Umuhimu wa Kiarabu kuwa lugha Rasmi Tanzania

Oh, umeni'pre empty' mkuu. Kwa kweli lugha kubwa duniani ni Kichina na hawa hatuwatendei haki kabisa kwa yale mema waliyotutendea na bado wanatutendea mema tu. Sasa halua na tende kutua tu basi baadhi yetu tumevurugwa! Aibu.
 
Utumwa vichwani mwa watu weusi ni wa kiwango cha juu mno. Leo wameona mfalme wa Morocco kaja sasa wanataka wawe waarabu hata kujifunza lugha zao!!

Kwa uwekezaji gani wa Arabs in Tz hadi tujifunze kiarabu, wazungu, wanafaransa, wajeruamani, waisrael waliotujengea vyuo ikiwamo UDSM na MIST na airports wapo miaka yote mbona hamjawahi sema tujifunze lugha zao!! Vipi wachina tuliowapa kila kitu na tunaoenda kwao kila siku kununua bidhaa mbona hamkusema tujifunze lugha zao

Kiswahili ni lugha ya pili kwa ukubwa barani Africa kwanini usiseme tusukume zaidi lugha yetu itumike na kukubalika zaidi badala ya kuacha ife na kuiga lugha za watu!!

Naona kuna la ziada nyuma ya hii hoja yako, na wengi wanatetea kwa sababu zao binafsi na si kwa lengo la taifa kwa ujumla.

Aidha mtu yeyote anaweza jifunza lugha yeyote atakayo ila sio kwa kushinikizwa kama unavyotaka iwe. Smh
 
Unataka tung'oe meno, kama kiingereza imekuwa ni taabu hivi je Kiarabu si ndio watu watakuwa na mapengo ya ukubwani.
 
Swadakta mkuu. Waarabu walipandikiza maneno yao pindi walipovamia huku kama walivofanya Wareno, Wajerumani, Wahindi na mpaka sasa Waingereza.
 
Mkuu, sie tumerogwa. Wenzetu haswa Afrika Magharibi lugha zao za asili (lugha mama) wanajifunza mashuleni na wanachanganya na lugha za kimataifa ndo maana wanafanikiwa mno. Sie lugha zetu za asili ni dhambi sawa na kuua mtu ndo maana hata hicho Kiingereza tunababaisha tu maisha yanasonga mbele.
 

Kuna contradictions Kibao kwenye ngonjera yako, una maana wazenji waaminifu sababu wanajua kiarabu? Kama waaminifu kwanini Zenji haiendelei badala yake bado ipo kama stone age? Kwanini hakuna wasomi wala educational institutions za maana? Lugha kama lugha ya kiarabu inawasaidia nini Zenji? Una habari kwamba Zenji ni hub ya madawa ya kulevya Africa, huo uaminifu wao upo wapi?

Ushirikiano wetu na waarabu hauwezi kupita ule wa Tz na China au Tz na nchi za Ulaya, kwanini tusingeanza kichina au English ambayo tunasoma toka vidudu hadi chuo kikuu na bado inatupiga chenga.

Acha kupotosha Kiswahili sio 75% kiarabu bali kimetohoa maneno kadhaa kama kilivyokopa toka lugha zingine na kama lugha zinginge zote zikopavyo.

Kiswahili ni lugha ya pili kwa ukubwa barani Africa kwanini tusisukume lugha yetu ili ikubalike na kutumika zaidi hadi hao waarabu wenu wajifunze lugha yetu badala ya sisi kuiga kwao kila kitu
 
Good luck kubishana na huyo bibie.
 

Hasbuna Allahu wa neiema L'wakil.

Nyundo ya namba 124 imekuingia kisawasawa mpaka unahororoja na kubwabwaja bila mpango.

Ukiona mwanamme anajidai mbele ya halaiki ujuwe huyo hafai, pengine mtungi kupanda ni shida.
 

Wacha upashkuna,herufi pekee kilatini,sasa kiswahili kiweje kiarabu?
Wajua herufi za kiarabu weye?
 
Fungua ubongo wako uone fursa,ndio maana ya hii thread,soma vizur uelewe usitoe povu tuu kabla ya kuelewa ujumbe uliopo,kifupi ni kwamba changamkia fursa najifunze jema haijalishi linatoka kwa nani
 

Do you know about ancient EGYPTIAN CIVILIZATION or NILE VALLEY CIVILIZATION kabla ya kuja kwa hao waarabu wako Afrika na Misri ya leo?

Je mafarao walikua waarabu????????
 
Do you know about ancient EGYPTIAN CIVILIZATION or NILE VALLEY CIVILIZATION kabla ya kuja kwa hao waarabu wako Afrika na Misri ya leo?

Je mafarao walikua waarabu????????


Huo ndiyo ujinga uliojazwa.

Waarabu Afrika hawakuja. Hilo neno Afrika lenyewe ni Kiarabu, for your information.

Uarabu si taifa, si nchi, si eneo, si rangi, ni lugha tu.

Lugha ya kwanza Afrika ni ipi?
 
Wanao kuja ndio wajifunze kiswahili.

Tutaangaika na lugha ngapi Duniani, wakati sisi tuna Lugha yetu ya Taifa?

Mataifa yote yenye Amani kama Tanzania yanaendelea kukua vizuri kiuchumi.

Afrika yetu imeshajua thamani ya Kiswahili, cha ajabu ni baadhi ya Watanzania hawajui thamani ya Kiswahili.

Tunaelekea kwenye uchumi wa kati, ni vizuri kwenda na Tunu zetu. Ikiwemo Mila na desturi za Mtanzania kuzingatiwa.

Tukianza kupuuza vya kwetu, tutapuuzwa kwa mengi, mwisho tushindwe yote.
 
Unafikili kwa kutumia----------kama alivyowaambia wabunge marehemu Dr.Masaburi
 
Kiswahili chenyewe ambacho ni lugha yako yako unapata 'F' unataka lugha ya kigeni iwe rasmi, post kama hizi utaziona JF pekee
 
Waarabu walikuja mwaka gani hapa tanganyika? Tuanzie hapo kwanza
Walikuja na wakawachukua babu na bibi zetu wengi sana kupita Taifa lolote lile duniani kufanya biashara ya utumwa, lakini walichoamua kuwafanyia watumwa wanajua wenyewe, walitutawala hata kibanda cha mkaa hawakuacha wanini hawa[emoji3] [emoji3] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 

Tafuta kamusi ya Kiswahili yenye etymology au mtafute mtaalam yeyote wa lugha ya Kiswahili utathibitishe kauli yangu. Tofauli iko kwenye matamshi na kwa kiasi fulani spelling. Kwa mfano neno "Swahili" kwa Kiarabu inatamkwa "Swahil"; "darasa" inatamkwa "darsa"; "mamlaka" inatamkwa "mamlakat", "halali" inatamkwa "halal"; "dini" inatamkwa "din", nk.
 
Acha upotoshaji kiswahili sio 50% kiarabu bali kimetohoa maneno kadhaa toka lugha ya kiarabu na lugha zinginge kama lugha zote duniani zilivyokopa maneno toka lugha zinginge.

Bila huku JF kuna wataalam wa lugha zote mbili. Wanaweza kuthibitisha hili.
 
Pia kiswahili kina lugha ya ki fars kutoka uajemi,au iran
 
Kwa hiyo mwakan tukipata wagen wengi toka nchi zinazungumza kireno kama ureno ,brazil,angola,cape vade,msumbiji n.k kireno iwe lugha rasm ya taifa?maajabu,
Ivyi ivyo tukipata wageni wengi toka nchi zinazotumia kifaransa na kihispaniola zote ziwe lugha rasm za taifa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…