Umoja wa wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Wajitetea kuhusu kupanda kwa Sukari. Hawajawahi kuficha Sukari, Si kazi yao kuagiza Sukari nje

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
4,611
Reaction score
5,009
Hali ya Bashe sasa itadhidi kuwa mbaya baada ya Kilombero Sugar kutema cheche

Wazalishaji sukari wavunja ukimya, wadai kutotendewa haki sakata la sukari

Muktasari:

Baada ya kushutumiwa kwa muda mrefu na kutajwa kuwa wao ndiyo chanzo cha kupanda kwa bei ya sukari nchini, umoja wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) wavunja ukimya.


Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi.

Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Pia soma: Mpina kuwapeleka Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria

Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari leo Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Kwa hivyo, waliomba utaratibu wa uagizaji sukari uwekwe.

Pia soma:
Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

Licha ya ufafanuzi huo, itakumbukwa siku chache zilizopita, kulikuwa na mijadala sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye Bunge lililoahirishwa Ijumaa Juni 28, 2024 iliyokuwa ikiwatuhumu wafanyabiashara hayo kuhusika katika kusababisha bei ya sukari kupanda bei.

Baadhi ya watu katika mijadala hiyo walidai wazalishaji wanatengeneza nakisi ya sukari kwa makusudi ili waweze kujinufaisha, jambo ambalo Mpungwe anasema si kweli.

“Kulikuwa na mawasiliano na si mara moja wala mbili, tulikuwa tunakumbushia na kweli ilipofika Desemba hali ikaanza kuwa vile tulivyosema,” amedai Mpungwe.

Amesema cha kushangaza, hadi Desemba vibali vya kuagiza sukari vilikuwa havijatoka na Kampuni ya Sukari Kilombero ikalazimika kuizuia meli yake iliyokuwa inapeleka tani 45,000 ya sukari nchi nyingine na kuagiza iingizwe nchini kwa lengo la kufidia upungufu mkubwa uliojitokeza.

Mpungwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kilombero Sugar, amesema si kweli kwamba kampuni hizo zilipewa vibali vya kuagiza sukari na kuviuza.

Amesema kazi ya uagizaji sukari kutoka nje si yao, wao ni wazalishaji tu na hulazimika kuingilia kati kwenye usambazaji kama kuna uhaba nchini kama walivyofanya kwa lengo la kukabiliana na uhaba na vurugu kama zilizokuwepo.

Pia soma: Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia

“Sisi kama Kilombero hatutaki kuingia katika biashara ya kuagiza sukari, tuko katika biashara ya kuzalishaji sukari, hili wazo la kuweka chombo cha Serikali kuagiza sukari nadhani lingekuja tangu mwanzo tungeunga mkono,” amesema Mpungwe.

Amesema wazalishaji hao waliamua kukaa kimya pale waliporushiwa maneno kwa sababu walikuwa wakiwasiliana na Spika wa Bunge ili wapate nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kilimo na Viwanda, lakini walipangiwa kukutana Agosti, mwaka huu.

“Tulipewa nafasi ya kukutana na kamati ya uchumi na bajeti wiki iliyopita, lakini ilikuwa ni kuzungumzia muswada wa fedha, tulijitahidi kuwa na mawasiliano lakini uamuzi umetoka bila sisi kuhusishwa tumekuwa watuhumiwa hadi tumehukumiwa bila sisi kusikilizwa,” amesema Mpungwe.

Amesema kutuhumiwa kwamba hawawafikirii Watanzania zaidi ya milioni 60 si sawa, kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa unaodumu kwa zaidi ya miaka 60.

“Tumeshutumiwa kuwa sisi ni cartel ni tuhuma nzito katika biashara, huwezi kuwa na mpango mkubwa wa kuwekeza ukajiingiza katika mambo haya na tuhuma hizi haziamriwi kisiasa,” amesema.

Amesema kama kuna hofu kuwa wawekezaji hawa wanacheza mchezo mchafu kwenye biashara, wapelekwe Tume ya Ushindani (FCC), wakajibu tuhuma zao huko.

Naye Mwakilishi wa Bagamoyo Sugar, Hussein Sufian amesema kauli ya kuvitaka viwanda vya sukari kutoficha sukari wakati hakuna kiwanda kilichowahi kuficha sukari, sio sahihi.

Amesema wamejengewa taswira mbaya isiyo na ukweli kwa washirika wa maendeleo ya sekta ya sukari na umma kwa jumla.

Kuhusu dhamira ya kuondokana na uzalishaji sukari nchini ili kuleta sukari ya nje na wakulima kuhamasishwa kulima mazao mbadala kama mpunga, amesema inadhoofisha jitihada zilizokwishafanyika za kuleta utulivu kwenye sekta ya sukari.

Wakati hayo yakisemwa, Sufian amesema pia sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama kubwa za uzalishaji.

“Gharama za mahitaji muhimu kwa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni pia uwepo wa sera zisizotabirika za soko la sukari ni tatizo,” amesema Sufian.

Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba kutaka kujua undani wa malalamiko hayo, akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa; “Ningekushauri kwa hoja kama hizi ni vyema ukaanza na wizara ya sekta husika.”

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alipoulizwa kuhusu barua zilizoandikwa na TSPA aliomba kutumiwa ujumbe mfupi ambao haukujibiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Naibu wake, Joseph Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweri simu zao ziliita bila kupokelewa.
 
The Don Ami Mpungwe 🔥🔥
Huyu mzee namfahamu sana kama balozi na nguli wa diplomasia.

Ameeleza uzuri mambo mengi ambayo watanzania wengi hawayafahamu.

Ila hii video imechakachuliwa kwenye dakika ya 6 pale anapozungumzia udhibiti wa sukari ulianza rasmi lini.

Hapo Michuzi ameharibu na hii yazidi kunithibitishia mashaka na uadilifu wa hawa watu wa media ya Tanzania.
 
Kwa mtazamo wangu, Bashe ameshinda hii Vita, amefanikisha kumtoa nyoka pangoni. Hii ni hofu ya financial bill, Mimi sijaona hoja yenye mashiko kwao, zaidi ya kujitetea kuwa wao sio maharamia Wala so mapapa. Ila kwangu Bashe amewashika pabaya. Amepiga kwenye mshono. Bashe anatakiwa kuungwa mkono na kupewa nguvu.
 
Balozi Mpungwe ni mtu nyeti sana

Kama kuna Waziri kamchezea faulo basi yajayo yanafurahisha 😀🔥
Nafahamu hilo kwa asilimia 102

Kwanza kaeleza tatizo la sukari lilianza lini (December 2023)

Pili, kaeleza hatua walozichukua kujitayarisha (contingency plans)

Tatu, kasema wana mchambuzi au analyst ambae kila kukicha humpa taarifa za hali ya hewa hivyo huwa wako tayari wakati wote.

Nne, Kasema vibali walianza kupewa mwezi Januari 2024.

Tano, kasema Sukari bidhaa nyeti hivyo haiwezi kupakiwa tu kwenye meli yoyote iso na sifa ya kubeba chakula.

Na pia kawashauri watu wa media wakasome tena waelewe maana ya neno Cartel maana lina maana yake mtambuka.
 
Back
Top Bottom