Umri Upi ni Sahihi kwa Mtu Kustaafu kazi?

Umri Upi ni Sahihi kwa Mtu Kustaafu kazi?

Marumeso

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2009
Posts
1,410
Reaction score
1,325
Wakuu tujadili umri sahihi kwa mtu kustaafu ni upi? Awe ni mtu binafsi anayefanya shughuli zake mwenyewe au za kuajiriw na kama ni lazima uwe na hela za kutosha kwanza ndio uamue kustaafu.
 
Umri sahihi kwangu sio umri sahihi kwako. Ila ni vema mtu akajipanga akastaafu mapema iwezekanavyo.
 
fanya kazi Hadi umri wako kisheria ustaafu ufike kipindi ukiwa kazini jitaidi ujiwekeze kivyovyote ili uikistaafu unaendeleza ulichowekeza maisha hayana mapumziko pigana kadri uwezavyo kutimiza matarajio yako Aya Mambo ya kustaafu mapema ilisijui ufanye nn ni mitizamo tu
 
Wakuu tujadili umri sahihi kwa mtu kustaafu ni upi? Awe ni mtu binafsi anayefanya shughuli zake mwenyewe au za kuajiriw na kama ni lazima uwe na hela za kutosha kwanza ndio uamue kustaafu.
Umri wa "kifo"kama waujua ndipo unapotakiwa ujistaafishe kazi uingie huko ambapo hutadai ugali Wala dagaa !!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Piga kazi kadri uwezavyo..fanya investment kadri uwezavyo..kisha ukiona miradi inaingiza pesa mara tatu ya mshahara wako.piga kazi kasimamie miradi yako.
 
Kuna kustaafu kuajiriwa na kuna kustaafu katika ajira uliojiajiri; Kustaafu katika ajira uliyojiajiri inaweza kuchukua muda mrefu, mpaka pale mwendelezaji atakapopatikana; ila kwa aliyeajiriwa, ni vizuri ustaafu mapema ili ukasimamie miradi yako.
Nb: Hakuna tajiri aliyeajiriwa
 
Bakhresa kwa umri n ukwasi alionao, bado hajastaafu.

  • Bill Gates bado anazichanga
  • Malkia yupo tu!
  • Museven hataki kabisa kusikia kuhusu kustaafu
  • Biden ndo kwanza anasuka mipango ya kupiga term ya pili.
  • Lipumba karudi, mwalimu wa Samia akiwa sekondari, kateuliwa
  • Majaji wastaafu wanateuliwa, maraisi na watumishi wa govt waliokuwa vigogo wastaafu wanapewa teuzi, sijui maana ya kustaafu hapa!

Ukiniuliza umri sahihi wa kustaafu, haupo, serikali yenyewe haiujui!
 
Ujisikiapooooo,
Umri UPI sahihi kuoa/olewa..... Ujisikiapooo
 
Back
Top Bottom