Umri umeenda: Nahitaji mchumba aje awe mke mwenye sifa hizi ndani ya mwaka huu

Umri umeenda: Nahitaji mchumba aje awe mke mwenye sifa hizi ndani ya mwaka huu

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Habarini ndugu zangu, kaka na dada zangu. Kiuhalisia leo naandika huku nikiwa nimejawa huzuni, majonzi na sononeko kubwa sana moyoni.

Nikitizama umri wangu kwa kweli umeenda na mpaka sasa sijashika mwenza wa kusema huyu ni wangu nami ni wake. Nimechoka maisha ya kuhangaika na wanawake nimewaza week nzima maisha ninayo ishi najikuta nakosa kitu muhimu sana.

Nmeamua kubadilika kuwa mtu mwa nami sasa nahitaji wife. Seriously nahitaji mwanamke ambaye tutapendana.

Sifa zake ziwe ni hizi;
1. Asiwe mlevi kama anakunywa basi iwe kiasi tu kwa hamu
2. Awe na elimu ya kuanzia kidato cha sita na kuendelea. Asiwe alifail kidato cha sita.
3. Awe tayari kupima afya kabla hatujaanza mahusiano.
4. Awe na rangi yoyote ile ya asili asiwe amejichubua.
5. Awe na umbo maridhawa asiwe mwembamba sana, awe na umbo lilolojigawa na pia anayependeza.
6. Anipende kwa mapenzi ya dhati asiwe na hasira, matusi kwangu au kwa mtu yeyote.
7. Kama ana mtoto then mtoto wake asizidi miaka 5. Na nipate uhakika ameshaachana na baba wa mtoto kabisa. Mimi nina mtoto mmoja so tunaweza ongeza mmoja pia. Ampende mtoto wangu asimtese.
8. Awe na kazi kama hana awe tayari nimfungulie biashara atayoiweza ila baada ya kuwa tuna uhakika wa kuishi pamoja. Awe tayari kubadilisha ID aliyokuwa anatumia humu ndani.

9. Awe msafi wa mwili na roho, asiwe mchoyo na mwenye dharau. Ajipende avae apendeze niende naye popote pale na pia aweze kukutana na rafiki zangu ambao wengi ni wazungu so ajue lugha ya kiingereza.

10. Awe na mapenzi ya dhati kwangu, awe na akili za kiutu uzima za maendeleo na kutunza family hasa napokuwa nimesafiri.

Umbo lake naomba tafadhali liwe la mvuto maana sipendi niwe na mwanamke halafu nianze tamani wa nje. Ajiamini na ajione yu mzuri, aweze kunimiliki na kuniona mimi ni mali yake kama yeye alivyo mali yangu. Mwepesi kusamehe na mwenye kunikosoa na kunifunza. Kama kuna mtu tupo serious naomba tuwasiliane naye pembeni tuanze na urafiki kwenye simu na baadaye tuonane. Awe Dar maana ni rahisi zaidi kuonana naye.

Nimeandika haya kwa udhati wa moyo wangu sijashinikizwa na mtu na wala simjaribu mtu. Naombeni sana mnisamehe kwa mengine yote ya kale.

NAHITAJI MCHUMBA.
 
Kila la kheri, ila hiyo avatar itakukosesha warembo.!!!
 
Naomba niulize swali: Unataka kuoa kwa sababu tu unaona umri umeenda!?
 
Hahahaha...sasa umri umeenda wahitaji mwenza na uko na mashart mia kidogo....utampatia wapi mkamilifu mwenye vigezo vyote ivooo hahahahaha...coz naamin hata yeye akakupa masharti yake mengine huto yaweza
 
Usiangalie umri Mkuu Oa kwasababu muda wa kuoa umefika sio umri umeenda.

Kila la kheri
 
Daaah.. mara ya kwanza nasoma mwandiko wako ukiwa serious. Naamini utakuwa unamaanisha ulichokiandika
 
yupo mmoja inst anajiita Sanchoka ni mrembo mwenye umbo zur alitangaza ukiwa na mil10 tu anakubal kuolewa
 
Back
Top Bottom