Sina bando ujumbe unasemaje?
Halafu mimi bado sijafika Menopause km unamaanisha hivyo..!!
Akinadada wengi hudhani menopause ni mpaka ufike 49! Hiyo kitakwimu tunaita wastani. Kuna early menopause ambayo mwanamama anaweza kuipata akiwa chini ya hapo au late menopause akiwa hata zaidi ya 60.
Nina mifano hai kutoka kwa watu wangu wa karibu. Mama yangu alipata bahati mbaya ya kupata early menopause akiwa na umri wa miaka 35. Hiyo kitu ilileta kizaa zaa katika familia yetu.
Imagine baba alikuwa anamzidi miaka 3! Na huko kwetu kusini Vijijini elimu ya hizo wakati huo ilikuwa bado. Ilikuwa kivumbi na jasho, nguo kuchanika. Nakumbuka nikiwa mdogo just 8 years nilimkabili baba na kumuuliza: Kwanini ikifika usiku, anampiga mama? Yeye kwa upole, alinijibu; wewe bado mtoto, ukikua na kuoa utaelewa. Hilo neno lilinikaa kichwani sana. Namshukuru Mungu nilipata bahati ya kuongea naye kabla hajafariki kuwa Nisamehe nimeyaona. Wewe unafikiri Kwanini tunawafukuzia?
Late menopause Mfano ni mkwe kwani boss wangu alizaliwa akiwa na umri wa miaka 56 ingawa yeye ni last but one.
Hitimisho: siyo lazima ufike miaka 50 ndipo upate menopause, hizo ni nadharia za vitabuni but in real life inategemea mtu na mtu na Mazingira aishimo.
Samahani kwa majibu marefu, ni ugonjwa unaotokana na profession zetu. Maana topic hizo ndizo zimetukuza na kutufanya tuifahamu JF