John Mwilolezi
New Member
- Jun 12, 2023
- 1
- 1
Kwa kila mwaka, serikali inahitaji makadilio ya mapato na matumizi ili iweze kuendesha nchi na kutekeleza miradi mbalimbali ili kunufaisha wananchi na kuleta maendeleo yaliyo thabiti.
Hii pia huchagizwa na uwepo wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo kwa kila mwaka lazima likae bunge la bajeti na kuipa nafasi kila wizara kuwasilisha makadilio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha, na baadae waziri wa fedha kuwasilisha bajeti nzima ya serikali kwa mwaka ujao.
Katika kuhakikisha kuwa serikali inafanya kazi na inawajibika vyema kwa wananchi wake, kuna ulazima sasa wa kila Wizara kuwa na utaratibu wa kusoma mapato na matumizi ya mwaka uliopita, hii itachagiza ukuuaji wa uongozi bora, maadili katika ngazi ya viongozi, uwajibikaji kwa kila taasisi ya serikali na kuondoa mtazamo wa watu kuhusu matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Kwa kufanya hivyo, jamii na watanzania kwa ujumla watapata faida zifuatazo:-
Mosi, kujua taarifa sahihi ya mapata na matumizi kwa mwaka uliopita baina mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na taarifa ya wizara itakayoletwa bungeni wakati wizara husika ikiwa inawasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya mwaka ujao, hii itachangia ukuuaji wa watu kujua kwamba wizara zinawajibika ipasavyo na si kutegemea mtu mmoja pekee yaani Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Pili, katika kuelezea matumizi na utekelezaji wa fedha kwa mwaka uliopita, wananchi watapata uelewa kuwa fedha hizo zinaenda katika sehemu sahihi kwani bungeni ndio sehemu pekee wananchi wanawakilishwa na si kusubiri mpaka watu wahoji kuhusu miradi ya serikali, hii itajenga ukweli na uwazi katika masuala ya uwajibikaji kwani kuna baadhi miradi ambayo hufia kwenye makaratasi tuu na pia kiongozi huyohuyo anakuja tena kuomba bajeti ambapo bajeti iliyopita haijakamilisha mradi tajwa na hata hawaleti mrejesho husika, hii inajenga dhana ya imani kuwa wizara zinapokuja kuomba kupitishiwa bajeti ni fedha zao na angalau watakumbuka miradi ya wananchi jambo ambalo si sawa katika uendeshaji wa nchi yetu.
Tatu, kuijengea uaminifu wizara iliyoaminiwa na kupitishiwa bajeti na bunge. Kwa maana ya kwamba, kila wizara ikiwa inaomba kupitishiwa bajeti, lazima isome matumizi ya bajeti iliyopita na kujengea uaminifu mbele ya bunge na wananchi kwa ujumla kuwa fedha zinaenda sehemu stahiki. Kwa mfano, utamkuta mbunge anaelezea utekelezaji wa miradi ambayo imetajwa kwenye wizara fulani, lakini hii ingefaa zaidi siku ambayo waziri mwenye dhamana husika akaisome pia bungeni ili kuweka usawa wa uwajibikaji katika kutekeleza majukumu husika.
Nne, kuwatambua viongozi bora walioshika madaraka ya juu. Hii n kutokana na uwajibikaji kwa minajili hiyo itawezesha wananchi kumjua ni nani anapaswa kuwa kiongozi wao kwani itachochea utendaji kazi katika ngazi zote za serikali na kuleta chachu ya maendeleo kwa Taifa.
Tano, kujenga imani ya muunganiko mzuri na mahusiano thabiti baina ya wizara na ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa wananchi. Hii itasaidia katika pande zote tatu yaani wananchi, wizara na ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali kuamianiana na kuondoa sintofahamu kwa wananchi hasa pale ambapo miradi haijatekelezwa kwa wakati na kuleta majibu sahihi wakati wa taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali na taarifa ya wizara husika wakati wa kuomba bajeti mpya ndani ya bunge zikifanana inaleta ule mjumuiko wa imani nzuri kwa viongozi wa Taifa.
Sita, itapunguza uwezekano wa uwepo wa rushwa na kusaidia kwa namna nyingine kupambana na rushwa na kuwa chini zaidi kwani italeta usawa wa matumizi na matumizi yake yatakuwa kwa umakini zaidi, na ukaguzi wake utakuwa makini. Japo kuna mgawanyo wa madaraka lakini katika suala la pesa za wananchi inahitaji taarifa zaidi za siyo za uapnde mmoj tuu bali pande mbili ama zaidi ili kuleta chachu ya uwajibikaji na uongozi bora.
Hivyo basi, katika kutekeleza haya, serikali bila kukumbushwa wajbu wake kila mara itakuwa inaomba kila mwaka bajeti ambayo matumizi yake yanakuwa hayana taarifa zaidi kwa wananchi, kwani huwa tunaona kila wizara kwa kila mwaka inakuja na makadilio ya mapato na matumizi ambayo yamekuwa yakizidi kila mwaka lakini wakituletea na wao jinsi ambavyo walitumia bajeti iliyopita itakuwa jambo la msingi na la kujivunia katika nchi yetu ya Tanzania.
Lakini haya yote hayawezi kutekelezeka mpaka kufanyike kwa mabadiliko ya kikatiba ambayo yatawataka mawaziri wa wizara husika kufanya au kuleta mrejesho wa matumizi ya fedha za awali. Hii pia itaonesha makuzi ya kidemokrasia ndani ya nchi yetuna mataifa yote kwa ujumla, kwani viongozi wote watawajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao na kujenga msingi wa utawala bora kwa viongozi wajao na kwa taifa la kesho.

Upvote
1