Ummy Mwalimu: Wagonjwa kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti moja ya sababu kuyumba kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

Duuh

Waziri anatangaza muwa Mfuko upo kwenye hatare ya kufilisika kutokana na gharama za uendeshaji kuzidi mapato yake lakini hapo hapo anawatoa wasiwasi kuwa huduma zitaendelea kuwa bora na tusiwe na wasiwasi
 
View attachment 2342142

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
Ummy,! Ni utasikia uliopita! Wewe mwenyewe Kwa kauli yako ulituambia Baada ya kushuhudia madaktari wakiombana Rushwa Sasa ukitarajia mgonjwa afanyeje au ndugu wasemeje! Kumbe basi tatizo Liko humo ndani mwenu liondoeni kwanza!
Duuh Tanzania kila Kona ni tambara bovu na Bado wanajifunikia! ! Hatari.
 
Ummy wa awamu hii sio Ummy yule wa Magu, ni Ummy mwenye mbwembwe ninyi ili kuilinda chinjio lake ama mkate wake, anaongea kwa bashsha kama anaimba taarabu hana tena dhamira ya dhati kuwatumikia Watanzania bali show off basi.
 
Yote yanasababishwa na madaktari wenu, unakuta daktari anakuandikia kipimo CT-SCAN anakuja mwingine au huyo huyo anakuambia ukapime tena.

Nashangaa ndio utaratibu au wanapenda kusumbua watu na kupoteza pesa za watu, kwann asitumie ile ya kwanza kama reference kwake?
 
Kwan hakuna system inayoweza kutambua jana mwanachama alichek kitu kadhaa leo mbona anachek tena.? Kwan ulaya wanafanyaje fanyaje?
 
Vipimo vingi wakati mwingine ni vya makusudi tu ili kuongeza kipato hususani hospitali binafsi. Kwa mfano naenda kituo binafsi natoa maelezo namafua na joto la mwili liko juu... Hapo utashangaa unaansikiwa vipi hata vitano maabara. Kapime UTI, Typhoid, Malaria, TB. Tabu tupu
 
View attachment 2342142

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
Hii point nakubaliana nayo shida madaktari kutoamini vipimo vya hospital flani , kweli na wakati mwingine htashi wa wagonjwa hapo kwenye vipimo vile vile walimit kabisa kuokoa mfuko
 
View attachment 2342142

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi na wanachama wa NHIF akieleza kuwa pamoja na mfuko huo kukabiliwa na changamoto nyingi bado utaendelea kuwepo na kutoa huduma bora za afya.

Ameongeza kuwa, ili mfuko uweze kuendelea vizuri mambo kadhaa yanapaswa kufanyika ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama, kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma za afya.
Utafiti ufanyike vizuri ili kujua chanzo halisi cha nhif kuyumba.mwanzoni wakati shirika linaanza,watumishi wengi hawakulikubali,hivyo walikuwa wanabeba familia zote kila siku Kwa ajili ya matibabu ili kulikomoa,lakini halikuyumba.Haya magonjwa ya Leo hata wakati nhif inaanza yalikuwepo,lakini halikuyumba.Nini kimetokea?
 
Mtu hadi anatoka Hospital A to Hospital B, ni kutokana na huduma finyu zinazonekana hata kwa macho, matokeo yake mtu anakosa imani anaenda ku cheki na kwingine asije kuwa kapewa tango pori
Ninani aliesema huduma ni finyu, kama ni hivyo sasa hospitali zianze kufungiwa. Sihuduma nifinyu.
 
Siku akiumwa tuone kama hatajaribu hosp mbalimbali hadi aende India.

Kwingine vipimo vinatofautiana

Mtu anapigania uhai, hakuna mtu anapenda kuumwa.
Hapa ndio maana mtu hufikia treatment failure na figo kugonga mwamba. Ugonjwa haujaribiwi bali unajitibu. Usikubali mwili wako utumike kama test subject kwasababu unajiangamiza mwenyewe ila bado Mtanzania yeye ni mguu na njia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtu hadi anatoka Hospital A to Hospital B, ni kutokana na huduma finyu zinazonekana hata kwa macho, matokeo yake mtu anakosa imani anaenda ku cheki na kwingine asije kuwa kapewa tango pori
Hahah unakuta dokta kakuseti kuwa una UTI na Malaria kumbe hata UTI yenyewe huna unabugia antibiotic unawaongezea faida 😂😂😂
 
Huyu naye. Kwahiyo tusipate mitazamo tofauti juu ya magonjwa yetu?
Mnatunyonya na bado mfuko unayumba. Lol
Nani aliyekukataza kupata msimamo tofauti. Ila siunajua window period ya dosage kuisha au wewe ni storage ya dawa. Pia chukulia ile ni pesa yako, sasa fanya kama hivyo uone madhara. Mtanzania nimtu mgumu kumuelewesha.
 
Hahah unakuta dokta kakuseti kuwa una UTI na Malaria kumbe hata UTI yenyewe huna unabugia antibiotic unawaongezea faida 😂😂😂
Hii wengi sana imewakuta, wanapewa dozi nzito nzito ili kuondoa madawa kwenye store ilhali mtu haumwi au ana ka ugonjwa kadogo tu
 
Back
Top Bottom