sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Maisha ni siasa,bila Siasa hakuna maisha. Unapozuia siasa unazuia maisha.
Damu ya Maisha ni siasa,unapozuia damu isitembee kwa wiki mbili,unazuia uhai wa maisha yanayoendeshwa kwa misingi ya siasa.
Unaweza usione athari kama walivyo wajinga wengi,lakini ulishawahi kufikiri kwanini mtoto mkubwa nyumbani asiposimamia nafasi yake ipasavyo walio chini yake hupoteza dira,ndiyo maana wanazuoni wa theolojia walifikiri kwa kina na kuona umuhimu wa kuwaombea wazaliwa wa kwanza.
Chama kikuu cha upinzani ndiyo mtoto mkubwa wa upinzani anayepambana na mifumo mibovu na kandamizi inayoathiri ndugu zake wa upinzani.
Kukishambulia chama kikuu cha upinzani na vyama vingine kudhani hiyo ni fursa kwao,wanajidanganya sana, kwa kuwa kila atayekuwa mpinzani wa kweli ajiandae kupitia maswahibu haya anayopitishwa CHADEMA.
Umahiri wa CHADEMA kupambana na mifumo na vikwazo kila kukicha kunaendelea kukiimarisha kukabiliana na misukosuko,lakini kuendelea kuaminiwa na kila mpenda haki wa Taifa hili.
Na kwa kuwa kukubalika kwake kuna wakera watawala, mihimili imeungana kupambana naye kwenye kila idara katika kudhoofisha nguvu ya upinzani nchini. Kwa muktadha huo mahakama imepata nguvu ya kuzuia kwa kuwa imeamua kujiondoa kuwa sehemu ya haki na kuwa sehemu ya maelekezo ya simu kama alivyosema Rostam.
Kwa msingi huo Mahakama imezuia shughuli ya kisheria ya kazi ya siasa kwa CHADEMA ambayo ipo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa,sheria namba 5 ya mwaka 1992 sura ya 258, ambayo imeakiasi takwa la katiba ya JMT ibara ya 3.-(a) na (b).
Unapozuia shughuli halali ya kisiasa maanake unazuia mawazo mbadala au kinzani yenye kuleta lahaja za kisiasa katika muktadha mzima wa siasa za ushindani,ambazo zipo kwa mujibu wa katiba ya JMT.
Kumekuwa na sikitiko kubwa linalodhoofisha mfumo wa siasa za vyama vingi kutokana na kuvunjika kwa separation of power kwa mihimili mitatu ya nchi na kuifanya idara za serikali zinazofanya kazi kwa maagizo ya serikali.
Mhimili pekee unaotazamwa angalau kwa macho ya rohoni lakini sasa unatia kinyaa ni Mahakama. Hii inatokana na mfumo unaosimamia maadili ya mahakama kuingiza wanasiasa kuingilia taaluma na mhimili unaojitegemea.
Ikitokea mahakama ikapoteza mwelekeo, Taifa nalo limepotea kwa kuwa hakuna haki itakayosimama zaidi ya utashi wa mtawala aliyeko kwenye kiti cha enzi.
Leo mahakama imezuia chama cha siasa kufanya siasa kwa muda wa siku 14,Taifa lipo kimya linastaajabu ya Samia wanayaona ya Jaji Juma.
Siasa ndiyo mwamuzi wa maisha ya wananchi,na siasa ndiyo mfumo wa maisha unaoamua maisha ya watawaliwa waishi kwa kiwango gani,umaskini uliokithiri au umaskini wa kati,au utajiri wa kupindukia.
Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa ukiwa umeoa wake zaidi ya mmoja jitahidi sana mahusiano yao yasiws sawa wakati wote, vinginevyo maisha yako yatakuwa hatarini na huenda ukaharibu mfumo wako wa maisha.
Mwingine akasema "wizi wowote ili ufanikiwe lazima uwe na connection"
Mihimili mitatu ya mamlaka imeungana na kusahau kuwa wao ni mitala,maisha ya mume wao (Wananchi) yapo hatarini,kwa kuwa mbinu zote chafu za kumdhibiti muwe wao zimeathiri mwenendo mzima wa maisha ya mtafutaji huyu.
Maanake nini! Taifa limepoteza mshikamano wa kisiasa na kwa kuwa damu ya maisha ya wananchi imeingia cancer ya damu,watakaoumia ni wananchi.
Hakuna aliye salama kwenye mchezo huu mchafu wa maisha ya wananchi yanayoendeshwa kwa misingi ya siasa. Wapo wanaojifariji kusema ndiyo maana hatutaki siasa,lakini wanasahau kuwa wanayafanyia mgomo maisha kwa kuwa mgomo wao unaathiri mwenendo mzima wa mfumo wa maisha.
Tumesema wizi ni connection,Taifa linaibiwa haki yake ya kuiwajibisha serikali kwa kuwa mihimili imetengeneza connection ya kudhibiti viherehere wanaonusa michezo michafu( vyama vya upinzani) ya mtawala na idara zake,mahakama na bunge.
Athari zinazojitokeza, Hakuna aliye salama kwa kuwa aliyezoea kula nyama ya binadamu kamwe hawezi kuacha tabia yake hiyo,hata yanayofanyika sasa ni urafiki wa mashaka kumuangamiza mmoja kwa muda maalumu ilihali unayeshabikia ni kitoweo cha miaka mitano ijayo.
TCD ina dhima kubwa ya kufanya kuweza kulinda hadhi yao ya mapambano ya haki dhidi ya mwingiliano wa mwanachama mmoja mwenye vinasaba na serikali.
Msingi wa umoja huu ni kuuwa ushindani wa kisiasa ,vinginevyo umoja huu kwa kuwa umepoteza maana na kwa kuwa umevifanya vyama vya siasa kuwa wapiga chapuo wa CCM kuendelea kutawala bila kuzingatia misingi ya Demokrasia hauna budi kuvunjwa rasmi.
Leo CHADEMA anapambana na vikwazo vya mtawala asiyekuwa muumini wa ushindani wa Demokrasia na utawala bora ndani ya 4R's zake fake.
Mapambano haya ni mkakati madhubuti kuhakikisha CCM haina mpinzani wa kweli zaidi ya kutanua wigo wa fursa ya kukopea na misaada yenye masharti ya kutaka uimarishaji Demokrasia.
Lakini wapo wapinzani marafiki wa mfumo kandamizi wanadhani kufa kwa chadema ni fursa kwao,waulizeni NCCR MAGEUZI,C.U.F na TLP.
Ni wakati muhimu sana vyama vyote ambao ni mawindo ya baadaye ya watawala wasimame kwa sauti moja,kupinga udhalilishaji wa makusudi wenye taswira ya kuvunja hata Muungano.
Athari ya haya yanayotokea yanagusa Muungano na viashiria hivyo vimeanza kujadiliwa kutokana na mbinu chafu za mtawala kwa kutumia watu wake wazone yake kutekeleza mikakati hiyo ovu dhidi ya vyama vya Siasa.
Watanzania wa sasa si wale wazidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,wanachanganua mambo kwa kina na kutazama athari kwa jicho kali sana.
Lazima tukemee kwa umoja na mshikamano wetu bila kujali vyama vyetu kwa kuwa mizizi inayosimikwa ina athari kubwa kwa Taifa na inausimika rasmi Utawala wa Kidikitekta.
Ally Mussa Mjema
0748008622