Umoja Party kikiachana na tabia za upinzani wa sasa kitakuwa chama mbadala

Kweli kabisa. Waache tabia za upinzani. Wawe kama TLP, UDP, nk hapo watachukua dola.
 
Afrika upinzani hawapati madaraka kistaarabu lazima upambane kama hutaki mishikeshike badalisha fani.
 
Wewe ni mpumbavu na dunia inajua kuwa ccm hutumia mabavu kama una akili timamu huwezi andika huu utopolo.
 
Hiki ni chama chetu ambacho kimeundwa nasi wafuasi wa JPM.....
Tunapata wengi kutoka kanda ya Ziwa

Mnaleta ukabila Tanzania. Mambo ya ukabila peleka Kenya. Kanda ya ziwa ninvyama viwili tu CCM na CHADEMA. Jaribu kujifunza kutoka kwa Zitto Kabwe alisema 2015 hakuna chama kitashinda ubunge mkoa wa Kigoma, lakini mwisho wa siku alipata Jimbo moja tu la Kigoma Mjini.
 
Afrika upinzani hawapati madaraka kistaarabu lazima upambane kama hutaki mishikeshike badalisha fani.

Hakuna kitu Kama hicho Africa Ni uroho wa madaraka wa wachache. Sio kweli mbona Kuna nchi zinabadilisha uongozi Bila mapambano?. Kuna Ghana, Zambia, Malawi, cape Verde, Nigeria etc.

Kwanini Tanzania tuchague mapambano ndio tubadilishe uongozi?. Halafu anayepambana na Wenzake ni mwenye madaraka yani waliopo madarakani ndio wanapambana kwa kutumia dola dhidi ya waliopo nje ya madaraka.
 
Sera za umoja party zikoje?

Wao wanasimamia nini mpaka uwape credit za kua mbadala wa ccm??
Kusimamia yale yasiyosimamiwa na upinzani wa sasa inatosha kusema kitafaa kwa matumizi ya baadaye ya mtanzania
 
Tulia na usome kwa makini!
Sisi tutatumia nembo ya JPM
 
Mleta mada na wewe unaamini eti au umoja ni wapinzani wa CCM, basi utakuwa mgeni kwenye siasa za Tanzania.
 
Chama cha wasukuma hiki.
 
Sawa subiri ukabidhiwe madaraka na CCM kupitia kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…