SoC01 Umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo

Stories of Change - 2021 Competition

Abrianna

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
4,696
Reaction score
15,390
Utangulizi
Dira kwa maana fupi ni muelekeo. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision (TDV) 2025 ilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2000 lengo kuu likiwa kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. 'www.tanzania.go.tz' (tovuti kuu ya serikali)

Melengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni pamoja na kuboresha hali ya maisha ya kila Mtanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani usalama na umoja,kujenga utawala bora,kujenga jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani. (Nukuu kutoka Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025).

Katika andiko hili, nitaangazia malengo makuu matano kama yalivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025. Andiko langu litaangazia pia utekelezaji wa malengo haya na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Katika uhalisia, Maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa yamekua yakitegemea Ilani ya chama tawala pamoja vipaumbele vya Rais aliye madarakani. Mfano halisi ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa madaraja ambao uliingiza nchi katika madeni makubwa na umaskini. Ni wazi kwamba Dira ya Maendeleo ni kijarida tu ambacho kimetengenezwa kutimiza wajibu lakini hakina nafasi kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Serikali imeunda mipango mingi kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo kama vile mpango wa maendeleo wa miaka mitanpo (Five Year Development Plan), MKUKUTA, Mpango wa Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa), Mpango wa maboresho ya utumishi wa Umma,pamoja na Maleongo ya Maendeleo ya Millenia chini ya nchi za Umoja wa Mataifa.

Katika mipango tajwa, yote ina malengo yanayolandana kwa maana ya kutokomeza umaskini kwa kuboresha huduma za afya, elimu, nishati, kilimo, maji, biashara, mahusiano ya kimataifa, ajira, kuboresha utumishi wa umma, kuweka usawa wa kijinsia pamoja na mengine mengi.

Hebu tuangazie miaka kumi nyuma tulinganishe na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na hali halisi ya Watanzania mpaka leo hii.

Hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kuwa duni pamoja na kwamba nchi yetu ipo katika uchumi wa kati wa chini, Mtanzania wa kawaida anashindwa kumudu gharama ndogo za mlo wa siku ilhali tunatangaziwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 7% ( NBS 2019/2020).

Katika kujenga utawala bora, hali imezidi kuwa tete, ni wazi kwamba utawala wa sheria umekua jambo gumu katika nchi yetu hali inayopelekea kutokuwajibika kwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma (Rejea ripoti ya CAG 2020).

Katika Dira ya Mendeleo 2025, serikali imeonyesha nia ya kujenga jamii iliyoelimika na inayojifunza kila siku kulingana na mazingira na nyakati tulizopo, tukirudi kwenye uhalisia, kiwango cha ubora wa elimu zetu hakikidhi viwango vitakavyowawezesha wasomi wetu kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania, shule zetu nyingi hazina waalimu wa kutosha wala vifaa vya kufundishia, matamko ya kisiasa kwa upande mwingine yamekua yakiathiri mifumo ya elimu.

Kwa mfano mnamo mwezi Desemba 2020, Rais JPM aliagiza somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa katika shue za msingi mpaka sekondari, Wizara ya elimu iliandaa machapisho kwa ajili ya somo husika lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani somo hilo lilisitishwa rasmi.

Kwa upande mwingine serikali ilichangia kupotosha jamii badala ya kuelimisha. Nitoe mfano mdogo wa janga la Covid 19. Serikali ilisimama kidete kuuaminisha umma kwamba janga hili ni vita ya mabeberu dhidi yetu badala ya kutumia wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu namna bora ya kujikinga ili kuepuka maambukizi. Serikali ilienda mbali zaidi na kuhamasisha tiba mbadala na njia za asili ambazo zilitumika katika vituo vya afya pia.

Kauli ya serikali pamoja na viongozi wakuu wa nchi imeleta mkanganyiko pamoja na hisia tofauti juu ya janga hili na kusababisha watu kuishi pasipo kuchukua tahadhari hata baada ya serikali kubadili msimamo na kuamua kufuata njia za kitaalamu. Ukijaribu kuongea na watanzania kumi, tisa kati yao wanaogopa chanjo na kuamini kwamba mabeberu wanataka kutumaliza.

(picha kutoka mtandaoni)

Katika uboreshaji wa utumishi wa umma, vilio vimekua vingi, utekelezaji wa dhima hii umesahaulika kwa miaka zaidi ya mitano iliyopita, vilio vingi vya wafanyakazi kuhusu nyongeza za mishahara pamoja na kupanda madaraja, makato makubwa, na mishahara duni ambayo haikidhi maisha ya kila siku.

Mambo ya muhimu yaliyotajwa katika utekelezaji wa malengo ya milenia ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimataifa, kutokomeza umaskini wa kipato na njaa. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imepuuza kwa kiasi kikubwa sana mahusiano ya kimataifa kutokana na misimamo ya kiongozi aliyekua madarakani. Vipato vya wananchi vimeshuka kutokana na tozo kubwa katika bidhaa na huduma, mfumuko wa bei umeathiri pembejeo za kilimo na bidhaa mbalimbali, uonevu kwa wafanyabiashara,ubambikaji wa kesi na kodi uliosababisha biashara nyingi kufungwa. Tunao mfano halisi wa sasa katika tozo ya miamala ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi masikini ambao hata kula yao ni ya tabu.

Mapendekezo
• Serikali ianzishe taasisi maalumu kwaajili ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa. Chombo hicho kiwe na kazi ya kuandaa, kusimamia pamoja na kuishauri serikali iliyopo madarakani bila kujali chama.Taasisi hii ihakikishe sera sera na mipango ya taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wizara zina uelekeo mmoja na zinashirikiana ka ukaribu. Kwa mfano suala la kuzalisha wahitimu wenye weledi ni lazima liendane na uboreshaji mfumo wa elimu, kwa hiyo ni lazima wizara ya kazi na wizara ya elimu zishirikiane kubaini mapungufu yanayoonekana kwa wahitimu wanaoajiriwa ili waweze kubaini njia bora ya kuboresha.

Taasisi hii ipewe mamlaka ya kusimamia serikali kama ilivyo bunge na mahakama na kwamba ilani ya chama cha kiongozi aliyeko madarakani ilenge kutafuta au kuonyesha njia sahihi za kuipeleka nchi kule ambako dira inaonyesha, hii itasaidia kutekeleza miradi iliyoachwa au iliyoanzishwa na kiongozi aliemaliza muda wake, mfano wakati Rais JPM naingia madarakani alisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa madai kwamba mikataba ilikua mibovu na iliyojaa unyonyaji, siku chache baada ya Rais Samia kuingia madarakani mapitio ya ujenzi wa bandari yameanza, hii ni kwa sababu hakuna mfumo wa kusimamia viapaumbele vya maendeleo ya Taifa badala yake kila kiongozi anajiamulia kile anachopenda.

• Ipatikane katiba imara ambayo itasaidia kudhibiti na kusimamia viongozi walioko madarakani na hata baada ya kustaafu kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Marekani na Afrika ya Kusini. Hii itahakikisha viongozi wote wanafanya kazi kwa kuheshimu haki za binadamu na sheria na taratibu zilizopo bila kuathiri malengo ya Taifa kwa ujumla. Katiba imara pia itasaidia kuweka uwajibikaji na usawa kati ya watumishi/viongozi, kuondoa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• Serikali ijikite zaidi katika kuvumbua vyanzo vipya vya mapato badala ya kujikita katika kuongeza kodi katika huduma mbalimbali za kijamii ili kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na badala yake wananchi wapate unafuu wa maisha. Mfano sekta ya utalii na madini zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama tukiweka usimamizi mzuri na mifumo ya kuaminika ili kuepusha mianya ya ubadhirifu. Pia serikali ijikite katika kuboresha mfumo wa elimu ili kuruhusu vijana wengi kujiajiri katika nyanja mbalimbali badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

• Bajeti za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge zisitumike kinyume na lengo ili tuweze kutekeleza mipango iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa serikali. Huko nyuma tulishuhudia pesa zikipelekwa katika matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge hali iliyochangia kukwamishwa kwa miradi mingi ya maendeleo iliyoidhinishwa na bunge. Bajeti inayoidhinishwa pia iende sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

• Serikali iunde mfumo shirikishi utakaosaidia wananchi kushiriki katika kuonyesha vipaumbele vya maendeleo pamoja na utekelezaji. Hii itasaidia wananchi kuwa wasimamizi wa moja kwa moja wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

• Serikali iwatumie wataalamu wa masuala ya uchumi walioko nchini badala ya kutumia wanasiasa pekee katika kuandaa bajeti na matumizi ya serikali, pia serikali ijenge utamaduni wa kuwatumia wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali nchini katika kuandaa na kusimamia sera mbali mbali kwaajili ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuheshimu mawazo na maelekezo ya wataalamu katika sekta mbalimbali hata pale yanapotokea majanga yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu. Kwa kufanya hivi, tutapunguza au kudhibiti matamko ya kisiasa katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu kama vile Afya, Elimu na Uchumi.

Hitimisho
Natoa wito kwa viongozi/wenye mamlaka, na watunga sera wa nchi, maamuzi yoyote wanayofanya yanaathiri au kufaidisha jamii nzima, wao ni sehemu ya jamii na hivyo wataathirika au kufaidika na maamuzi hayo kwa namna moja au nyingine. Ni vyema kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka athari zozote zitakazoisababishwa na maamuzi yao ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Asanteni Sana​
 
Upvote 1.3K
Asante sana, nakubaliana na wewe kabisa, tunahitaji katiba ya wananchi ili itusaidie kusimamia dira ya maendeleo na kuwaongoza watawala kutekeleza matakwa ya wananchi kama yalivyoainishwa katika dira
 
Umesema vizuri mkuu, unajua Nyerere alikua na sauti kubwa na inayosikilizwa hata na viongozi wenzake!angeamua kusimamia zoezi la mchakato wa katiba mpya asingepata pingamizi toka kwa yeyote, kwa sasa wananchi wamebweteka tunawaachia upinzani kila kitu, viongozi wa upinzani wanahenyeshwa na dola, wanateswa na kupigwa, wanawekwa ndani kila siku na familia zao zinateseka just kwa sababu wanapigania maslahi yetu ila tunashindwa hata kuwapambania, tunashindwa hata kuwaunga mkono japo kwa kujitokeza barabarani na mambango, ndio maana serikali inachukua hii advantage kuwaonea upinzani kwa sababu wananchi tumekua wapole, tungeamua wote kuonyesha makali yetu hata polisi wangeshika adabu.

Tunahitaji tume huru ya uchaguzi pia ili tuweze kupata viongozi tuliowachagua, angalia sasa, wabunge wooote yulichaguliwa na mwendazake na wapo bungeni kwa maslahi ya ccm na sio maslahi yetu sisi, tozo zikipitishwa wanasema ndiioooo huku wamesinzia, kwa kifupi hakuna sauti ya wananchi ndani ya bunge kwa sababu ya tume ya ccm ambayo imetuletea viongozi maboga kabisa

Tusipokua na katiba mpya na tume huru, tusahau kuhusu utekelezaji wa dira[emoji19]
 
Mzigo mkubwa wa kodi unaua biashara na maendeleo ya wananchi, kuendelea mzigo wa kodi lazima upungue
Mkuu mzigo wa kodi hauwezi kupungua badala yake kila siku mwingulu anakuja na mapya, awamu hii ya mdemko tutegemee kodi na tozo nyingi sana
 
Ubarikiwe mwandishi,uzi unajieleza vizuri sana
 
Binafsi uandishi wako kidogo nimeulewa ila jambo ambalo limebaki kuwa debate yenye utata mkubwa hapa kwetu limekuwa ni jambo la ubora wa elimu na ubora wa wahitimu katika institution za elimu hapa kwetu.

Mara nyingi kuna group of theorists wanaoamini kiwango cha wahitimu katika elimu yetu kimekuwa hakina ubora ule unaotakiwa

Hoja zinaweza kuwa nzuri au otherwise ila kitu ambacho mara nyingi nimekuwa napenda njue kutoka kwao ni hili jambo.

Je wanapo claim kuwa wahitimu wanaviwango ambayo si bora walishajiuliza ni kiasi gani wamewekeza kutoa hao wahitimu bora?

Kuna watu wanasema kwamba education sector ni industry kama zilivyo industries nyingine na kama hii ni sahihi basi wahitimu wetu ni malighafi na wanakuwa processed ndio tunapata hii end product ambayo kila aliyejaliwa kuongea basi uwasema vile itampendeza

Ila tunasahau ata mbegu ikipandwa inahitaji mbolea, maji, mwanga n.k ili iweze kuwa na mazao bora.Hili jambo kwetu kwenye elimu ni kama halizingatiwi katika namna bora ila jambo ambalo kila mtu analiweza ni kulaumu tu wahitimu hawana ubora

Kuhitimisha nipende kuomba radhi maana kunaweza kukawa na uandishi usio kuwa mzuri na kuchanganya lugha but guess what! najaribu kila wakati ili niweze kuboresha

Asanteni
 
Kwa bahati mbaya bado sijaona jitihada za kueleweka zilizowekwa na serikali katika kuhakikisha elimu yetu inakuwa bora na wahitimu wa vyuo mbalimbali wanakuwa wazuri kuendana na mahitaji ya sasa ya Nchi, serikali imejikita sana kwenye kuboresha miundombinu katika shule na vyuo mbalimbali ilihali rasilimali watu,pamoja na mitaala ya elimu ikiwa ni ileile isiyokidhi mahitaji yetu, mwisho tunaishia kupata wahitimu wengi wenye elimu na ujuzi usioendana na mahitaji yetu.
 
Kati ya threads zilizoanzishwa kwa hili sindano, pamoja na mapungufu yake this looks like to be the best of all. To me you are the clear winner. Congrats!

Ila kitu kingine ambacho serikali inatakiwa iachane nacho ni hizi teuzi au appointments za ngazi mbalimbali hasa za kuanzia Wakurugenzi Wasaidizi kwa ngazi zote serikalini, Taasisi na mashirika ya Umma. Hizo nafasi ilitakiwa ziwe zinatangazwa na kugombewa na Watanzania wote wenye qualification na uwezo.

Mgumo wa sasa wa kila mkubwa kuteuliwa na Rais unakwamisha pia utendaji na chain of command. Waziri anaweza kuwa mzito kutake into account mtu wake wa chini kwa kuwa naye ni mteule wa Rais. Pia anakuwa hajui why the guy was given that position.

Kwenye Taasisi na mashirika ya Umma all senior positions ziwe performance based na zitolewe kwa mkataba wa miaka 5 na mtu asikalie hiyo nafasi kwa zaidi ya miaka 15. Interviews zao zifanywe na independent individuals pamoja na some board members. Final appoints zifanywe na Mawaziri husika badala ya Rais kutegemea matokeo na mapendekezo baada ya interview.

Board za Wakurugenzi ziteuliwe na Mawaziri husika kwa kuzingatia na kushirikisha Wadau huku zikiinclude Wadau wenyewe kwenye hizo board kama Wawakilishi.
 
I second this!! Tena iwe independent kabisa ili maamuzi yao yasiingiliwe na Executive.

Mada murua kabisa hii, receive my upvote
 

Well said! Of course hizo zitakua success parameters za dira ya mpango wa maendeleo wa taifa, something holistic, inclusive, ranging from quality education to social services.
 

Mkuu unamuwajibishaje mtu uliyemkabidhi cheo/ wadhifa kama ngekewa? Hana mpango wowote wa atakachofanya kwenye hiyo nafasi.

Kama ulivyopendekeza, nafasi itangazwe, vigezo vitolewe, unaulizwa ukiipata hii nafasi tutarajie yapi kutoka kwako? Mtu ajivishe kamba mwenyewe shingoni.

Uwezekano wa kuongezwa mkataba utegemee utakavyoweza kufanya kazi vizuri na kutekeleza malengo ya hiyo nafasi. Hii nchi itabadilika.
 
Andiko zuri, mwandishi anafaa kuchukua nafasi ya mzee wa tozo! Watu wenye akili wapo mtaani huku kina Babu T wako mjengoni! Nchi hii bhana .........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…