Usiwape China sifa mbovu kwa kutoelewa kwako.

Hapo ingekuwa ni China, huyo mama 'Chura Kiziwi' asingekuwepo kabisa katika nafasi hiyo, na kama angetokea kuwepo, huyo ndiye angekula hiyo risasi unayoizungumzia hapa.

"Kutetea ujinga" ni kujuwa kwamba kuna 'cartel', badala ya kutumia sheria/taratibu zilizopo, huyo "mjinga" anavuruga taratibu hizo na kuvunja sheria mwenyewe kwa kugawa vibali kwa mashemeji na ndugu zake nje ya taratibu.

Sukari kuuzwa Tsh10,000/ hiyo ni kazi ya Bashe na kundi lote linalomsaidia kutafuta hela za kuchafua chaguzi zijazo. Zile za waarabu zinatafutiwa hizi chache za kuzifunika zisionekane bayana.
 
Tatizo lako wewe ni kuona kila Jambo ni la kiuchaguzi tu. Kwahiyo wewe ndio kiziwi zaidi maana hutaelewa, lakini usilazimishe uelewako kwa Watanzania wote. Sisi tunaakili timamu tunajua kutazama Mambo jwa jicho la tatu. Na sio wewe utulishe mitazamo yako hiyo haikubaliki. Unafikiri kwanini Hadi muda huu viongozi wote wa vyama mbadala hawajazungumzia Jambo Hilo?
 
sasa wangezalisha sukari ya kutosha na bei nafuu hao mashemeji unaozungumzia wasinge jaribu hata kuomba kibali cha kuingiza juice embe, isitoshe hao wote nyani mtini wanaruka tawi moja kwenda jingine kutuchanganya akili
 
Kabisa hiyo ni Cartel, ndio hoja yangu hapo. Wao ni sawa tu na OPEC na wanafanya Yale Yale ya OPEC, Wana cutt production ili kutengeneza shortage na kuongeza Bei kupata supernormal profit. Ni Yale Yale waarabu wanafanya kwenye mafuta.
Mkuu rejea kwa yule mkulima- una cut production ya muwa wa sukari kwa kutumia njia gani- nasubiri jibu lako mkuu
 
Mkuu rejea kwa yule mkulima- una cut production ya muwa wa sukari kwa kutumia njia gani- nasubiri jibu lako mkuu
Kaka unachanganyq mada, yule mzee ni mzalishaji wa sukari na hakuna mkulima wa miwa aliekuja kwenye ile press. Sasa mbona tunaongelea kitu ambacho hakipo pale. Kwani Kuna sehemu serikali imezungumzia kuwa hawatazalisha sukari ndani au wale watu wasizalishe. Issue ilikuwa ni gap sugar na namna hatua serikali walizochukua kushughulika na hiyo issue. Sasa mkulima wa miwa ulimuona pale na alizungumza Nini? Labda wewe uniambie mkulima wa miwa pale kwenye press alizungumza Nini.
 
sasa wangezalisha sukari ya kutosha na bei nafuu hao mashemeji unaozungumzia wasinge jaribu hata kuomba kibali cha kuingiza juice embe, isitoshe hao wote nyani mtini wanaruka tawi moja kwenda jingine kutuchanganya akili
Kwani imeelezwa popote kwamba hao wazalishaji walikataa kwa maksudi kuzalisha sukari nyingi. Hili wewe umelitoa wapi. Hukusikiliza yaliyoelezwa kwenye hizo picha?

Watazalisha vipi kwenye uwezo, wakati viwanda vyao havijafikia ngazi hiyo? Hivi watu wengine mnatumia akili kufikiri kweli?
 
Iangalie yote- mie nilinuona mkulima pia baada ya yule mtu wa Bagamoyo Sugar
 
Iangalie yote- mie nilinuona mkulima pia baada ya yule mtu wa Bagamoyo Sugar
Kaka pitia taarifa ya bodi ya sukari kwenye press ya leo, yapo Mambo utajifunza. Kaka Mimi ni mkulima wa kawaida huku Newala Ila najifunza kuwa baada ya Jambo kutokea usitoe judgement ya Mapema. Maneno yakishatamkwa hayawezi kurudi Tena mdomoni. Ziko hoja Zina mashiko lakini wale jamaa ni Kama mwamba ngoma tu. Tazama press ya bodi ya sukari please.
 
Mkuu nimewasikiliza mwanzo mwisho.
 
Kwa hiyo free art ni kama ukahaba wa kiuchumi na biashara yote yaliyo haramu na halali yana kuwa ruksa ndiyo maana nikakuambia kuwa dubai ni danguro la ufisadi duniani
 
Kazi ya Mungu haina makosa.

Cartel mama na Bashe wameivuruga. Na bado.

Waambie kuna mabaniani wa sukari kutoka Uganda wapo Tanzania, waliulizwa vipi huko sukari rahisi Tanzania ghali, wakacheka tu, wakasema Tanzania sukari inatakiwa iwe bei chini sana kuliko Uganda. Sasa hivi wanatafuta sehemu ya kuweka mashamba makubwa. Hapo hiyo cartel ya kijinga ndiyo wataelewa nini maana ya kuwatumikia wananchi.
 
Kwa hiyo free art ni kama ukahaba wa kiuchumi na biashara yote yaliyo haramu na halali yana kuwa ruksa ndiyo maana nikakuambia kuwa dubai ni dabguro la ufisadi duniani
Vyovyote uonavyo, "cartel" ya sukari imekumbana na Msomali, imebamizwa.
 
Mara hii umekwisha sahau 'NONSENSE' aliyopewa Profesa, tena Profesa mwenye heshima, anaambiwa 'nonsense' na mtu ambaye elimu yake inatia mashaka sana!
Huu 'uchawa' wenu, kwa sababu zenu mbalimbali mnaoutumia kulaghai watu mwishowe utagonga ukuta tu. Hamuwezi kumpaka wanja na hina nguruwe halafu mje hapa kuwaambia watu bibi harusi kapendeza!
Nguruwe atabaki kuwa nguruwe tu siku zote.
Hebu tuelezeni hao mliowapa vibali vya kuagiza sukari mliwapata wapi na kwa njia zipi?
 
"Profesa" wa kutunukiwa UDSM?

Usilete utani bana, si tumewaona ma profesa wanavyotetea hoja zao kwenye mahakama ya Kimataifa?

Si kila profesa inamaanisha kaelimika, maprofesa wengi walisomea ujinga.
 
"Profesa" wa kutunukiwa UDSM?

Usilete utani bana, si tumewaona ma profesa wanavyotetea hoja zao kwenye mahakama ya Kimataifa?

Si kila profesa inamaanisha kaelimika, maprofesa wengi walisomea ujinga.
Kama wewe una mashaka na profesa huyo, nitahitimisha leo leo kwamba elimu yako ni mbovu kabisa kutojuwa profesa wa kweli.
Najuwa "ulevi" umeteka akili yako, lakini mara moja moja, kama nilivyo shuhudia hivi karibuni humu humu JF, nategemea ukauweka pembeni ulevi huo na kutumia akili halisia uliyo nayo.

Lakini sita shangaa iwapo hujui kutambua Profesa wa ukweli, na hao wa michongo, ambao nakubaliana na wewe wamejazana hata hapo UDSM. Hali hiyo tuwashukuru CCM kwa kukigeuza Chuo Kikuu hiki kuwa "Jalala".
Sasa hata Ph.D za Heshima ni za kugawa tu bila kujali sifa na uwezo alio nao anaye tunukiwa. Kila kitu ni siasa sasa!
'Chancellor wa chuo mwenyewe si ndiyo huyo, utategemea kitu gani hapo?'
 
Kanjanja tu huyo.

Ameifanyia nini cha maana Tanzania?
 
Kanjanja tu huyo.

Ameifanyia nini cha maana Tanzania?
Katika hali iliyopo Tanzania sasa hivi unategemea 'msomi' yeyote afanye lipi la ziada? Kazi iliyo baki ni kujisalimisha kwa hawa viongozi wasiokuwa na kitu kichwani ili na wao maprofesa waambulie uchafu wanaofyonza kutoka kwa hao viongozi.
 
Unapokuwa na 'mungu' unaye muumba ndani ya akili zako mwenyewe, kwa hakika 'mungu' huyo hawezi kufanya kazi yoyote ambayo utaiona wewe kuwa na makosa.
Hapana Mungu apasaye kuabudiwa isipokuwaa Allah.

Kumbuka hilo.
 
Katika hali iliyopo Tanzania sasa hivi unategemea 'msomi' yeyote afanye lipi la ziada? Kazi iliyo baki ni kujisalimisha kwa hawa viongozi wasiokuwa na kitu kichwani ili na wao maprofesa waambulie uchafu wanaofyonza kutoka kwa hao viongozi.
Mapriofesa wapo Havard, Princeton, Oxford. Hivi vi profesa uchwara ya Tanzania hata kujieleza vinashindwa na vyo unavihesabu?

Si japo angetajwa Profesa Assad, ameiteteemesha serikali nzima kutokea Umoja wa Mataifa, na hajakaa bila kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…