Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Mimi ushauri wangu mtoto akifiia secondary school mnunulie laptop na siyo smartphone.Smart phone na social media haviepukiki katika dunia ya leo. Moja ya faida ni kuelimisha, kuna binti wa miaka 10 aliweza kuandaa period pack yake kabla hata ya kupevuka kutokana na uwelewa alioupata kutoka kwenye Internet. Hii ni moja ya faida chanya za social media.
Watoto wanapata habari nyingi mno na nyingine ni hatari kwao kufahamu, kutokana na uwezo wao wa kupambanua mambo. Maisha ya sasa hivi yalivyo hata usipomnunulia mtoto simu, kuna ndugu na marafiki wa karibu watakao waza zawadi ya simu kwa birthday au sikukuu ya dini.
Ni umri gani ni sahihi kumruhusu mtoto kuwa na simu hii na ni jinsi gani unaweza kumlinda?
Kama kutakuwa na ulazima wa mawasiliano mnunulie simu ya kitochi.
Wengi mtashangaa sana why laptop na siyo smartphone na gadget zote hizo zina access Internet ila ukweli nawaambia smartphone zinatia ujinga zaidi hawa watoto, lakini laptop ina tofauti kubwa sana na smartphone.