Nahitaji mwanamke wa kuoa maana nipo mpweke sana na nahitaji mtu ambaye tutaishi naye ili kujenga familia na kuwa na watoto kwaajili ya maisha ya baadaye.
Naomba kuwasilisha....
naegemea kipande hiki ndugu , kusema unahitaji mke kwa sababu uko mpweke ni kama unajiongopea ndugu yangu!
unaweza kuwa ndani ya ndoa ukawa mpweke kuliko unavyotarajia na nmna yakufanya hautakuwa nayo tena.
nazungumza hivyo kwa sababu mimi nina ushahidi wa hilo ndugu.
ndoa haihitaji kikisingizio chochote ili iwepo, sijui upweke ama kuongeza familia ,kupata watoto ,ama furaha ama kupata wepesi wa maisha au kuongeza kipato nknk, ukitumia sababu hizo kuingia kwenye ndoa utakutana matokeo yalio tofauti na matarajio.
tulia kwanza, fanya upembuzi yakinifu, jipange, tena jipange haswa, hakuna namna utakayo kwepa majukumu kama mwanaume hata kama huyo mwanamke angekua na hela kiasi gani! kwanza sijui kama wanawake unawajua vizuri ndugu yangu, hela yao haliwi na mwanaume!
utanyanyasika mpaka uombe poo!!!
jipange , maana utafika kipindi mpaka ngua ya ndani utashindwa kununua brother!
japo najua badiko hili haumaanishi lakini ukweli ndoa nikama hivyo nakuzidi, lakini pia inaweza kuwa kinyume chake, kila jema.