Umuhimu wa kutozima simu usiku: Daraja la Wokovu Wakati wa Dharura

Umuhimu wa kutozima simu usiku: Daraja la Wokovu Wakati wa Dharura

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Wandugu zingatieni sana hili hasa ukiwa pekeyako

Ni uamuzi wa busara sana kutozima simu yako unapoenda kulala, kwani hatua hii ndogo inaweza kuwa tofauti kati ya usalama na janga kubwa.

Nyakati za usiku zimejaa mambo yasiyotabirika, na simu yako ikiwa hewani inafanya kazi kama kiunganishi kikuu cha usalama kwa pande zote mbili.

Kwa upande mmoja, unaweza kuwa nguzo pekee ya matumaini kwa ndugu, rafiki, au jirani anayepatwa na dharura ya ghafla kama vile ugonjwa au uvamizi! na anahitaji msaada wako wa haraka ili kuokoa maisha yake.

Kwa upande mwingine, simu hiyo hiyo inaweza kuwa uokozi wako mwenyewe; watu wanaokujali au mamlaka za usalama wanaweza kukupigia simu kukupa tahadhari ya haraka kuhusu hatari inayokaribia makazi yako, kama vile moto au mafuriko ama wasiojulikana na hivyo kukupa nafasi ya kuchukua hatua kabla ya kuchelewa.

Kuzima simu ni kujitenga na ulimwengu wakati ambao unahitaji ulinzi na mawasiliano kuliko wakati wowote ule.
 
Mimi simu yangu muda wote vibration siweki mlio , nilijuta siku nilipiga usiku sasa saba mtu amekwama anahitaji Msaada wa haraka simu iliita na alituma text bila mafanikio nilistuka saa 9 usiku nikaona missed call na text . Nikamsaidia alinishukuru japo nilichelewa kutoa Msaada
 
Binafsi simu tangu huwa vibration, sipendi makelele ya simu kuita hasa nikiwa kati kati ya watu.
 
Kuna siku majirani zangu walifungiwa makomeo ya nje na wakaibiwa vitu walivyoviacha nje. Wezi walishindwa kunifungia kwa nje, jirani walinipigia simu usiku nikawafungulie milango yao iliyofungwa kwa nje. Hakuna sababu ya maana kuzima simu usiku
 
Weka simu wazi. Na tujifunze kupokea simu pia kwa wakati..ikiwa tu upo pahala pagumu.
Na wale umepewa namba ya mtu sikuhizi madeni mengi..ukipiga mara 1😀 ifuate text ya kujitambulisha.

"Mkuu mie fulani namba nimepewa na Mshana Jr,,kuna jambo la ugali waweza pokea au ukiwa na muda utanirejea"
 
Dah haya bhana
 
Hatuna tofauti bwashee mimi kuna msumari tu nafanyaga kuubadili tu ukilegea
Mimi kama nyinyi tu! Hua naweka taulo tu pale juu ya mlango ili ushikane na frem, ukisukuma tu uko ndani.
 
Huwa ikifika saa nne nazima simu na kuwasha asubuhi saa mbili au saa tatu. Matatizo nitashughulika nikiamka
 
Back
Top Bottom