RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,047
- 521
Enyi viongozi wa vyama na wanasiasa,
Nataka niwaambie ukweli mchungu:
Mpaka sasa hakuna chama kilichojipambanua kuwakilisha mawazo ya wananchi wengi,
Kama wananchi watapiga kura 2025 watapiga kura za visilani tu, usishangae hata vyama visivyopata kura nyingi vikapata kura nyingi kuliko wakati wowote.
Lakini ni juu ya wanasiasa kulijua hilo, na kama wanaweza kuchukua jukumu la kuwasimamia wananchi walio wengi basi watazipata kura halali.
Kwa sasa kiasi kikubwa wananchi waliowengi hawana uongozi, wamemeza uchungu na hakuna wakuwatapisha, mnawaangalia kama hamjui kwa kuwa siasa za wanasiasa wengi ni siasa za uongo na wizi zikitanguliwa na sura ya uzalendo kumbe ni ujanja'ujanja tu.
2025 itaongea.
Hawa Umoja Party nilidhani wamekuja kuweka rekodi sawa na kuendeleza uzalendo wa kweli lakini nadhani lilikuwa tawi la wahuni kwa ajili ya kuchota akili za watu na kuwaacha kwenye mataa ikiwa ni jitihada za kuzima harakati halali za kuondokana na uhuni ambazo kwa vyovyote zingeweza kuibuka kipindi hicho.
Nchi inahitaji chama kilicho na wanasiasa wenye mioyo yenye uchungu, na wasiopepesa macho, wawazi na wakweli.
R.I.P JPM ulionyesha njia na legacy yako ipo, ulipendwa na wengi na kuchukiwa na wahuni.
Walioumia katika kipindi chako kimakosa lilikuwa ni jambo lisilokwepeka kwa kuwa ilikuwa ni vita na tulishaelewa hivyo, hata kama mimi ningeumia pia ningeelewa ni ajali vitani.
Maisha yako yalikuwa somo kubwa,
Bwawa lilijaa viumbe wa kila aina, halali na wasiohalali,
Hakukuwa na namna yoyote isipokuwa kulivurugavuruga ili kila mmoja aijue nguvu ya asili inavyofanya kazi.
Ilikuwa kama nyakati za Nuhu ambapo ililazimika kushusha mvua ambayo ilitafuna wema na waovu japo kizazi kingine kilisalimishwa.
Haikuwa bahati mbaya, yalikuwa makusudi ya Mungu kukuleta na kukuchukua,
Somo lilishaeleweka.
Yapo yaliyofanyika maalum kwa ajili ya kipindi cha operation hiyo tu, kwa uwezo na kipawa chako tu, ambayo mwingine hawawezi kufanya na labda hatuwezi hata kuwaelewa kwa kuwa sio muktadha wake.
Watu kama wewe ni baada ya miaka nenda rudi kutokea tena.
Lakini pia kwa kuwa somo lililoachwa na JPM lilisomwa na wenye uchungu na nchi na wahuni, maana yake ni kuwa ajaye hawezi kufanya km JPM kwa kuwa hawatamwacha aende mbali,
Atapaswa kuwa na style yake kama atapenda kuishi kwa raha,
La awe tayari kwa lolote ndio atakidhi mahitaji ya walio wengi.
Awe tayari na ajue ni vita.
Kwa sasa sioni yeyote kati ya waliojitokeza, sioni 🤷
Wapo ndani ya CCM na CHADEMA, wakitaka kujitokeza tunawatambua, maana tunawajua,
Labda ni swala la wakati,
Katiba mpya sawa lakini isiandaliwe ku'intertain wahuni.