Umoja ni nguvu

Umoja ni nguvu

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Kuna usemi usemao "umoja ni nguvu utengano ni udhaifu" pia ipo moja ya nadharia imetokana na sayansi ya siasa "consequalism" inayoelezea ni jinsi gani utaweza kujua jambo au maamuzi unayoyachukua ni sahihi kwa kutumia kuangalia muitikio wa maamuzi kwa walengwa ikiwa idadi ya wanaokubali maamuzi ni kubwa basi tunasema jambo hilo ni sahihi na ikiwa jambo halitakuwa popular basi jambo hilo ni batili.

Sasa ni upi msingi wa kuandika uzi huu?

Lengo kubwa nahitaji kuweka sawa demand ya katiba kwa baadhi ya watu ambapo asilimia chache wanaona unapobadilika katiba ndiyo itakuwa msingi mkuu wa kupata maendeleo wanayoyawaza ila kumbe sivyo kwani ni wangapi huandika malengo na yakapotelea mbali bila ya kufikwa?

Tanzania ni nchi changa kwa idadi ya idadi ya watu hivyo hali ya uchumi,siasa,na kijamii bado haijapiga hatua ya kimaendeleo kama baadhi ya nchi ila haimaanishi kuwa ni nchi isiyokuwa na maendeleo ila ni Taifa changa kwa umri.

Kumezuka upotoshaji mkubwa wa baadhi ya wanasiasa kwa kuona demand ya katiba mpya lakini wakiwa na shabaha ya kimaslahi kuliko ya kitaifa why nasema hivi? Sababu kubwa kila chama cha siasa ni dola ambayo ndani yake kuna kinga ya mamlaka inayoficha na kulinda kila uovu kwa kutumia vyombo vya kiusalama hivyo kila chama kinavyoingia au kutaka madaraka huwaza kumiliki nguvu ambayo itakuwa favor kwa upande wao.

Vile vile moja ya sifa ya chama hua kinabeba individual interests(matakwa/matarajio) hivyo sio kila wanaohitaji katiba mpya watakuwa wanapata maisha fikiria hili ya kuletewa chakula chumbani hapana bali watamiza expection za hawa watakaoshika dola ila sisi wengine tunakuwa daraja lao la kufikia malengo yao.

Ni ipi njia sasa kwangu? Umoja ni nguvu kama taifa tukubali na kuikubali mifumo iliyopo kwani hata hao wanaosema tatizo ni mfumo wamekulia na kukua ndani ya mfumo wanaosema kuwa ni mbaya "shukrani ya punda ni mateke".

N.B
Katika political system zipo njia nyingi za kushughulikia mahitaji ya wananchi zipo mahakama, na asasi za kiraia nk kwa kushughulikia mambo ya kijamii.
 
Fact. But kidogo unakuja kwakuwa ni maono yako ila kama we sio Ccm utanijibu. Tatizo sio mfumo, Tatizo ni waongoza mfumo... Viongozi wako na Tamaa sio viongozi wa cha tawala au vyama pinzani hakuna kiongozi atakuja kukuletea maendeleo kwako we fanya kazi acha utumwa. Siasa ni mchezo mchafu kila mtu anajali familia yake so endelea kupambana tushaachana na siasa.
 
Fact... but kidogo unakuja kwakuwa ni maono yako ila kama we sio Ccm utanijibu. Tatizo sio mfumo, Tatizo ni waongoza mfumo... Viongozi wako na Tamaa sio viongozi wa cha tawala au vyama pinzani hakuna kiongozi atakuja kukuletea maendeleo kwako we fanya kazi acha utumwa. Siasa ni mchezo mchafu kila mtu anajali familia yake so endelea kupambana tushaachana na siasa.
Exactly tuangalie maisha yetu tuwaachie wanaotuongoza kutengeneza mazingira mazuri kwetu ila tukiendeleza matamanio ya kisiasa tutakuja kuishi kama congo na Libya.

Selfish ndiyo tabia ya kibanadamu.
 
Back
Top Bottom