Kuna mantiki inapotoshwa kuhusu Chadema na kulamba asali, hasa nichukulie mfano wa viongozi wakuu wawili wa chama hicho, Lissu, na Mbowe.
Nikianza na Mbowe, huyu tunatambua fika madhila yote aliyofanyiwa wakati wa JPM, kuanzia wakati ule DC wa Hai akiwa Mnyeti, huyu alihakikisha anaharibu mashamba ya Mbowe kwa namna alivyopenda, ajabu JPM akampa Ukuu wa Mkoa kama zawadi kwa kazi aliyofanya.
Akaja DC Sabaya, huyu nae alifanya uharibu kwa asset za Mbowe kwa makusudi, tena kinyume cha sheria, alivamia hoteli ya Mbowe usiku akiwa na silaha, akaharibu mashamba yake kwa visingizio tofauti, inawezekana huyu nae alikuwa anakaribia kupewa zawadi ya Ukuu wa Mkoa, kama sio Mungu "kuingilia kati".
Kuonesha Magufuli alivyokuwa na hasira na chuki kwa Mbowe, hata asset zake nje ya Kilimanjaro kama Club Billicanas hazikuachwa salama..
Tukija kwa Lissu, lile shambulio dhidi yake, risasi zaidi ya kumi na sita, lililomuacha na kilema cha maisha ni mfano tosha, hawa watu wanastahili kufidiwa kwa maumivu waliyosababishiwa na utawala uliopita, na wakifanyiwa hivyo, huko sio kulambishwa asali kama wengi mnavyodai, wale wamepewa haki zao, huu ndio uhalisia wa mambo.