Umuhimu wa kuchaguliwa Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti IDU

Adverse Effect

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2017
Posts
3,700
Reaction score
9,570
UMUHIMU WA KUCHAGULIWA LISSU KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA IDU KATIKA SIASA ZA UPINZANI NCHINI TANZANIA!

Watu wengi wanajadili kuhusu Tundu Lissu kuchaguliwa Makamu Mwenyekiti wa IDU. Kilichovutia wengi ni kitendo cha kuchaguliwa kwake akiwa gerezani hivyo kuthibitisha uwezo na mvuto wa Lissu hata nje ya Tanzania.

Lakini jambo ambalo wengi hawajaliangazia ni juu ya Mwenyekiti wa IDU. Mwenyekiti wa IDU ni Stephen J. Harper, Waziri Mkuu mstaafu wa Canada. Kwa maneno mengine ni hivi; IDU ni taasisi kubwa yenye ushawishi mkubwa zaidi duniani kwa kuwa inahusisha viongozi walioko madarakani na wa upinzani katika nchi nyingi na zenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani.

IDU ni umoja wa wanademokrasia duniani au democratic alliance; sio umoja wa wajamaa (socialist alliance) na sio umoja wa waliberali (liberal alliance). Umoja wa wanademokrasia ndio wenye nguvu kubwa kiuchumi pamoja na ushawishi zaidi wa kisiasa duniani kwa sasa!

Kwa sababu hiyo, nguvu iliyo nyuma ya Lissu na CHADEMA kwa ujumla ni nguvu kubwa zaidi kuliko watu wanavyoweza kufikiri. Taarifa kuwa Lissu amepewa kesi ya uhaini kwa kuwa yeye analengwa kudhoofishwa kisiasa na kuweza ni mambo yanayojadiliwa sana na wakuu wengi wa nchi nyingi zenye nguvu na ushawishi zaidi duniani kuliko watu wa Itunge wanavyofikiri!

Kauli ya Marekani kutaka uchunguzi ufanyike juu ya kunyanyaswa na kuteswa wanaharakati wa Kenya na Uganda waliokuja Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya Lissu ni 'mbwibwi' tu au chemichemi ya agenda na hoja zilizotoka katika ule Mkutano Mkuu wa IDU na Bunge la Ulaya. Lakini hatutashangaa kuona Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au UN kuanza kuijadili Tanzania kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki kwa watu wake.

Tunatarajia sana na hatutashangaa kusikia pia tamko la Uingereza. Ikumbukwe kuwa Robert (Bob) Amsterdam aligusia kuwa ataiandikia Jumuiya ya Madola kuhusiana na suala la uhusika wa Serikali katika kumpiga risasi Mhe. Tundu Lissu. Uhusiano wa Jumuiya ya Madola na Uingereza ni kama uhusiano wa mama na binti! Watu wengi hawajui hili.

Lakini kitendo cha Lissu kuchaguliwa Makamu Mwenyekiti wa IDU, ni ushindi mkubwa sana kwake na CHADEMA na pigo kubwa sana kwa watu walioasisi kesi yake! Kwa sasa, aliyeko katika magereza ya Ukonga, sio Lissu tena bali ni Makamu Mwenyekiti wa IDU.

Wakati serikali ya Tanzania ikitumia pesa nyingi sana ili kuendesha kesi ya uhaini dhidi ya Lissu ili kusudi akikutwa na hatia anyongwe hadi afe, viongozi wakuu wa dunia wanamchagua kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi kubwa na iliyo na ushawishi mkubwa zaidi duniani. Lakini ni kwa vyovyote vile, uchaguzi wake haukuwa wa bahati mbaya. Ni matokeo ya ushawishi mzito pamoja na kampeni za hali ya juu sana ambazo huenda ziliongozwa na watu wenye ushawishi, mvuto na heshima kubwa ndani ya IDU!

Huenda watawala wa Tanzania ni kama walijua kilichotarajiwa katika Mkutano Mkuu wa IDU. Hii ndio sababu ya kutumia nguvu kubwa sana katika kumdhibiti Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA asihudhurie mkutano ule. 'Mandeleni' aliwahi kusema ya kuwa hata hayo mengine aliyofanyiwa Lissu ilikuwa ni namna ya kutaka 'kumuepusha' na kikombe cha kuwa Makamu Mwenyekiti wa IDU! Lakini kumsikiliza 'Mandeleni' ni sawa na kusema wewe ni 'Falala' wa Kyela Sokoni au 'Litwele' wa Kalumbulu!

Je, nani ajuaye kuwa kama Lissu angekuwepo katika ule Mkutano angekuwa Mwenyekiti? Nduhuu!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 24 Mei 2025
 
Yajayo yanafurahisha. Samia na magenge yake acha waendelee kushupaza shingo tu.
 
Eeh, mchezo huu unachezwa vizuri sana..

Huko magogoni hawajui watoke vipi kwenye hili saga...

Tuendako ni kuzuri. Japo, wanaoitengeneza njia ya uzuri huu, wanapita ktk bonde kuu la uvuli wa mauti...

Lakini tumaini ni kuwa, "....tujapita katika bonde la uvuli wa mauti, gongo lako Bwana Yesu Kristo na fimbo yako vyalinda.."
 
Back
Top Bottom