Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Umri wa kuanza darasa la kwanza uanzie miaka 10, sababu hizi hapa

Mwanafunzi ya zamani vijijini ilikuaga hivyo unakuta mmama yuko std iv....pia bonge ya jitu shabab lipo std v na midevu. Nakumbuka hayo yalikuwa hayachapwi! Ma ticha walimalizana nao kimya kimya ki utu uzima pembeni! Hata likichelewa shule asubuhi no fimbo
 
Mleta hoja upo vizuri sana, Ila miaka 7 kwa la Kwanza ni mizuri Ila form 5 na 6 ndo ziondolewe wakimaliza form 4 waende kwenye elimu ya kujitegemea chuo au stadi za kazi hiyo 5 na 6 ndo inawapotezea watoto kupata taaluma zao wakiwa wanahangaika na academy.
 
Labda uongezwe na muda wa kustaafu

Nenda English medium kuna watoto eleven years anamaliza la saba

We Chelewa na mwanao utamchelewesha kila kitu hata scholarship na ukijeba wake hapati
Tatizo napomaliza chuo akili mnazielekeza kwenye kuajiriwa wakati mnaambiwa kazi hakuna. Hata hivyo tunaweza kupunguza madarasa tubaki la kwanza Hadi la Sita, form one mpaka form three form five Na six wakajifunza mafunzo ya Veta Tu ndipo huingia chuo kikuue nako mtu amalize degree moja sio kuwa Na madegree mengi kama let mutuz Alafu ayafanyi kitu
 
Mods naomba kubadirishwa headinge,isomeke la kwanza badala ya la saba
 
Pumba ndiyo maana wengine bado mko slow mpaka leo. Mtoto anatakiwa kuanza kufundishwa akiwa na miaka 5 na la kwanza miaka 7 sasa kama wengine wana lishe ni tatizo la kimasikini sio akili ya mtoto. Umasikini wetu tusipeleke kwa watoto. Lishe tatizo wakati tuna mashamba! Tukitaka wengine kuwekeza kwenye kilimo wanasema tunachukuwa maeneo makubwa , ukiwapa wananchi hakuna lishe. Hili ya miaka 10 ni wazo la kuchekesha mwandishi inaelekea upeo kidogo ni tatizo
 
Mtoa mada, andiko lako halina scientific backing.
Mtoto yeyote ambaye hajadhurika ubongo wakati wa mimba na wakati wa kujifungua,
Brain development hukamilika akifikisha miaka 5.
So hapo mtoto anatakiwa kuanza kujifunza.

Sky eclat asante kwa mchango wako.
 
Miaka 10 niko darasa la 5 we ndo unasema ningekua la kwanza??

No wayy..
La kwanza ni miaka 5 siku hizi
 
Ili uweze kuanza darasa la saba ukiwa na umri wa miaka 10 inabidi uanze darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka 3. Jamaa nadhani anaongelea ndoto aliyoiota leo usiku.
 
Wana JF

Makuzi ya binadamu wa mtanzania yanapitia magumu mengi, hivyo pia akili uchelewa kukomaa kupota uelewa wa kujifunza kitu Kwa umakini. Natoa sababu Kwa nini umri miaka 10 ndio unafaa mtoto kuanza la Saba.

1. Umri ukiwa miaka kumi mtoto anakuwa amekomaa, huondoa woga na anaweza kuhoji kama kitu sio sahihi.
2. Waliokosa lishe bora huwa ndio wakati ambao makuzi ya akili yanakuwa sawa.
3. Mtoto hadanganyiki kirahisi na akifanyiwa vitu vya unyanyasaji wa kijinsia ana uweza wa kumweleza mama yake au baba yake.
4. Ni umri ambao vipaji uchipuka mtoto kujua anapenda nini Na ana kipaji gani.
5. Kutokukubali kuonewa na mtu yeyote Kwa kuwa sio mwoga.
6. Urahisi wa kuweza masomo walimu hawapati shida.
7 . Kama shule ipo mbali huyu ndiye mwenye uwezi wa kutembea umbali mrefu.
8. Akimaliza darasa la saba anaweza kusaidia shughuli za kilimo au kuanza kujitegemea
9. Hauhitaji kumlea kama mtoto ikiwa hakufaulu kuendelea na masomo.
10. Kutokana na umri anakuwa amepunguza michezo mingi hatarishi kwa kuwa tayari ana uelewa

Kumbukumbu zinaonyesha wengi waliofanikiwa wengi walianza shule wakiwa na miaka 12.
Mimi mwenyewe nilianzishwa nikiwa na miaka 10, nilikuwa nawafundisha wale wadogo
 
Mkuu tatizo sio umri, tatizo ni malezi tunayowaalea watoto wetu.

Mtoto shule anafundishwa kuwa ndioo mzee hata kama ana maswali ya kuuliza.

Kaa na watoto wako jadiliana nao taratibu mambo mbali mbali ukiwauliza maswali na kuwapa challenge ndogondogo wazitatue.

Nimetumia njia hii kwa mdogo wangu anaenifuata watu wanashangaa dogo namleeaje mbona amekuwa kama mtu mzima na kwanza yuko form two anaonekana ana uwezo wa mtu wa miaka 25.

Ishu ni malezi kaka
 
Mimi ni mmojawapo wa walioanza la kwanza na miaka 10.

Sio kwamba sikuwa na akili, bali tatizo ni ufupi na mkono ulikuwa mfupi nikiambiwa shika sikio la upande wa pili siwezi.

Toka nina miaka 7 naenda kuanza la kwanza lakini narudishwa.

Wote walionifanyia unyama huu nimewasamehe, nyambafu zenu.

Unforgetable
Heshima yako bosi Andunje.
 
Kuna research ilifanyika baada ya ongezeko la watoto wenye Attention deficit hyperactivity disorderADHD Marekani kuwa kubwa kulinganisha na nchi za Ulaya.

Waligundua kuwa watoto wa nchi za Scandinavian hupata muda mwingi wa michezo katika elimu ya awali. Elimu hasa huanza mtoto anapofikisha miaka 5.

Miaka 10 ni kumchelewesha mtoto, huu ni muda mtoto anajiandaa na mitihani ya kumaliza shule ya upili, anajua kuandika insha, hesabu za kujumlisha, kutoa, kugawanya kuzidisha na percentage hata algebra.

My point is kumuwahisha sana mtoto shule kuna hasara hali kadhalika kumchelewesha.
Kwa hiyo umri sahihi zaidi ni upi?
 
Unamaanisha huyu kibonge wangu nimpeleke la kwanza
 
Mwanangu kwa uwezo Mungu aliompa yuko darasa la 7 akiwa na miaka 10..kuna madarasa matatu huku chini hakusoma..kuna wakati namhurumia sana lakini darasani yuko vizuri na tayari seminary moja wameshasema watamchukua akaanze form one.. kichwani yuko gado sana japo anapozewa ugali na uji mpaka leo..
 
ndio ni mzee Ulaya hata Nigeria hapo huo umri mtu anakuwa na Phd tayari sio kidigrii cha kwanza
Juzi nilikua naangalia makala flani ya Nigeria nikaona mdada anasema 16 yrs mtu yupo university.. hii imekaaje mfumo wao wa elimu ukoje?

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi ni mmojawapo wa walioanza la kwanza na miaka 10.

Sio kwamba sikuwa na akili, bali tatizo ni ufupi na mkono ulikuwa mfupi nikiambiwa shika sikio la upande wa pili siwezi.

Toka nina miaka 7 naenda kuanza la kwanza lakini narudishwa.

Wote walionifanyia unyama huu nimewasamehe, nyambafu zenu.

Unforgetable
Mkuu umemliza la 7 na miaka 17........ila form one itakuwa hukupiga simu chooni maana hata form 2 walikuwa wanakuamkia
 
Mwanangu kwa uwezo Mungu aliompa yuko darasa la 7 akiwa na miaka 10..kuna madarasa matatu huku chini hakusoma..kuna wakat namhurumia sana lkn darasan yuko vizur na tayar seminary moja wameshasema watamchukua akaanze form one..kichwan yuko gado sana japo anapozewa ugali na uji mpaka leo..
Hata moto wa bro....mwaka huu kaanza form one na miaka 11, madarasa matatu primary hajasoma
 
Waanze na miaka 5 kwa serikali, watu wasihangaike kupeleka vitoto vyao English Medium.......
 
Back
Top Bottom