Umoja ni nguvu: Wapinzani nchi hii bila kuungana wasahau kushika Dola

Tunakujua una nongwa na cdm. Kipindi cha dhalimu ulitulia dhidi ya Cdm, kwakuwa ndio chama haswa yule mtu muovu alikuwa anadeal nacho. Kwa maneno marahisi ulifura wao kufanyiwa, hapo hata ww hakukupa furaha. Udini utakulostisha dogo.

Udini vip sasa,kwamba nawachukia chadema kwa kuwa ni wakristo af ccm ni waislam au??

Unajua nyinyi watoto. Wa bavicha akili zenu wote ni kama za mdude tuh,that's why mnatupwa jela mnaishia kushikwa shikwa masaburi na wakulungwa kule
 

Mkuu Joka Kuu,

Nimekusoma.
 

Chadema ingekuwa na position kama ya ACT wazalendo zanzibar,ingeunda serikali ya mseto au ingegoma??
 
Uujngane na Lipumba?
 
Chadema ingekuwa na position kama ya ACT wazalendo zanzibar,ingeunda serikali ya mseto au ingegoma??
Kwa kuangalia issue ya wabunge wa viti maalum unapata jibu wangefanyaje.

Hapa bara walipata hizo nafasi na wamegomea kwa sababu wanasema uchaguzi haukuwa fair, mpaka zikafanyika mbinu za kihuni watu kuapishwa bila kueleweka.

Nitajie vyama serious vya upinzani ambavyo unataka viungane?
 
Wewe umeunganisha nguvu? Why unadhani wapinzani pekee yao ndo wanapaswa waunganishe nguvu? Ungesema wananchi waunganishe nguvu. By the way CCM itatoka soon or later, kwa amani au kwa Shari.
 
Sasa mkuu, bila kuungana wapinzan wa nchi hii wataweza vip kuidondosha CCM?

Mbowe ana miaka 17 yupo hatak kutoka.

Lipumba miaka zaid ya 17 yupo hataki kutoka.

Mbatia na wenzake hivyo hivyo,Mimi nakuambia hawa ni waganga Njaa tuh
Kwani hoja ni kukataa kutoka ama kuungana?
 
Wewe umeunganisha nguvu? Why unadhani wapinzani pekee yao ndo wanapaswa waunganishe nguvu? Ungesema wananchi waunganishe nguvu. By the way CCM itatoka soon or later, kwa amani au kwa Shari.

Wapinzani ndiyo mbadala wa chama tawala,that's why tunatoa Rai kuwa waungane Ili waweze kuitoa ccm madarakan
 
Kwa katiba hii?hata wakiungana na malaika...HAKUNA USHINDI MBELE YA CCM...
 
Mkuu Joka Kuu,

Nimekusoma.

..pamoja na mapungufu waliyonayo wapinzani, lakini ktk kipindi cha awamu ya 5 walifanyiwa mambo mabaya sana.

..katika maisha yangu sikuwahi kutegemea kama nitashuhudia unyama wa serikali dhidi ya wapinzani kama kilichotokea ktk awamu ya 5.

..Na uchaguzi mkuu nao ulikuwa kituko na aibu kubwa. toka lini kukawa na uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi halafu chama kimoja peke yake ndicho kinachopewa nafasi ya kuonekana kwenye vyombo vya habari?

..kwa kweli sijui watu wa vyombo vya habari wanajisikia vipi kwa kile walichokifanya kwa hiari au kulazimishwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

..Na vyombo vya habari ni eneo moja tu, lakini tunaweza kuangazia ktk kada, na taasisi mbalimbali, jinsi zilivyoshiriki ktk dhuluma ile dhidi ya vyama vya upinzani.

..wengine ni viongozi wa DINI ambao waliamua kukaa kimya. hivi kweli kiongozi wa DINI anatakiwa kufumbia macho dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa wapinzani?
 
Unaungana na nani? ikiwa kwa mfano Chadema wanazunguka Nchi nzima kujenga Chama hao wengine wako twita wakisubiri teuzi watu wa hivyo unaungana nao ili iwejr
 
Unaungana na nani? ikiwa kwa mfano Chadema wanazunguka Nchi nzima kujenga Chama hao wengine wako twita wakisubiri teuzi watu wa hivyo unaungana nao ili iwejr
Sawa,lakin hao wengi walioenda kupokea teuzi ni kutoka kwenu,usisahau hilo
 
Ukweli ni kuwa hata wakiungana wote hawawezi kuongoza nchi hii kwa mfumo wa kikatiba na kisheria uliopo. Huo ndiyo ukweli wenyewe na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 

mbna walishaungana na wakachukua na ziada ya ccm ila wap
 

Vyama vya siasa vina itikadi, malengo na sera tofauti. Kazi yao ni kuwashawishi wananchi juu ya ubora wa mielekeo yao hiyo tofauti katika kuchochea maendeleo na ustawi wa taifa.

Hakuna mantiki kwa vyama hivyo kuungana eti kwa lengo moja tu - kuiondoa CCM madarakani. Vikishaungana vitaeneza itikadi ipi? Malengo gani? Na sera zipi? Vitawaaminisha wananchi vinasimamia nini hasa? Kama kweli CCM ndio chama bora kinachokubalika na Watanzania wengi, tatizo liko wapi?

Tatizo la kubwa la Tanzania sio “mabadiliko ya chama tawala tu”. BALI ni CCM kuwa chama dola kilichohodhi madaraka kidikteta na kuhujumu mfumo mzima wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Kwa kutumia vyombo na taasisi za dola, CCM imejihakikishia kukaa madarakani kwa nguvu bila ridhaa ya wananchi.

Kutoliona hilo ni kielelezo cha uongo na unafiki.
 

Kama ndivyo ulivyo, huo utashi wa kuzungumzia siasa za vyama unatoka wapi? Halafu inakuwaje unaotoa ushauri usio na mantiki wala uhalisia? Unataka CCM iondolewe madarakani? Why? Is it sarcasm of sorts?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…