SoC01 Umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo

Stories of Change - 2021 Competition

Abrianna

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
4,696
Reaction score
15,390
Utangulizi
Dira kwa maana fupi ni muelekeo. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision (TDV) 2025 ilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2000 lengo kuu likiwa kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. 'www.tanzania.go.tz' (tovuti kuu ya serikali)

Melengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni pamoja na kuboresha hali ya maisha ya kila Mtanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani usalama na umoja,kujenga utawala bora,kujenga jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani. (Nukuu kutoka Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025).

Katika andiko hili, nitaangazia malengo makuu matano kama yalivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025. Andiko langu litaangazia pia utekelezaji wa malengo haya na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Katika uhalisia, Maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa yamekua yakitegemea Ilani ya chama tawala pamoja vipaumbele vya Rais aliye madarakani. Mfano halisi ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa madaraja ambao uliingiza nchi katika madeni makubwa na umaskini. Ni wazi kwamba Dira ya Maendeleo ni kijarida tu ambacho kimetengenezwa kutimiza wajibu lakini hakina nafasi kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Serikali imeunda mipango mingi kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo kama vile mpango wa maendeleo wa miaka mitanpo (Five Year Development Plan), MKUKUTA, Mpango wa Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa), Mpango wa maboresho ya utumishi wa Umma,pamoja na Maleongo ya Maendeleo ya Millenia chini ya nchi za Umoja wa Mataifa.

Katika mipango tajwa, yote ina malengo yanayolandana kwa maana ya kutokomeza umaskini kwa kuboresha huduma za afya, elimu, nishati, kilimo, maji, biashara, mahusiano ya kimataifa, ajira, kuboresha utumishi wa umma, kuweka usawa wa kijinsia pamoja na mengine mengi.

Hebu tuangazie miaka kumi nyuma tulinganishe na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na hali halisi ya Watanzania mpaka leo hii.

Hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kuwa duni pamoja na kwamba nchi yetu ipo katika uchumi wa kati wa chini, Mtanzania wa kawaida anashindwa kumudu gharama ndogo za mlo wa siku ilhali tunatangaziwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 7% ( NBS 2019/2020).

Katika kujenga utawala bora, hali imezidi kuwa tete, ni wazi kwamba utawala wa sheria umekua jambo gumu katika nchi yetu hali inayopelekea kutokuwajibika kwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma (Rejea ripoti ya CAG 2020).

Katika Dira ya Mendeleo 2025, serikali imeonyesha nia ya kujenga jamii iliyoelimika na inayojifunza kila siku kulingana na mazingira na nyakati tulizopo, tukirudi kwenye uhalisia, kiwango cha ubora wa elimu zetu hakikidhi viwango vitakavyowawezesha wasomi wetu kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania, shule zetu nyingi hazina waalimu wa kutosha wala vifaa vya kufundishia, matamko ya kisiasa kwa upande mwingine yamekua yakiathiri mifumo ya elimu.

Kwa mfano mnamo mwezi Desemba 2020, Rais JPM aliagiza somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa katika shue za msingi mpaka sekondari, Wizara ya elimu iliandaa machapisho kwa ajili ya somo husika lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani somo hilo lilisitishwa rasmi.

Kwa upande mwingine serikali ilichangia kupotosha jamii badala ya kuelimisha. Nitoe mfano mdogo wa janga la Covid 19. Serikali ilisimama kidete kuuaminisha umma kwamba janga hili ni vita ya mabeberu dhidi yetu badala ya kutumia wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu namna bora ya kujikinga ili kuepuka maambukizi. Serikali ilienda mbali zaidi na kuhamasisha tiba mbadala na njia za asili ambazo zilitumika katika vituo vya afya pia.

Kauli ya serikali pamoja na viongozi wakuu wa nchi imeleta mkanganyiko pamoja na hisia tofauti juu ya janga hili na kusababisha watu kuishi pasipo kuchukua tahadhari hata baada ya serikali kubadili msimamo na kuamua kufuata njia za kitaalamu. Ukijaribu kuongea na watanzania kumi, tisa kati yao wanaogopa chanjo na kuamini kwamba mabeberu wanataka kutumaliza.
1626861526209.png
1626861576665.png

(picha kutoka mtandaoni)

Katika uboreshaji wa utumishi wa umma, vilio vimekua vingi, utekelezaji wa dhima hii umesahaulika kwa miaka zaidi ya mitano iliyopita, vilio vingi vya wafanyakazi kuhusu nyongeza za mishahara pamoja na kupanda madaraja, makato makubwa, na mishahara duni ambayo haikidhi maisha ya kila siku.

Mambo ya muhimu yaliyotajwa katika utekelezaji wa malengo ya milenia ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimataifa, kutokomeza umaskini wa kipato na njaa. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imepuuza kwa kiasi kikubwa sana mahusiano ya kimataifa kutokana na misimamo ya kiongozi aliyekua madarakani. Vipato vya wananchi vimeshuka kutokana na tozo kubwa katika bidhaa na huduma, mfumuko wa bei umeathiri pembejeo za kilimo na bidhaa mbalimbali, uonevu kwa wafanyabiashara,ubambikaji wa kesi na kodi uliosababisha biashara nyingi kufungwa. Tunao mfano halisi wa sasa katika tozo ya miamala ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi masikini ambao hata kula yao ni ya tabu.

Mapendekezo
• Serikali ianzishe taasisi maalumu kwaajili ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa. Chombo hicho kiwe na kazi ya kuandaa, kusimamia pamoja na kuishauri serikali iliyopo madarakani bila kujali chama.Taasisi hii ihakikishe sera sera na mipango ya taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wizara zina uelekeo mmoja na zinashirikiana ka ukaribu. Kwa mfano suala la kuzalisha wahitimu wenye weledi ni lazima liendane na uboreshaji mfumo wa elimu, kwa hiyo ni lazima wizara ya kazi na wizara ya elimu zishirikiane kubaini mapungufu yanayoonekana kwa wahitimu wanaoajiriwa ili waweze kubaini njia bora ya kuboresha.

Taasisi hii ipewe mamlaka ya kusimamia serikali kama ilivyo bunge na mahakama na kwamba ilani ya chama cha kiongozi aliyeko madarakani ilenge kutafuta au kuonyesha njia sahihi za kuipeleka nchi kule ambako dira inaonyesha, hii itasaidia kutekeleza miradi iliyoachwa au iliyoanzishwa na kiongozi aliemaliza muda wake, mfano wakati Rais JPM naingia madarakani alisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa madai kwamba mikataba ilikua mibovu na iliyojaa unyonyaji, siku chache baada ya Rais Samia kuingia madarakani mapitio ya ujenzi wa bandari yameanza, hii ni kwa sababu hakuna mfumo wa kusimamia viapaumbele vya maendeleo ya Taifa badala yake kila kiongozi anajiamulia kile anachopenda.

• Ipatikane katiba imara ambayo itasaidia kudhibiti na kusimamia viongozi walioko madarakani na hata baada ya kustaafu kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Marekani na Afrika ya Kusini. Hii itahakikisha viongozi wote wanafanya kazi kwa kuheshimu haki za binadamu na sheria na taratibu zilizopo bila kuathiri malengo ya Taifa kwa ujumla. Katiba imara pia itasaidia kuweka uwajibikaji na usawa kati ya watumishi/viongozi, kuondoa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• Serikali ijikite zaidi katika kuvumbua vyanzo vipya vya mapato badala ya kujikita katika kuongeza kodi katika huduma mbalimbali za kijamii ili kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na badala yake wananchi wapate unafuu wa maisha. Mfano sekta ya utalii na madini zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama tukiweka usimamizi mzuri na mifumo ya kuaminika ili kuepusha mianya ya ubadhirifu. Pia serikali ijikite katika kuboresha mfumo wa elimu ili kuruhusu vijana wengi kujiajiri katika nyanja mbalimbali badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

• Bajeti za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge zisitumike kinyume na lengo ili tuweze kutekeleza mipango iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa serikali. Huko nyuma tulishuhudia pesa zikipelekwa katika matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge hali iliyochangia kukwamishwa kwa miradi mingi ya maendeleo iliyoidhinishwa na bunge. Bajeti inayoidhinishwa pia iende sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

• Serikali iunde mfumo shirikishi utakaosaidia wananchi kushiriki katika kuonyesha vipaumbele vya maendeleo pamoja na utekelezaji. Hii itasaidia wananchi kuwa wasimamizi wa moja kwa moja wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

• Serikali iwatumie wataalamu wa masuala ya uchumi walioko nchini badala ya kutumia wanasiasa pekee katika kuandaa bajeti na matumizi ya serikali, pia serikali ijenge utamaduni wa kuwatumia wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali nchini katika kuandaa na kusimamia sera mbali mbali kwaajili ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuheshimu mawazo na maelekezo ya wataalamu katika sekta mbalimbali hata pale yanapotokea majanga yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu. Kwa kufanya hivi, tutapunguza au kudhibiti matamko ya kisiasa katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu kama vile Afya, Elimu na Uchumi.

Hitimisho
Natoa wito kwa viongozi/wenye mamlaka, na watunga sera wa nchi, maamuzi yoyote wanayofanya yanaathiri au kufaidisha jamii nzima, wao ni sehemu ya jamii na hivyo wataathirika au kufaidika na maamuzi hayo kwa namna moja au nyingine. Ni vyema kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka athari zozote zitakazoisababishwa na maamuzi yao ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Asanteni Sana​
 
Upvote 1.3K
Umeongea mambo ya msingi na umetoa mapendekezo mazuri ila CCM sio watu wanaoweza kupokea ushauri kama huu.Yote haya yanawezekana ila labda siku CCM wametoka madarakani.

Hata wakichukua mawazo haya, utekelezaji wake hautokuwa serious.
Ni kweli kabisa, serikali haijawahi kuwa serious kwenye mambo ya msingi, wanaweza kuyachukua haya mawazo lakini sasa Taasisi watakayoanzisha ikawa kituko sawa na hakuna.
 
Kuna kipindi nilikuwa naamini upinzani utaleta mabadiliko ila mwaka 2015 yaliotokea baada ya Lipumba na wengine kufanya uhuni basi imani yote kwa wapinzani ilipotea, ukiangalia kabisa unaona hakuna wapinzani wa kweli nchi wote ni wapigaji tu.
Ccm, chadema, act, cuf... Wote ni wachumia tumbo tu kwa kweli.
 
Utangulizi
Dira kwa maana fupi ni muelekeo. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision (TDV) 2025 ilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2000 lengo kuu likiwa kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. (tovuti kuu ya serikali)

Melengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni pamoja na kuboresha hali ya maisha ya kila Mtanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani usalama na umoja,kujenga utawala bora,kujenga jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani. (Nukuu kutoka Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025).

Katika andiko hili, nitaangazia malengo makuu matano kama yalivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025. Andiko langu litaangazia pia utekelezaji wa malengo haya na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Katika uhalisia, Maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa yamekua yakitegemea Ilani ya chama tawala pamoja vipaumbele vya Rais aliye madarakani. Mfano halisi ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa madaraja ambao uliingiza nchi katika madeni makubwa na umaskini. Ni wazi kwamba Dira ya Maendeleo ni kijarida tu ambacho kimetengenezwa kutimiza wajibu lakini hakina nafasi kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Serikali imeunda mipango mingi kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo kama vile mpango wa maendeleo wa miaka mitanpo (Five Year Development Plan), MKUKUTA, Mpango wa Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa), Mpango wa maboresho ya utumishi wa Umma,pamoja na Maleongo ya Maendeleo ya Millenia chini ya nchi za Umoja wa Mataifa.

Katika mipango tajwa, yote ina malengo yanayolandana kwa maana ya kutokomeza umaskini kwa kuboresha huduma za afya, elimu, nishati, kilimo, maji, biashara, mahusiano ya kimataifa, ajira, kuboresha utumishi wa umma, kuweka usawa wa kijinsia pamoja na mengine mengi.

Hebu tuangazie miaka kumi nyuma tulinganishe na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na hali halisi ya Watanzania mpaka leo hii.

Hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kuwa duni pamoja na kwamba nchi yetu ipo katika uchumi wa kati wa chini, Mtanzania wa kawaida anashindwa kumudu gharama ndogo za mlo wa siku ilhali tunatangaziwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 7% ( NBS 2019/2020).

Katika kujenga utawala bora, hali imezidi kuwa tete, ni wazi kwamba utawala wa sheria umekua jambo gumu katika nchi yetu hali inayopelekea kutokuwajibika kwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma (Rejea ripoti ya CAG 2020).

Katika Dira ya Mendeleo 2025, serikali imeonyesha nia ya kujenga jamii iliyoelimika na inayojifunza kila siku kulingana na mazingira na nyakati tulizopo, tukirudi kwenye uhalisia, kiwango cha ubora wa elimu zetu hakikidhi viwango vitakavyowawezesha wasomi wetu kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania, shule zetu nyingi hazina waalimu wa kutosha wala vifaa vya kufundishia, matamko ya kisiasa kwa upande mwingine yamekua yakiathiri mifumo ya elimu.

Kwa mfano mnamo mwezi Desemba 2020, Rais JPM aliagiza somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa katika shue za msingi mpaka sekondari, Wizara ya elimu iliandaa machapisho kwa ajili ya somo husika lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani somo hilo lilisitishwa rasmi.

Kwa upande mwingine serikali ilichangia kupotosha jamii badala ya kuelimisha. Nitoe mfano mdogo wa janga la Covid 19. Serikali ilisimama kidete kuuaminisha umma kwamba janga hili ni vita ya mabeberu dhidi yetu badala ya kutumia wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu namna bora ya kujikinga ili kuepuka maambukizi. Serikali ilienda mbali zaidi na kuhamasisha tiba mbadala na njia za asili ambazo zilitumika katika vituo vya afya pia.

Kauli ya serikali pamoja na viongozi wakuu wa nchi imeleta mkanganyiko pamoja na hisia tofauti juu ya janga hili na kusababisha watu kuishi pasipo kuchukua tahadhari hata baada ya serikali kubadili msimamo na kuamua kufuata njia za kitaalamu. Ukijaribu kuongea na watanzania kumi, tisa kati yao wanaogopa chanjo na kuamini kwamba mabeberu wanataka kutumaliza.

View attachment 1862120View attachment 1862121
(picha kutoka mtandaoni)

Katika uboreshaji wa utumishi wa umma, vilio vimekua vingi, utekelezaji wa dhima hii umesahaulika kwa miaka zaidi ya mitano iliyopita, vilio vingi vya wafanyakazi kuhusu nyongeza za mishahara pamoja na kupanda madaraja, makato makubwa, na mishahara duni ambayo haikidhi maisha ya kila siku.

Mambo ya muhimu yaliyotajwa katika utekelezaji wa malengo ya milenia ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimataifa, kutokomeza umaskini wa kipato na njaa. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imepuuza kwa kiasi kikubwa sana mahusiano ya kimataifa kutokana na misimamo ya kiongozi aliyekua madarakani. Vipato vya wananchi vimeshuka kutokana na tozo kubwa katika bidhaa na huduma, mfumuko wa bei umeathiri pembejeo za kilimo na bidhaa mbalimbali, uonevu kwa wafanyabiashara,ubambikaji wa kesi na kodi uliosababisha biashara nyingi kufungwa. Tunao mfano halisi wa sasa katika tozo ya miamala ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi masikini ambao hata kula yao ni ya tabu.

Mapendekezo
• Serikali ianzishe taasisi maalumu kwaajili ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa. Chombo hicho kiwe na kazi ya kuandaa, kusimamia pamoja na kuishauri serikali iliyopo madarakani bila kujali chama.Taasisi hii ihakikishe sera sera na mipango ya taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wizara zina uelekeo mmoja na zinashirikiana ka ukaribu. Kwa mfano suala la kuzalisha wahitimu wenye weledi ni lazima liendane na uboreshaji mfumo wa elimu, kwa hiyo ni lazima wizara ya kazi na wizara ya elimu zishirikiane kubaini mapungufu yanayoonekana kwa wahitimu wanaoajiriwa ili waweze kubaini njia bora ya kuboresha.

Taasisi hii ipewe mamlaka ya kusimamia serikali kama ilivyo bunge na mahakama na kwamba ilani ya chama cha kiongozi aliyeko madarakani ilenge kutafuta au kuonyesha njia sahihi za kuipeleka nchi kule ambako dira inaonyesha, hii itasaidia kutekeleza miradi iliyoachwa au iliyoanzishwa na kiongozi aliemaliza muda wake, mfano wakati Rais JPM naingia madarakani alisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa madai kwamba mikataba ilikua mibovu na iliyojaa unyonyaji, siku chache baada ya Rais Samia kuingia madarakani mapitio ya ujenzi wa bandari yameanza, hii ni kwa sababu hakuna mfumo wa kusimamia viapaumbele vya maendeleo ya Taifa badala yake kila kiongozi anajiamulia kile anachopenda.

• Ipatikane katiba imara ambayo itasaidia kudhibiti na kusimamia viongozi walioko madarakani na hata baada ya kustaafu kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Marekani na Afrika ya Kusini. Hii itahakikisha viongozi wote wanafanya kazi kwa kuheshimu haki za binadamu na sheria na taratibu zilizopo bila kuathiri malengo ya Taifa kwa ujumla. Katiba imara pia itasaidia kuweka uwajibikaji na usawa kati ya watumishi/viongozi, kuondoa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• Serikali ijikite zaidi katika kuvumbua vyanzo vipya vya mapato badala ya kujikita katika kuongeza kodi katika huduma mbalimbali za kijamii ili kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na badala yake wananchi wapate unafuu wa maisha. Mfano sekta ya utalii na madini zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama tukiweka usimamizi mzuri na mifumo ya kuaminika ili kuepusha mianya ya ubadhirifu. Pia serikali ijikite katika kuboresha mfumo wa elimu ili kuruhusu vijana wengi kujiajiri katika nyanja mbalimbali badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

• Bajeti za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge zisitumike kinyume na lengo ili tuweze kutekeleza mipango iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa serikali. Huko nyuma tulishuhudia pesa zikipelekwa katika matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge hali iliyochangia kukwamishwa kwa miradi mingi ya maendeleo iliyoidhinishwa na bunge. Bajeti inayoidhinishwa pia iende sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

• Serikali iunde mfumo shirikishi utakaosaidia wananchi kushiriki katika kuonyesha vipaumbele vya maendeleo pamoja na utekelezaji. Hii itasaidia wananchi kuwa wasimamizi wa moja kwa moja wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

• Serikali iwatumie wataalamu wa masuala ya uchumi walioko nchini badala ya kutumia wanasiasa pekee katika kuandaa bajeti na matumizi ya serikali, pia serikali ijenge utamaduni wa kuwatumia wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali nchini katika kuandaa na kusimamia sera mbali mbali kwaajili ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuheshimu mawazo na maelekezo ya wataalamu katika sekta mbalimbali hata pale yanapotokea majanga yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu. Kwa kufanya hivi, tutapunguza au kudhibiti matamko ya kisiasa katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu kama vile Afya, Elimu na Uchumi.

Hitimisho
Natoa wito kwa viongozi/wenye mamlaka, na watunga sera wa nchi, maamuzi yoyote wanayofanya yanaathiri au kufaidisha jamii nzima, wao ni sehemu ya jamii na hivyo wataathirika au kufaidika na maamuzi hayo kwa namna moja au nyingine. Ni vyema kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka athari zozote zitakazoisababishwa na maamuzi yao ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Asanteni Sana​
[emoji848]
 
kumekuwa na mipango mingi kuhusiana na dira za Taifa toka tuo wakati wa chama kimoja labda nikukumbushe moja ya mkakati uliokuwepo chini ya chama kimoja ni kumaliza tatizo la maji mwaka 2000 lakini mpaka sasa hivi bado tuna tatizo la maji na hakuna dalili ya kumalidhika sasa hivi.
Sioni tatizo kwa chama tawala kuandaa dira au ilani za uchaguzi lakini tatizo kubwa ni chama kushindwa kusimamia serikali kutekeleza ilani zao au dira zao.
Baada ya Mkapa kuingia madarakani alisema wazi ilani ya chama haitekelezeki lakini hata marais wote waliokuja kuanzia Mwinyi mpaka rais wa sasa wamekuwa wakitekeleza mambo kwa jinsi wanavyoona wao bila kufata mwongozo au ilani ya chama na kwa aina ya mtindo huu huwezi kutegemea kufanikiwa kwa jambo lolote china wameweza sababu chama chao kimeweza kuisimamia serikali kikamilifu na sasa hivi china wametokomeza ugonjwa wa malaria mbali na kuwa na nguvu kubwa kiuchumi.
Tatizo moja kubwa tulilonalo tumekuwa mabingwa wa kuandaa maandiko lakini tumeshindwa kufanya tathimini kujua ni kwa kiasi gani tumetekeleza kile kilichoandaliwa.
Makamu wa rais kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa fedha alikuwa akihusika kuandaa dira za maendeleo ya taifa lakini leo ukimwuliza kile mlichokuwa mnaandaa kimefikia wapi sidhani kama ana jibu la kukupa.
Kama chama cha mapinduzi kingekuwa imara kingeweza kuandaa dira ya maendeleo hata ya miaka 50 lakini kikawa kinaisimamia serikali au rais anayechaguliwa kuitekeleza dira hiyo badala ya kila rais anayeingia kuingia na miradi yake kama bwawa la umeme, treni ya mwendo kasi, kuhamisha makao makuu dodoma au kuanzisha somo la historia mpya.
 
Tukihoji tunaambiwa hamieni burundi
Ukitaka dalali wa nyumba, vyumba, viwanja. Nicheki PM. Mwenzako nshatafuta hifadhi tayari. Ila hawajui kiswahili. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]

Yule Waziri ni kichwa maji kweli kweli, yani mwananchi ndio anakulipa "Mshahara wa ubunge & Mshahara wa Uwaziri (Mishahara Miwili Kwa Pamoja)" hapo hapo anakulipa "Posho Za Ubunge & Posho Za Uwaziri (Posho Mbili Kwa Pamoja)" bado anakuwekea Mafuta, Vocha, Umeme, Maji n.k

Halafu unamletea kiburi na unamfukuza kwenye nchi yake??? Ina maana wananchi walikosea sana kukuchagua ukawawakilishe bungeni (Au pengine ndio athari za kuiba kura hizi kufikia hatua wabunge wanakuwa na dharau kwa wananchi kwasababu hawaja chaguliwa na wananchi)

Abrianna

Rasilimali zipo za aina tatu kwa uelewa wangu mdogo rafiki, kuna rasilimali; Rasilimali Watu (Human Resource), Rasilimali Za Kutengenezwa Na Binaadamu (Man Made Resource) na Rasilimali Asilia (Natural Resource).

Katika dira hio ambao Tanzania iliojiwekea, kwa upande wangu haikuwekea mipaka (Borders) thabiti ya kutofautisha umuhimu wa hizo rasilimali na mchango wake katika kufikia malengo.

Imeshindwa (Naweza kusema) kutambua na kuwakinisha rasilimali kwa umakini. It failed to identify state resources and support programs.

Support programs zinafanywa kienyeji bila mikakati madhubuti wala malengo, mfano ujenzi wa miundo-mbinu (Ref: Daraja La Kigamboni, Fly-Overs, Bus Stands e.t.c).

Vitu hivo vinajengwa kweli, wala sipingi, tena ni vizuri sana, na vinaonekana na kuvutia haswaa. Serikali inajenga kwa mantiki na nia nzuri.

● Ila kwa kutumia resource zipi na kwa dira ipi??? Mikopo??? Kwa kupandisha kodi kandamizi??? Kwa kutumia Polisi kubambikiza makosa ya barabarani madereva??? Kwa kutumia TRA kubambikiza wafanyabiashara kodi??? Kutumia DPP kubambikiza raia kesi za uhujumu uchumi???

My vision, serikali ina "BOMOA SEKTA FULANI" ili "IJENGE SEKTA FULANI", yani lets say inabomoa Sekta ya biashara ili ijenge sekta ya miundo-mbinu. So we as Tanzania are going no where.

Tuje kwenye, Matumizi Ya Rasilimali kwenye Bunge na Wizara.

Matumizi ya rasilimali fedha kwenye serikali, sekta ya Bunge na Wizara ni mabovu mabovu mabovu kweli kweli, yaani ni kichefuchefu sana.

Mfano, Waziri asiekua na utendaji mzuri, anapokea;

1) Mishahara Miwili (Mshahara Wa Uwaziri na Mshahara Wa Ubunge).

2) Posho na marupurupu mawili (Posho Kama Mbunge na Posho Kama Waziri).

Tuna Mawaziri na Manaibu Waziri wangapi wanaopokea hivo??? Jibu ni WOTE!!!

● Sio matumizi mabaya ya rasilimali haya??? Kwanini tusiwe na katiba/sheria imara kwamba mtu akiwa Waziri/Naibu Waziri hatakiwi kuwa mbunge. Waziri awe anaitwa bungeni pale Wizara yake inapotakiwa kwenda kuhojiwa tu na bunge, au pale anapopeleka budget ya Wizara yake bungeni tu, na sio kuingia katika kila kikao cha bunge wala kupokea mishahara na posho mbili mbili.

Tukija kwenye Rasilimali Watu (Human Resources) serikali haina dira kwenye kukuza hii sekta, ajira hakuna, serikali bado inaongeza kodi kila kukicha kuwakandamiza rasilimali watu na kuiangamiza hii sekta kabisa. Watu wastaafu na waliosimamishwa kazi hawapewi mafao yao ili waweze kujiajiri kwa kufungua biashara na mengineyo.

● Serikali kuongeza tozo kwenye miamala ya simu ni kuangamiza mzunguko wa fedha kitaifa. Serikali kuweka kodi kwenye uvuvi wa kienyeji ni kuangamiza sekta ya uvuvi na wavuvi. Serikali kuweka kodi kwenye kilimo na kuongeza kodi kwenye mbolea (Kutoka Sh 42,000/= mpaka kuwa 92,000/= kwa mfuko mmoja) ni kuua ajira.

Tuje kwenye dira ya Rasilimali Za Kutengenezwa na Binaadamu (Man Made Resources).

Tanzania hatuna dira nzuri katika sekta hii. Mfano, Tanzania tuna ardhi kubwa sana, tuna mito na maziwa, ila tuna dira gani ya kuitumia ipasavyo kwa miaka 50 au 100 ijayo??? Hatuna dira.

● Tulipaswa kuwa na dira, mfano ya miaka 50 au 100 ijayo "KUIPITA CONGO KWA KUWA NA MISITU YA MITI". Kivipi, ingewekwa sheria kila wilaya nchini (Dira ikiongozwa na Wakuu Wa Wilaya) katika kupanda na kukuza kwa kumwagilia miti ya mbao/biashara kwa mwaka isipungue miti ya mbao 5,000.

Kwa miaka miwili kila wilaya inakua imepanda na kukuza miti 10,000. Na kwa miaka 4 inakua imepanda miti 20,000. Mpaka kufikia miaka 50 tunakua tumepanda miti 250,000 katika Wilaya moja nchini (Ukipiga mahesabu ya wilaya zote nchini kwa miaka 50 basi idadi inakua kubwa sana sana). Congo na hata Brazil wangesubiri kwa idadi ya misitu kwa Tanzania.

Hii ingefufua vyanzo vya maji, kama mito na maziwa, ambavyo vimekauka. Pia tungekua na reserve ya miti ya akiba ambayo tungeweza kuuza kwa Trillions of Dollars. Nchi ingekua tajiri.

Mtazamo wangu,

Serikali ianze kufumuafumua taasisi za serikali kwanza na kuzifuma upya, tuwe na taasisi imara zenye kuwajibishwa na wananchi, pia serikali kwa kutumia bunge ifute/ibadili sheria kandamizi na mbovu ili ziwe sheria rafiki na flexible, halafu ndio tuje kufanya mabadiliko za dira kama taifa.

Kwasasa dira yetu ni "ANAEZICHOTA RASILIMALI ZETU (Watendaji Wa Serikali kama Mawaziri) ANATAKA AENDELEE KUZICHOTA, NA ASIEPATA KITU (Mwananchi) AENDELEE KUTOKUPATA KITU" wakati miaka inasonga mbele. Theory ni simple kwa sasa, ukitaka utajiri basi nenda kagombee cheo bungeni au serikalini.

I stand to be corrected. Ni mtazamo wangu binafsi huo.
 
Ukitaka dalali wa nyumba, vyumba, viwanja. Nicheki PM. Mwenzako nshatafuta hifadhi tayari. Ila hawajui kiswahili. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]

Yule Waziri ni kichwa maji kweli kweli, yani mwananchi ndio anakulipa "Mshahara wa ubunge & Mshahara wa Uwaziri (Mishahara Miwili Kwa Pamoja)" hapo hapo anakulipa "Posho Za Ubunge & Posho Za Uwaziri (Posho Mbili Kwa Pamoja)" bado anakuwekea Mafuta, Vocha, Umeme, Maji n.k

Halafu unamfukuza kwenye nchi yake?

Abrianna

Rasilimali zipo za aina nyingi kwa uelewa wangu mdogo rafiki, kuna rasilimali; Rasilimali Watu na Rasilimali
Umezungumza vyema kuhusu rasilimalia
 
kumekuwa na mipango mingi kuhusiana na dira za Taifa toka tuo wakati wa chama kimoja labda nikukumbushe moja ya mkakati uliokuwepo chini ya chama kimoja ni kumaliza tatizo la maji mwaka 2000 lakini mpaka sasa hivi bado tuna tatizo la maji na hakuna dalili ya kumalidhika sasa hivi.
Sioni tatizo kwa chama tawala kuandaa dira au ilani za uchaguzi lakini tatizo kubwa ni chama kushindwa kusimamia serikali kutekeleza ilani zao au dira zao.
Baada ya Mkapa kuingia madarakani alisema wazi ilani ya chama haitekelezeki lakini hata marais wote waliokuja kuanzia Mwinyi mpaka rais wa sasa wamekuwa wakitekeleza mambo kwa jinsi wanavyoona wao bila kufata mwongozo au ilani ya chama na kwa aina ya mtindo huu huwezi kutegemea kufanikiwa kwa jambo lolote china wameweza sababu chama chao kimeweza kuisimamia serikali kikamilifu na sasa hivi china wametokomeza ugonjwa wa malaria mbali na kuwa na nguvu kubwa kiuchumi.
Tatizo moja kubwa tulilonalo tumekuwa mabingwa wa kuandaa maandiko lakini tumeshindwa kufanya tathimini kujua ni kwa kiasi gani tumetekeleza kile kilichoandaliwa.
Makamu wa rais kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa fedha alikuwa akihusika kuandaa dira za maendeleo ya taifa lakini leo ukimwuliza kile mlichokuwa mnaandaa kimefikia wapi sidhani kama ana jibu la kukupa.
Kama chama cha mapinduzi kingekuwa imara kingeweza kuandaa dira ya maendeleo hata ya miaka 50 lakini kikawa kinaisimamia serikali au rais anayechaguliwa kuitekeleza dira hiyo badala ya kila rais anayeingia kuingia na miradi yake kama bwawa la umeme, treni ya mwendo kasi, kuhamisha makao makuu dodoma au kuanzisha somo la historia mpya.
Umesema vyema rafiki,asante sana
 
Ukitaka dalali wa nyumba, vyumba, viwanja. Nicheki PM. Mwenzako nshatafuta hifadhi tayari. Ila hawajui kiswahili. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]

Yule Waziri ni kichwa maji kweli kweli, yani mwananchi ndio anakulipa "Mshahara wa ubunge & Mshahara wa Uwaziri (Mishahara Miwili Kwa Pamoja)" hapo hapo anakulipa "Posho Za Ubunge & Posho Za Uwaziri (Posho Mbili Kwa Pamoja)" bado anakuwekea Mafuta, Vocha, Umeme, Maji n.k

Halafu unamfukuza kwenye nchi yake?

Abrianna

Rasilimali zipo za aina tatu kwa uelewa wangu mdogo rafiki, kuna rasilimali; Rasilimali Watu (Human Resource), Rasilimali Za Kutengenezwa Na Binaadamu (Man Made Resource) na Rasilimali Asilia (Natural Resource).

Katika dira hio ambao Tanzania iliojiwekea, kwa upande wangu haikuwekea mipaka (Borders) thabiti ya kutofautisha umuhimu wa hizo rasilimali na mchango wake katika kufikia malengo.

Imeshindwa (Naweza kusema) kutambua na kuwakinisha rasilimali kwa umakini. It failed to idenrify state resources and support programs.

Support programs zinafanywa kienyeji bila mikakati madhubuti wala malengo, mfano ujenzi wa miundo-mbinu (Ref: Daraja La Kigamboni, Fly-Overs, Bus Stands e.t.c).

Vitu hivo vinajengwa kweli, wala sipingi, tena ni vizuri sana, na vinaonekana na kuvutia haswaa. Serikali inajenga kwa mantiki na nia nzuri.

● Ila kwa kutumia resource zipi na kwa dira ipi??? Mikopo??? Kwa kupandisha kodi kandamizi??? Kwa kutumia Polisi kubambikiza makosa ya barabarani madereva??? Kwa kutumia TRA kubambikiza wafanyabiashara kodi??? Kutumia DPP kubambikiza raia kesi za uhujumu uchumi???

My vision, serikali ina "BOMOA SEKTA FULANI" ili "IJENGE SEKTA FULANI", yani lets say inabomoa Sekta ya biashara ili ijenge sekta ya miundo-mbinu. So we as Tanzania are going no where.

Tuje kwenye, Bunge na Wizara.

Matumizi ya rasilimali fedha kwenye sekta ya Bunge na Wizara ni mabovu mabovu mabovu kweli kweli, yaani ni kichefuchefu sana.

Mfano, Waziri asiekua na utendaji mzuri, anapokea;

1) Mishahara Miwili (Mshahara Wa Uwaziri na Mshahara Wa Ubunge).

2) Posho na marupurupu mawili (Posho Kama Mbunge na Posho Kama Waziri).

Tuna Mawaziri na Manaibu Waziri wangapi wanaopokea hivo??? Jibu ni WOTE!!!

● Sio matumizi mabaya ya rasilimali haya??? Kwanini tusiwe na katiba/sheria imara kwamba mtu akiwa Waziri/Naibu Waziri hatakiwi kuwa mbunge. Waziri awe anaitwa bungeni pale Wizara yake inapotakiwa kwenda kuhojiwa tu na bunge, au pale anapopeleka budget ya Wizara yake bungeni tu, na sio kuingia katika kila kikao cha bunge.

Mtazamo wangu, serikali ianze kufumuafumua taasisi za serikali kwanza na kuzifuma upya, tuwe na taasisi imara zenye kuwajibishwa na wananchi, halafu ndio tuje kufanya mabadiliko za dira kama taifa.

I stand to be corrected. Ni mtazamo wangu binafsi huo.
Alexander The Great umeongea mambo ya msingi sana, usimamizi wa dira ni mgumu pasipo kuwa na sheria imara

Mifumonya serikali imeoza ikiwa ni pamoja na vypmbo vinavyoisimamia serikali, mpaka mahakama haiaminiki, kwa maana hiyo bila kufumua mifumo hata katiba mpya haitasaidia

Katiba ya sasa haiheshimiwi, hata mahakama ambayo ni chombo cha haki kinaheshimu maagizo ya kisiasa kuliko katiba, kwa namna hiyo nadhani kuna kazi kubwa ya kutengeneza mfumo

Ila bado naona uzalendo ni kitu adimu na ndio chanzo cha matatizo mengi katika mifumo yetu
 
Mimi naona viongozi wa upinzani wa kuaminika wapo. Ila watanzania raia wa kuaminika ndo hawapo. Wapo tu kama mifugo. Hata ufanyike ukatili wa namna gani na unyanyasaji hatuchukui hatua.

Lakini wakati huo huo tunataka akina Lissu wakatupiganie pamoja na ku risk maisha yao.
Kama hizi tozo za mihamala ya simu zimeshindwa kutuchukulisha hatua tukubali tu kwamba watanzania ni watu waoga na wabinafsi zaidi duniani. Kila mmoja anafuata yake. Leo mmoja akipigwa risasi kwa kutetea maslahi ya nchi anaambiwa ametafuta mwenyewe na ana kiherehere.

Tupo kwenye kipindi tukipewa haki zetu tunaona ni favour na tunawapigia magoti na kuwashukuru waliotunyima haki zetu kumi then wakaturejeshea 3. Tunawasifu huku tukisema wanaupiga mwingi. Lakini kama Mungu aishivyo kila mtu atavuna na tutatolea hesabu ya kila neno na tendo tumefanya hapa duniani. Hapo ndipo Mungu anabaki kuwa juu sana
Taja viongozi wa upinzani japo wa3 wa kuaminika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka dalali wa nyumba, vyumba, viwanja. Nicheki PM. Mwenzako nshatafuta hifadhi tayari. Ila hawajui kiswahili. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]

Yule Waziri ni kichwa maji kweli kweli, yani mwananchi ndio anakulipa "Mshahara wa ubunge & Mshahara wa Uwaziri (Mishahara Miwili Kwa Pamoja)" hapo hapo anakulipa "Posho Za Ubunge & Posho Za Uwaziri (Posho Mbili Kwa Pamoja)" bado anakuwekea Mafuta, Vocha, Umeme, Maji n.k

Halafu unamfukuza kwenye nchi yake?

Abrianna

Rasilimali zipo za aina tatu kwa uelewa wangu mdogo rafiki, kuna rasilimali; Rasilimali Watu (Human Resource), Rasilimali Za Kutengenezwa Na Binaadamu (Man Made Resource) na Rasilimali Asilia (Natural Resource).

Katika dira hio ambao Tanzania iliojiwekea, kwa upande wangu haikuwekea mipaka (Borders) thabiti ya kutofautisha umuhimu wa hizo rasilimali na mchango wake katika kufikia malengo.

Imeshindwa (Naweza kusema) kutambua na kuwakinisha rasilimali kwa umakini. It failed to idenrify state resources and support programs.

Support programs zinafanywa kienyeji bila mikakati madhubuti wala malengo, mfano ujenzi wa miundo-mbinu (Ref: Daraja La Kigamboni, Fly-Overs, Bus Stands e.t.c).

Vitu hivo vinajengwa kweli, wala sipingi, tena ni vizuri sana, na vinaonekana na kuvutia haswaa. Serikali inajenga kwa mantiki na nia nzuri.

● Ila kwa kutumia resource zipi na kwa dira ipi??? Mikopo??? Kwa kupandisha kodi kandamizi??? Kwa kutumia Polisi kubambikiza makosa ya barabarani madereva??? Kwa kutumia TRA kubambikiza wafanyabiashara kodi??? Kutumia DPP kubambikiza raia kesi za uhujumu uchumi???

My vision, serikali ina "BOMOA SEKTA FULANI" ili "IJENGE SEKTA FULANI", yani lets say inabomoa Sekta ya biashara ili ijenge sekta ya miundo-mbinu. So we as Tanzania are going no where.

Tuje kwenye, Bunge na Wizara.

Matumizi ya rasilimali fedha kwenye sekta ya Bunge na Wizara ni mabovu mabovu mabovu kweli kweli, yaani ni kichefuchefu sana.

Mfano, Waziri asiekua na utendaji mzuri, anapokea;

1) Mishahara Miwili (Mshahara Wa Uwaziri na Mshahara Wa Ubunge).

2) Posho na marupurupu mawili (Posho Kama Mbunge na Posho Kama Waziri).

Tuna Mawaziri na Manaibu Waziri wangapi wanaopokea hivo??? Jibu ni WOTE!!!

● Sio matumizi mabaya ya rasilimali haya??? Kwanini tusiwe na katiba/sheria imara kwamba mtu akiwa Waziri/Naibu Waziri hatakiwi kuwa mbunge. Waziri awe anaitwa bungeni pale Wizara yake inapotakiwa kwenda kuhojiwa tu na bunge, au pale anapopeleka budget ya Wizara yake bungeni tu, na sio kuingia katika kila kikao cha bunge.

Tukija kwenye Rasilimali Watu (Human Resources) serikali haina dira kwenye kukuza hii sekta, ajira hakuna, serikali bado inaongeza kodi kila kukicha kuwakandamiza rasilimali watu na kuiangamiza hii sekta kabisa.

● Serikali kuongeza tozo kwenye miamala ya simu ni kuangamiza mzunguko wa fedha kitaifa. Serikali kuweka kodi kwenye uvuvi wa kienyeji ni kuangamiza sekta ya uvuvi na wavuvi. Serikali kuweka kodi kwenye kilimo na kuongeza kodi kwenye mbolea (Kutoka Sh 42,000/= mpaka kuwa 92,000/= kwa mfuko mmoja) ni kuua ajira.

Mtazamo wangu, serikali ianze kufumuafumua taasisi za serikali kwanza na kuzifuma upya, tuwe na taasisi imara zenye kuwajibishwa na wananchi, halafu ndio tuje kufanya mabadiliko za dira kama taifa. Kwasasa dira yetu ni "ANAEZICHOTA RASILIMALI ZETU (Watendaji Wa Serikali kama Mawaziri) ANATAKA AENDELEE KUZICHOTA, NA ASIEPATA KITU (Mwananchi) AENDELEE KUTOKUPATA KITU"

I stand to be corrected. Ni mtazamo wangu binafsi huo.
Hivi Alexander The Great uliishia wapi na vile vitambi[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Umeongea mambo ya msingi na umetoa mapendekezo mazuri ila CCM sio watu wanaoweza kupokea ushauri kama huu.Yote haya yanawezekana ila labda siku CCM wametoka madarakani.

Hata wakichukua mawazo haya, utekelezaji wake hautokuwa serious.
Wenyewe wana wimbo wao wanakwambia ccm ni ile ile oooh ni ile ileeee
 
Wapinzani hawataki katiba kwaajili ya maendeleo ya nchi hii, wanataka katiba kwaajili ya kuingia madarakani tu.
Nakumbuka warioba alisema wanasiasa wanataka katiba kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa na sio maslahi wa wananchi
 
Back
Top Bottom