LGE2024 Umtakaye kaenguliwa piga Kura ya HAPANA

LGE2024 Umtakaye kaenguliwa piga Kura ya HAPANA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kura za HAPANA zinaweza kushinda kama anawekwa mgombea asiye na sifa zinazohitajika na wapiga kura.
Hatusemi wagombea wote wa CCM ni wabovu, hapana wapo wagombea wazuri na hao tutawapa kura bila kujali chama chao. Lakini kama kaenguliwa mgombea makini wa mtaani kwetu ili wasimamishe bumunda ambalo mtaani twajua ni bumunda hakuna kucheka na hawa mumiani ni kutwanga HAPANA tuu na kuisimamia kwa dhati.
 
Tatizo linakuja kwa kuwepo mfumo wa kuahirisha kufikiri, a.k.a, kujizima data. Mungu aipe maono jamii yetu kuweza kujua hujuma zilizoko kwenye chaguzi zetu
Uchaguzi wa serikali ya mtaa unazihusu hasahasa familia zetu na tunajuana vyema.
Ni jukumu la kuwaambia na kuwakumbusha wanafamilia yako ubaya wa kumpigia kura kiongozi aliyekuwepo na anataka tena wakati amewasumbua kwa kutaka rushwa, uwajibikaji mbovu na kiburi. Wale wote watakao piga kura waelewesha kadhia ya huyo bwana na kundi lake kurudi tena kusimamia hatma ya mambo yenu. Hata kama kapitishwa peke yake, wakumbushe kuwa hata watakaompa kura wata mpa za NDIO na nyie mumpe za HAPANA
 
🤣 🤣 🤣
Sasa hapana itasaidia nini
Ingekuwa haisaidii kusingekuwa na kipengele cha kupiga kura ya hapana inapotokea kukawa na mgombea mmoja kwenye nafasi husika. Kura za hapana zikizidi za ndiyo, ina maana kwamba huyo mgombea hakubaliki kwa wananchi wa eneo husika. Kwa hiyo kama hakubaliki, inabidi mchakato wa uchaguzi uanze upya
 
Kumbe Tz kubwa mimi ninaekaa uku mashavuni sjaona mgombea yyte akienguliwa na campeni zimeanza na kila mmoja ananadi sera
Apa mtaani kwangu kuna wagombea wa vyama 3
Ccm,ACT,chadema

Iv wenzetu mnakaanga Tz gan ambayo inaengua wagombea wa upinzani
Mi mtaani kwangu sjawai ona mgombea akienguliwa ila wizi wa kura sawa
 
CCM wamedhania kuengua wagombea na sasa kujitapa kuwa Wapinzani hawajaweka wagombea wa kutosha kama CCM ndio ujanja.

Kutokupiga kura ni kuihalalishia ushindi CCM hivyo njia sahihi ni wapinzani na wale wote wanaojitambua kupiga kura ya kuwakataa ya HAPANA kwa wingi sana hadi wajue pamoja na figisu zao hawakubaliki.

Ndugu Mtanzania, Fisi haachiwi bucha hivyo ni bora nyama kuimwagia sumu ili akiila afe.

Slogan iwe HAPANA ni HAPANA TUU
Nani wakala wa kura za hapana?
 
Back
Top Bottom