Umoja wa Ulaya haupaswi kukubali madai ya Marekani kuhusu sekta ya nishati safi ya China

Umoja wa Ulaya haupaswi kukubali madai ya Marekani kuhusu sekta ya nishati safi ya China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1717054648662.png

Marekani inajaribu kudai kuwa sekta ya nishati safi ya China ni tishio la pamoja kwa wenza wake wa Ulaya, lakini hata hivyo, kujaribu kuiaminisha Ulaya kuunga mkono shinikizo la kiuchumi la Marekani kwa China kunaweza kuwa kikwazo kwa mkakati wa uhuru wa bara hilo la Ulaya. Vitendo vya kujilinda vinavyofanywa na Marekani sio tu kwamba vinaelekezwa kwa China pekee, kama lengo ni kulinda viwanda vya Marekani, vizuizi vinaweza kuibuka katika pwani ya Atlantic.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen hivi karibuni alisema kuwa, Marekani na Ulaya zinapaswa kujibu ‘uzalishaji wa kupita kiasi’ wa viwanda vya China kwa njia ya kimkakati na ya pamoja ili kuwasaidia wazalishaji katika pande zote za Atlantic. Waziri huyo amesema uzalishaji wa China katika maeneo kama magari ya umeme, betri na paneli za umeme wa jua umezidi kidhahiri mahitaji ya dunia.

Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Kundi la Nchi 7 (G7), madai haya yasiyo na msingi ya Bi. Yellen yanaonekana kama onyo kwa wenza wa Marekani braai Ulaya kuhusu kile kinachoitwa tishio linalotokana na maendeleo ya China katika sekta ya nishati safi. Hatua hii inaonekana kama jaribio la Marekani kuzishawishi nchi za Ulaya kuungana nayo katika mkakati wake mkubwa dhidi ya China. Hata hivyo, mtazamo wa Marekani hauendani na ukweli, kwa kuwa mahitaji ya bidhaa za nishati safi duniani yanategemea juhudi za pamoja katika kuchochea mageuzi ya kijani.

Mchango mkubwa wa China katika sekta ya nishati safi duniani unaonekana wazi. Ikiwa nchi inayozalisha kwa wingi bidhaa za nishati safi, China inachukua nafasi muhimu katika kuchochea uvumbuzi na kuboresha matumizi ya teknolojia ya nishati safi. Maendeleo ya kasi ya China katika teknolojia ya photovoltaic, nishati ya upepo, magari ya umeme na betri sio tu kwamba yanatoa suluhisho sahihi na gharama nafuu lakini pia yameongeza kasi ya mageuzi ya dunia katika kupunguza utoaji wa hewa chafu. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati safi duniani, China kuongeza kwa uzalishaji kunatimiza hitaji hili, jambo ambalo ni la manufaa zaidi kuliko kuchukuliwa kama uzalishaji unaopita kiasi. Zaidi ya yote, uwezo wa uzalishaji wa China una uwezekano wa kushusha gharama za teknolojia ya nishati safi duniani, na kuifanya nishati safi kupatikana zaidi na kwa gharama nafuu.

Kwa mtazamo huu, ni rahisi kuona kwa nini Marekani inajaribu kuishawishi Ulaya kudhibiri sekta ya nishati safi ya China. Kwa mtazamo wa Marekani, kudhibiti sekta hiyo ya China hakutakuwa na matokeo ya uhakika na ufanisi bila ya kuhusisha wenza wake wa Ulaya, kwani Marekani inaweza tu kulinda maslahi yake ya kiuchumi na kimkakati kwa kushawishi nchi za Ulaya kuunga mkono mbinu zake za kimwamba.

Hata hivyo, bila kujali jinsi gani Marekani inajaribu kuhalalisha vitendo vyake kwa madai ya ‘uzalishaji unaopita kiasi,’ hatimaye inaonyesha nia yake halisi ya kudumisha mamlaka yake katika mnyororo wa kiviwanda duniani kupitia kukandamiza isivyo halali viwanda vinavyoibuka vya China.

Nchi za Ulaya hazipaswi kuruhusu msimamo wa kibiashara wa Marekani kuelekeza sera zao zenyewe za biashara. Badala yake, nchi hizo zinapaswa kuwa makini sana na hamu ya Marekani kuduisha mamlaka yake ya kiuchumi. Asili ya kujilinda ya Marekani inaamua kuwa, pale linapokuja suala la maslahi yake, nchi hiyo haitafikiria maslahi ya wenzi wake, kwani kuna mifano meingi inayoashiria kuwa, Marekani inaweza kujali tu mamlaka yake na kutozingatia wala kufikiria kuhusu maslahi ya nchi za Ulaya.

Ni kweli kwamba kuna ushindani kati ya China na Ulaya, lakini nafasi ya ushirikiano katika sekta ya nishati safi ni muhimu zaidi ya ushindani huo. Hivyo, ni matumaini ya wengi kuwa, nchi za Ulaya zitagundua nini hasa ni muhimu kwa maslahi yake, badala ya kufuata kama kipofu uongozi wa Marekani katika sera yake kuhusu China.
 
Back
Top Bottom