Umoja wa Ulaya na wenyewe unajiandaa kupitia upya sera ya miasada wanayotoa

Hii ni habari njema.
 
Hii inatisha sana, watu walitegemea maisha yao kwenda kupitia hii, Leo hii watapata wapi mshahara.
Pamoja na hayo kuna waathirika wengi wanaenda kuumia mkuu kama:-
1. Wategemezi wa watumishi.
2. Walio tenda kufanya services za magari kama Toyota, Nduvini and ect.
3. Wamiliki wa hotels ambao walikua wameingia mikataba na mashirika husika.
4. Wafanya biashara na waandaaji wa vyakula/ hafla na vikao.
5. Mzunguko wa pesa uliokuwepo maeneo husika utashuka sana.
6. Watoto wa watumishi wanaenda kupata mkanganyiko wa kuhamishwa mashuleni nakadhalika.
7. Wafaidika wa misaada ya kijamii kama wenye maambukizi ya HIV, Mama na Mtoto, Tohara, Mdomo sungura, Mguu kifundo and ect wanaenda kukosa misaada ama hata kufa kwa kukosa mahitaji ya muhimu.
Hapo ni kwauchache mkuu, list ni ndefu mno...
 
Niliuliza swali kwenye thread kwamba serikali imejipanga vipi, naona Kuna namna moderators hua wanafanya thread isomwe na watu wachache nafikiri Wana hio system, Sasa sjui na wao ni wanufaika wa hii misaada kwamba wamechukia ama vipi
Hii serikali Haina mpango wowote kwa sasa. Kipaumbele kwao ni uchaguzi tu. Hukuona yule mkuu wa wilaya aliyepata ajali kwenda kumpokea m/mwenyekiti!
 
Kabisa
 
Duh! Hili ni janga kweli kweli, Mungu atusaidie katika hili, maeneo mengi Sana yanaguswa
 

Nakumbuka maneno ya rais wa Ufaransa mheshimiwa Emmanuel Macron :



View: https://m.youtube.com/watch?v=IMhp8uPW3og
 
Hahaha "classmate" unawasiwasi tu, acha tujifunze nadharia ya kujitegemea. Mwalimu Nyerere alisema kujitegemea ndio ishara ya uhuru kamili, siyo hii yakutaka kuamuliwa baadhi ya mambo kwa kisingizio cha misaada.
 
Kweli huu mwaka wetu 🙌

Ndiyo ile waswahili husema "Siku ya kufa nyani Kila mti huteleza"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…