na degree nyingine kabisa ya medics nimeandika vitu vingapi kuhusu medical processes.

Mtu aje nimfundishe mimi mwenyewe maana ya medical ethics aje atafute neno Iloilo kwenye post nyingine halafu anikosoe jambo ambalo kajifunzia kwangu in the first halafu nijibizane nae.
 
Ndugu Kilatha, mimi nadhani unasumbuliwa na chuki tu. Kiuhalisia hata huyo aliyejitolea damu akipatwa na tatizo ambalo litahitaji kuongezewa damu, ndugu na jamaa wanaweza kumchangia damu. Na sidhani kama kuna mtu anajitolea damu ili akipata tatizo apewe kipaumbele. Huko ni kujiombea matatizo, kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza kufanya hivyo.

Naamini unasoma michango mbali mbali inayotumwa hapa kujaribu kukuelewesha. Tatizo lako ni kwamba unajifanya unajua kuliko watu wengine. Lakini bahati mbaya huelekei kama unajua kama ambavyo unavyotaka watu wakuchukuliye. Ndugu yangu hata maneno tu ya kitaalamu yanakushinda kuandika! Na bado umeng'ang'ana hapa kutuaminisha kuwa u mjuzi. Au unataka cheo?

Nakushauri pumzika ndugu yangu maana unazidi "kujivua nguo".
D3C8D377-1717-46E3-9230-FAA269794D74.jpeg

Unaelewa nini hapo unapoambiwa unapopanga strategy moja ya vitu vya kuzingatia ni code of conducts na medical ethics ni sehemu ya code of conducts.

Like I said sina shida na waziri ila hana uwezo wa kuisimamia hiyo wizara.
 
Hivi huyu mtu anafahamu hata Medical Ethics?

Waziri wa afya jifunze ‘medical ethics’ under the concept of ‘non malificence’ you can’t do harm to a patience.

Hakuna priority kwenye afya who deserve the resources than another. It’s either first come first served or who needs it the most based on their poor medical condition.

Lakini hakuna sera ya kuchangia, upendelewe. Ni jukumu la wizara ya afya kukusanya damu na watu wana mbinu za kufanya hiyo shughuli.

Wanakupenda huko kwa sababu siyo mtaalamu unaeongea ujinga mtupu na aliekupa hayo mapendekezo ni mjinga vile vile.

=====

Na. WAF - Dar Es Salaam
View attachment 2131495
Serikali kupitia wizara ya Afya imejipanga kutoa kadi za kieletroniki kwa wachangiaji damu wanaojitolea mara kwa mara angalau mara tatu kwa mwaka.

Hayo yamesemwa leo Februari 25, 2022 na Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika ziara ya kutembelea makao kuu ya mpango wa taifa wa damu salama jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Kadi za kieletroniki zitaepusha usumbufu kwa wachangia damu endapo watahitaji huduma ya damu kwani kadi hizo zitaonesha jina la mchangiaji damu, kundi la damu yake na namba ya kadi, na mchangiaji huyu atapewa kipaumbele akiwa na mgonjwa hata yeye mwenyewe.

"Kila Mtanzania ana haki ya kupata damu lakini kwa wale ambao watakaokuwa na kadi watapewa kipaumbele cha kwanza". Amesema Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu salama pamoja na vifaa vya ukusanyaji kwa Halmashauri zote nchini 184 ili kwenda kumaliza changamoto ya ukusanyaji ambayo imejitokeza nchini hivi sasa na kusababisha uhaba wa damu katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Nitoe wito kwa waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanapokea vifaa hivyo vya kuchangia damu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kutatua changamoto ya upatikanaji damu kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji". Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema vifo vingi vya kina mama wajawazito hutokana na ukosefu wa damu salama na hivyo kuitaka jamii iweze kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji huku akieleza kuhamasisha vikundi mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya uchangiaji.

Nae, Meneja mpango wa Taifa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo ameishukuru Serikali kwa hatua inayochukua juu ya upatikanaji damu salama kwa urahisi.

"Sasa kazi ni kwetu kuhakikisha damu salama inapatikana kwa kuungana na wananchi juu ya uchangiaji damu na naamini tukishirikiana tutaokoa vifo vingi". Amesema Dkt. Lyimo.

Huyu Ummy bado yupo?
Alikuwa kimya kama maji ya mtungi mazishi ya aliye mchongea kwa mwendazake.
Sasa sauti inatoka.
 
View attachment 2133011

Unaelewa nini hapo unapoambiwa unapopanga strategy moja ya vitu vya kuzingatia ni code of conducts na medical ethics ni sehemu ya code of conducts.

Like I said sina shida na waziri ila hana uwezo wa kuisimamia hiyo wizara.
Sifa ya mtu asiyejua vitu ni kukimbilia kutukana. Hata kama ulisoma nadhani wewe ni mtu wa kukariri vitu tu ndiyo maana umeambatanisha "contents" za "course" badala ya kuzingatia ushauri wangu kuwa upumzike. Unashindwa hata kuandika "patient" badala yake unaandika "patience" halafu unaendelea kusumbua watu hapa.

Uzuri wa JF ni kuwa hujui unabishana na nani. Usitukane. Narudia tena pumzika. Huna cha maana unachoeleza hapa.
 
Una quote post za watu humu ambao awapo pengine thread ingekuwa ishapotea badala ya kijibu hoja zao unawaambia hawajui vitu vya kijinga,

Na mimi pia hunijui vinginevyo usingelazimisha vimaneno vya kizungu kunisumbua.

Najibu unavyokuja ukija na ngebe utajibiwa kwa ngebe hakuna kingine and there is nothing you can do about that.

Unawekewea module content ungekuwa mwelewa you would have got the idea what the lectures (books, research paper) would cover siku ukiambiwa uandike report ya kuboresha eneo la kazi una ideas uanzie wapi or what references to search.

Wavivu wa kujifunza mambo mapya, lakini wepesi wa kuandika ujinga. Na ndio watu mnaomwingiza mkenge waziri kutangaza policies ambazo aziendani na standards wala miliki ya utoaji wa huduma za afya.

Na nitachangia kadri mada inavyoendelea; hujui kitu halafu unataka kupangia watu kwanini nisikwite lofa.

Do what you can as for me ukiendelea nakuelekeza kwenye ignore list tu; halafu we ufanye unavyoweza bogus kweli.
 
Sisi wenye sickle cell tusioweza kuchangia damu, twaafwa!
Msioweza kuchangia damu hamuwezi kufa, kwa sababu, utaratibu huu ukieleweka vizuri na wananchi wakajitoa, kutakua na reserve kubwa ya damu. Hii itawasaidia hasa Yale makundi maalum yenye uhitaji Mkubwa wa damu ikiwa ni pamoja na Sicklers.
Inasikitisha kuona ndugu wa mgonjwa aliyefika hospitali akiwa in critical state kwa upungufu Mkubwa wa damu, akaongezewa na afya yake ikaimarika, kugoma ku replace damu hiyo.
 
Ndio maana watu wanatumia mbinu za public health campaign kuhamasisha.

Tatizo la upungufu wa akiba ya damu sio wananchi; ni incompetent people responsible for inventory control.
-awafuati kiwango cha chini kwenye akiba kabla ya kuanza campaign (nina uhakika wa asilimia 100% lazima kuna kiwango cha order point) sema wao awafuati mpaka akiba inakuwa ndogo kiasi cha kulazimisha ndugu kuchangia.

-campaign yenyewe sio endelevu

-poorly communicated, wrong use of channel to reach into wider audience na mikwara juu.

Issue ni management incompetency isiyojua hata mbinu za kukusanya damu na inventory control; halafu wanalaumu wananchi.

Ndio maana ata solution inaenda kinyume na medical ethics.

Just get the right people in those places, waziri anategemea washauri ambao ni ovyo kwa kauli zake ambazo mara kadhaa aropoke mambo ya ovyo.

Upuuzi huo awawezi mshauri mtu kama Dr Gwajima au mtu wa caliber yake.

Mimi pamoja na makelele yangu kesho niteuliwe waziri wa fedha au mkurugenzi wizara ya afya ntaigopa hiyo nafasi na kukataa.

Mtu unakuta hana uwezo na nafasi kwa elimu, wala work experience lakini analilia technical position na hana uoga. Matokeo yake anaongea upuuzi kwa kujiamini kabisa as if nchi nzima viazi ailewi what is right and wrong; or how things out to be done.
 
Inasikitisha kuona ndugu wa mgonjwa aliyefika hospitali akiwa in critical state kwa upungufu Mkubwa wa damu, akaongezewa na afya yake ikaimarika, kugoma ku replace damu hiyo.
Wabongo wengi Wana ngoma kwasabb wanapenda Sana ngono. Ndiyo maana wanakwepa kupimwa kabla ya kuchangia damu kwa kuogopa kuumbuka. Mbaya zaidi wahudimu wa afya wa miaka hii hawana Siri.
 
😀Kwamba wabongo tunahofu ya kupewa majibu tusiyoyataka bila maandalizi. Hata hivyo, kujitolea damu kuna faida ikiwa ni pamoja na kujua Hali yako ya maambukizi ya HIV na virusi vinavyosababisha homa ya Ini. Pia, mchangiaji atajua kundi lake la damu, wingi wa damu na Hali yake ya magonjwa ya zinaa Kama Kaswende.
 
Mmh! Mkuu hatari ya mtu kuambiwa kuwa ana ngoma ni kubwa kuliko kuishi na hayo magonjwa pasipo kujua.

Huwa kwa miezi mitatu ya kwanza watu wanasinyaa kuliko maelezo na wengine hufaliki kabisa kabla ya kuizoea hali.
 
Mmh! Mkuu hatari ya mtu kuambiwa kuwa ana ngoma kuliko kuishi na hayo magonjwa pasipo kujua.

Huwa kwa miezi mitatu ya kwanza watu wanasinyaa kuliko maelezo na wengine hufaliki kabisa kabla ya kuizoea hali.
Uko sahihi mkuu. Ni kazi kuanza maisha mapya na mdudu. Tujilinde.
 
Ndugu Kilatha, mimi nadhani unasumbuliwa na chuki tu. Kiuhalisia hata huyo aliyejitolea damu akipatwa na tatizo ambalo litahitaji kuongezewa damu, ndugu na jamaa wanaweza kumchangia damu. Na sidhani kama kuna mtu anajitolea damu ili akipata tatizo apewe kipaumbele. Huko ni kujiombea matatizo, kitu ambacho sidhani kama kuna mtu anaweza kufanya hivyo.

Naamini unasoma michango mbali mbali inayotumwa hapa kujaribu kukuelewesha. Tatizo lako ni kwamba unajifanya unajua kuliko watu wengine. Lakini bahati mbaya huelekei kama unajua kama ambavyo unavyotaka watu wakuchukuliye. Ndugu yangu hata maneno tu ya kitaalamu yanakushinda kuandika! Na bado umeng'ang'ana hapa kutuaminisha kuwa u mjuzi. Au unataka cheo?

Nakushauri pumzika ndugu yangu maana unazidi "kujivua nguo".
Binafsi mimi ni blood donor wa miaka mingi sana, licha ya kujitolea kusaidia wengine, pia ninatoa kwa ajili ya manufaa yangu binafsi na watu wangu wa karibu- simple as that.
 
Mnajua wazi damu haiuzwi. Halafu kuna binadamu mmoja anajitolea mara tatu kwa mwaka kuchangia damu kwa hiyari na utashi wake. Kwa nini asipatiwe kipaumbele? To hell with ethics.

Mnajua yale masindano yanavyouma? Sasa kwa hiyari yake mtu huyu anatobewa mara tatu/nne kwa mwaka akichangia damu kwa watu asiowajua.

Nyie wengine wakati huyu anajiamsha kwenda kituo cha damu salama huwa mnakuwa wapi? Mnaogopa yale masindano, au mnaogopa kuambiwa damu yako si salama?
Mkitaka pasiwepo na upendeleo nanyi mkachangie.
Sure.
 
Uzuri wa JF ni kuwa hujui unabishana na nani. Usitukane. Narudia tena pumzika. Huna cha maana unachoeleza hapa.
Mkuu neene, nimekupenda bure na kukuelewa, na hata kutokurudi kuendelea kubishana pia nimekuelewa, otherwise people can't notice the difference!.
Ubarikiwe sana!.
P
 
Mmh! Mkuu hatari ya mtu kuambiwa kuwa ana ngoma ni kubwa kuliko kuishi na hayo magonjwa pasipo kujua.

Huwa kwa miezi mitatu ya kwanza watu wanasinyaa kuliko maelezo na wengine hufaliki kabisa kabla ya kuizoea hali.
Mkuu, si kweli kwamba hatari ya kuambiwa ukweli wa Hali ya maambukizi ni kubwa kuliko maambukizi yenyewe. Watu wengi wanaogundulika at late stages (3 or 4) husumbuka Sana kurudi kwenye Hali zao za awali kuliko wale wanaogundulika mapema. Hii inasababishwa na magonjwa nyemelezi ya hatua ya tatu na nne y UKIMWI. Lakini ukiwa asymptomatic, ukaanza dawa, hautaathirika kimwili Wala kiutendaji.
 
Back
Top Bottom