Swala LA sukari inaonekana Kuna mambo mengi nyuma
Wapigaji wameingia kwenye suala la kuagiza sukari kutoka nje.

Hilo bila shaka yoyote litawezesha kuingiza nchini sukari ilokwisha muda wake na isofaa kwa matumizi ya binadamu.

wauza vouchers ni wapigaji.

Wazalishaji wa sukari ni lazima walindwe na serikali wahitaji sana hiyo kinga ili kuwasidia kufanya biashara yao bila shida.

Huwezi kujenga kiwanda kama cha Bagamoyo Sugar ambacho mzee Bakhresa kaamua kuwekeza na hapohapo wakandamiza wazalishaji wa ndani.
 
Kasema nini huyu mwamba ? Niko kazini sina earphones.Tatizo Spika Tulia bunge haliwezi.

Tofauti ya Tulia na kina Mkwawa, Msekwa, Sitta, Makinda ni kwamba wale

1/ hawakupewa U-Spika na mamlaka za nchi

2/ walitokea sehemu nzito serikalini ambako walishajijengea heshima na hivyo hawakuiogopa serikali

Ndugai hakutokea serikalini lakini alishakaa bungeni miaka lukuki kabla, marais wa nchi kanywa nao chai maandazi kantini za bunge, hakuwaogopa sana, alishajijengea hadhi, uhuru na uwezo japo kiasi, na Uspika alipendekezwa na wabunge wenzie, hivyo hakujiona kama ni zao au kijakazi cha serikali.


Tulia kaokotwa "jalalani chuo kikuu," kalala mwalimu, masikini kapuku, kaamka spika wa nchi ya watu milioni 60. Kwa hiyo ni mnyenyekevu, mjipendekezi, obsequious, lap dog, mbwa wa mapajani wa mamlaka zilizomtoa jalalani, ana deni. Ndio maana anachemka. Hata taaluma ya sheria kaweka pembeni.

Mpina kamchambua uwezo wake mdogo wa kisheria, kasema kifungu alichotumia Spika kum punish kimeandikwa ni sheria ya vyombo vya habari vinapo cover bunge, sio mbunge anapoongea mitaani. Na Tulia alipojisikia kakosewa na Mpina, alipaswa kumuachia kiti Azzan Zungu ndio aseme Mpina apelekwe Kamati au apeteshwe. Lakini Tulia akasoma mpaka na hukumu ambayo Mpina atapewa akikutwa na hatia. Tulia Ackson is worst speaker in history of the legislature.
 
Mpaka sasa nimewasikiliza kwa dakika 30, naendelea kuwasikiliza lakini cha kusikitisha wanaongelea siasa na porojo nyingi. Kuwa "watazalisha" sukari ya kutosha kuanzia mwaka huu.

Pambaf kabisa, walikuwa wapi siku zote mpaka Bashe kaja kuwatia vidole vya masikio ndiyo wanasikia kuwa Watanzania wameathiriwa na bei za sukari?

Hawa wazalishaji hawatakiwi kutupigia porojo, wanatakiwa wazalishe sukari ishuke bei.

Ujinga mtupu.
 
Faiza kuna wakati unakuwa na akili kwel, hata kama Bashe kakiuka sheria kutatua swala hili, ila ninachoamini ni kwamba kawapiga kwenye mshono, walikuwa wanajiona miungu wantu
 
Faiza kuna wakati unakuwa na akili kwel, hata kama Bashe kakiuka sheria kutatua swala hili, ila ninachoamini ni kwamba kawapiga kwenye mshono, walikuwa wanajiona miungu wantu
Ila angeruhusu waagizaji wenye hadhi inoshabihiana na wao isingekuwa shida.

Mbona wakala wa taifa wa chakula yupo angepewa jukumu hilo la kuaguza sukari ndo ingekuwa ni bora zaidi.

Kwanini wauza vouchers wapewe jukumu la kuagiza sukario na si jukumu lao?

Bodi ya sukari ipo je imekwama wapi?
 
Hili suala limenifanya nimkumbuke spika wa Bunge la Marekani Newt Gingrich.
 
Kwa hiyo Mpina alikuwa sahihi, na Bunge lote lililopiga kura kumuengua walikuwa ni mbumbumbu
 
Mkuu ndio maana nimesema, kakiuka sheria, angalau siku nyingine tutaheshimiana
 
Kwa hiyo Mpina alikuwa sahihi, na Bunge lote lililopiga kura kumuengua walikuwa ni mbumbumbu
Njia ipi ilitumika kuwapata waagizaji binafsi wa sukari kutoka nje ya nchi?

Kama haikuwepo njia ya kihalali ya kuwaruhusu waagizaji halali, je njia hiyo ilitengenezwa lini?

Kwa mfano, kampuni ya Zenj general merchandise ltd ilipewa kibali kuagiza tani za sukari 6000 April 2024 kwa misingi ipi?
 
Asee unamponda hadi ami Bahalesa kweli ustaadhat
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…