SoC01 Umuhimu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotekelezeka kwa wakati na kwa kuzingatia rasilimali zilizopo

Stories of Change - 2021 Competition

Abrianna

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
4,696
Reaction score
15,390
Utangulizi
Dira kwa maana fupi ni muelekeo. Dira ya Maendeleo ya Tanzania (Tanzania Development Vision (TDV) 2025 ilianzishwa mwaka 1994 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1999 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2000 lengo kuu likiwa kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. 'www.tanzania.go.tz' (tovuti kuu ya serikali)

Melengo makuu matano yalioainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025 ni pamoja na kuboresha hali ya maisha ya kila Mtanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani usalama na umoja,kujenga utawala bora,kujenga jamii iliyoelimika na kujenga uchumi imara unaokabiliana na ushindani. (Nukuu kutoka Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025).

Katika andiko hili, nitaangazia malengo makuu matano kama yalivyoainishwa katika Dira ya Maendeleo 2025. Andiko langu litaangazia pia utekelezaji wa malengo haya na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Katika uhalisia, Maendeleo ya Nchi yetu kwa asilimia kubwa yamekua yakitegemea Ilani ya chama tawala pamoja vipaumbele vya Rais aliye madarakani. Mfano halisi ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa madaraja ambao uliingiza nchi katika madeni makubwa na umaskini. Ni wazi kwamba Dira ya Maendeleo ni kijarida tu ambacho kimetengenezwa kutimiza wajibu lakini hakina nafasi kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Serikali imeunda mipango mingi kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo kama vile mpango wa maendeleo wa miaka mitanpo (Five Year Development Plan), MKUKUTA, Mpango wa Big Results Now (Matokeo Makubwa Sasa), Mpango wa maboresho ya utumishi wa Umma,pamoja na Maleongo ya Maendeleo ya Millenia chini ya nchi za Umoja wa Mataifa.

Katika mipango tajwa, yote ina malengo yanayolandana kwa maana ya kutokomeza umaskini kwa kuboresha huduma za afya, elimu, nishati, kilimo, maji, biashara, mahusiano ya kimataifa, ajira, kuboresha utumishi wa umma, kuweka usawa wa kijinsia pamoja na mengine mengi.

Hebu tuangazie miaka kumi nyuma tulinganishe na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na hali halisi ya Watanzania mpaka leo hii.

Hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kuwa duni pamoja na kwamba nchi yetu ipo katika uchumi wa kati wa chini, Mtanzania wa kawaida anashindwa kumudu gharama ndogo za mlo wa siku ilhali tunatangaziwa uchumi wetu umekua kwa asilimia 7% ( NBS 2019/2020).

Katika kujenga utawala bora, hali imezidi kuwa tete, ni wazi kwamba utawala wa sheria umekua jambo gumu katika nchi yetu hali inayopelekea kutokuwajibika kwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma (Rejea ripoti ya CAG 2020).

Katika Dira ya Mendeleo 2025, serikali imeonyesha nia ya kujenga jamii iliyoelimika na inayojifunza kila siku kulingana na mazingira na nyakati tulizopo, tukirudi kwenye uhalisia, kiwango cha ubora wa elimu zetu hakikidhi viwango vitakavyowawezesha wasomi wetu kuingia katika ushindani ndani na nje ya Tanzania, shule zetu nyingi hazina waalimu wa kutosha wala vifaa vya kufundishia, matamko ya kisiasa kwa upande mwingine yamekua yakiathiri mifumo ya elimu.

Kwa mfano mnamo mwezi Desemba 2020, Rais JPM aliagiza somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa katika shue za msingi mpaka sekondari, Wizara ya elimu iliandaa machapisho kwa ajili ya somo husika lakini baada ya Rais Samia kuingia madarakani somo hilo lilisitishwa rasmi.

Kwa upande mwingine serikali ilichangia kupotosha jamii badala ya kuelimisha. Nitoe mfano mdogo wa janga la Covid 19. Serikali ilisimama kidete kuuaminisha umma kwamba janga hili ni vita ya mabeberu dhidi yetu badala ya kutumia wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu namna bora ya kujikinga ili kuepuka maambukizi. Serikali ilienda mbali zaidi na kuhamasisha tiba mbadala na njia za asili ambazo zilitumika katika vituo vya afya pia.

Kauli ya serikali pamoja na viongozi wakuu wa nchi imeleta mkanganyiko pamoja na hisia tofauti juu ya janga hili na kusababisha watu kuishi pasipo kuchukua tahadhari hata baada ya serikali kubadili msimamo na kuamua kufuata njia za kitaalamu. Ukijaribu kuongea na watanzania kumi, tisa kati yao wanaogopa chanjo na kuamini kwamba mabeberu wanataka kutumaliza.
1626861526209.png
1626861576665.png

(picha kutoka mtandaoni)

Katika uboreshaji wa utumishi wa umma, vilio vimekua vingi, utekelezaji wa dhima hii umesahaulika kwa miaka zaidi ya mitano iliyopita, vilio vingi vya wafanyakazi kuhusu nyongeza za mishahara pamoja na kupanda madaraja, makato makubwa, na mishahara duni ambayo haikidhi maisha ya kila siku.

Mambo ya muhimu yaliyotajwa katika utekelezaji wa malengo ya milenia ni pamoja na kukuza mahusiano ya kimataifa, kutokomeza umaskini wa kipato na njaa. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imepuuza kwa kiasi kikubwa sana mahusiano ya kimataifa kutokana na misimamo ya kiongozi aliyekua madarakani. Vipato vya wananchi vimeshuka kutokana na tozo kubwa katika bidhaa na huduma, mfumuko wa bei umeathiri pembejeo za kilimo na bidhaa mbalimbali, uonevu kwa wafanyabiashara,ubambikaji wa kesi na kodi uliosababisha biashara nyingi kufungwa. Tunao mfano halisi wa sasa katika tozo ya miamala ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi masikini ambao hata kula yao ni ya tabu.

Mapendekezo
• Serikali ianzishe taasisi maalumu kwaajili ya kuandaa na kusimamia Dira ya Maendeleo ya Taifa. Chombo hicho kiwe na kazi ya kuandaa, kusimamia pamoja na kuishauri serikali iliyopo madarakani bila kujali chama.Taasisi hii ihakikishe sera sera na mipango ya taasisi mbalimbali za serikali pamoja na wizara zina uelekeo mmoja na zinashirikiana ka ukaribu. Kwa mfano suala la kuzalisha wahitimu wenye weledi ni lazima liendane na uboreshaji mfumo wa elimu, kwa hiyo ni lazima wizara ya kazi na wizara ya elimu zishirikiane kubaini mapungufu yanayoonekana kwa wahitimu wanaoajiriwa ili waweze kubaini njia bora ya kuboresha.

Taasisi hii ipewe mamlaka ya kusimamia serikali kama ilivyo bunge na mahakama na kwamba ilani ya chama cha kiongozi aliyeko madarakani ilenge kutafuta au kuonyesha njia sahihi za kuipeleka nchi kule ambako dira inaonyesha, hii itasaidia kutekeleza miradi iliyoachwa au iliyoanzishwa na kiongozi aliemaliza muda wake, mfano wakati Rais JPM naingia madarakani alisitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kwa madai kwamba mikataba ilikua mibovu na iliyojaa unyonyaji, siku chache baada ya Rais Samia kuingia madarakani mapitio ya ujenzi wa bandari yameanza, hii ni kwa sababu hakuna mfumo wa kusimamia viapaumbele vya maendeleo ya Taifa badala yake kila kiongozi anajiamulia kile anachopenda.

• Ipatikane katiba imara ambayo itasaidia kudhibiti na kusimamia viongozi walioko madarakani na hata baada ya kustaafu kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Marekani na Afrika ya Kusini. Hii itahakikisha viongozi wote wanafanya kazi kwa kuheshimu haki za binadamu na sheria na taratibu zilizopo bila kuathiri malengo ya Taifa kwa ujumla. Katiba imara pia itasaidia kuweka uwajibikaji na usawa kati ya watumishi/viongozi, kuondoa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

• Serikali ijikite zaidi katika kuvumbua vyanzo vipya vya mapato badala ya kujikita katika kuongeza kodi katika huduma mbalimbali za kijamii ili kupunguza mzigo mkubwa wa kodi kwa wananchi na badala yake wananchi wapate unafuu wa maisha. Mfano sekta ya utalii na madini zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama tukiweka usimamizi mzuri na mifumo ya kuaminika ili kuepusha mianya ya ubadhirifu. Pia serikali ijikite katika kuboresha mfumo wa elimu ili kuruhusu vijana wengi kujiajiri katika nyanja mbalimbali badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini.

• Bajeti za maendeleo zilizoidhinishwa na bunge zisitumike kinyume na lengo ili tuweze kutekeleza mipango iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa serikali. Huko nyuma tulishuhudia pesa zikipelekwa katika matumizi ambayo hayakuidhinishwa na bunge hali iliyochangia kukwamishwa kwa miradi mingi ya maendeleo iliyoidhinishwa na bunge. Bajeti inayoidhinishwa pia iende sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

• Serikali iunde mfumo shirikishi utakaosaidia wananchi kushiriki katika kuonyesha vipaumbele vya maendeleo pamoja na utekelezaji. Hii itasaidia wananchi kuwa wasimamizi wa moja kwa moja wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

• Serikali iwatumie wataalamu wa masuala ya uchumi walioko nchini badala ya kutumia wanasiasa pekee katika kuandaa bajeti na matumizi ya serikali, pia serikali ijenge utamaduni wa kuwatumia wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali nchini katika kuandaa na kusimamia sera mbali mbali kwaajili ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuheshimu mawazo na maelekezo ya wataalamu katika sekta mbalimbali hata pale yanapotokea majanga yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu. Kwa kufanya hivi, tutapunguza au kudhibiti matamko ya kisiasa katika mambo nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa kitaalamu kama vile Afya, Elimu na Uchumi.

Hitimisho
Natoa wito kwa viongozi/wenye mamlaka, na watunga sera wa nchi, maamuzi yoyote wanayofanya yanaathiri au kufaidisha jamii nzima, wao ni sehemu ya jamii na hivyo wataathirika au kufaidika na maamuzi hayo kwa namna moja au nyingine. Ni vyema kufanya uchambuzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ili kuepuka athari zozote zitakazoisababishwa na maamuzi yao ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Asanteni Sana​
 
Upvote 1.3K
Mkuu ni kama ulikua kichwani kwangu aisee, hii kitu niliiwaza enzi za Jiwe baada ya kuona anawaambia wananchi wakichagua upinzani ahtawaletea maendeleo.nikajisemea ni heri kuwe na kitu kitakachosimamia maendeleo bila kujali itikadi za vyama au personal interest za Raisi
Badala ya kutengeneza mfumo ujiendeshe wenyewe tunatengeneza mtu wa kuendesha kila kitu
 
View attachment 1862120View attachment 1862121

Umeandika vizuri sana. Kwa kifupi, DIRA ndio chanzo kikubwa cha mafanikio kwa sababu inakuwa ndio common reference point.

Na kawaida suala la dira linatakiwa liwe jumuishi kwa makundi yote ya jamii. Uwepo wa dira katika nyanja zote muhimu za kiuchumi, kijamii na kisiasa inafanya jamii iwe na uelekeo mmoja na malengo yanayoinfaisha jamii nzima.

Hata hivyo suala la dira ni lazima liwe controlled na nyenzo zingine za kisheria ili uandaaji na utekelezaji wa dira hiyo ulindwe.
 
Asante sana mkuu kwa maoni yako
 
Kwanza nitoe pongezi kwa uzi uliobeba maudhui yenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
Hizi ndio mada zinazofaa kutiliwa mkazo na vijana ili kuleta mapinduzi ya kisiasa,kiutawala na kiuchumi pia.
Kwa kifupi Nchi yetu ilikuwa ni Taifa lililofeli kiuchumi japokuwa tuna utajiri wa rasilimali ambazo zingesimamiwa ipasavyo tungefika mbali.
Katika miaka mitano iliyopita chini ya utawala wa JPM niwapongeze kwa kuipandisha uchumi wa kiujumla wa nchi na kuingia katika uchumi wa kati na najivunia nchi yangu sasa iko katika kumi bora ya nchi tajiri Afrika tofauti na miaka ya nyuma ilikuwa ni nchi maskini duniani ikikaribiana na Burundi.
Lakini mbali na kupanda kwa uchumi wa kiujumla wa nchi yetu bado uchumi wa mtu mmoja mmoja ni tatizo raia bado ni maskini.
Tatizo na chanzo cha hili tatizo ni kukosekana kwa muendelezo wa mikakati kutoka awamu moja kwenda awamu nyingine.
Kwa mfano nikitolea mfano katika sekta ya Elimu na Sekta ya Afya awamu mbili zilizopita walijitahidi kuongeza shule na hospitali lakini hazina walimu na madaktari wa kutosha.
Sasa ilitakiwa awamu inayofuatia waendeleze kwa kuwaandaa wataalamu katika hayo majengo yaliyojengwa katika awamu iliyopita lakini badala yake awamu inayofuata hawalioni hilo na wanaanza upya kwa vipaumbele vyao vipya bila kurekebisha makosa ya awamu iliyopita.
Kwa huu utaratibu wa kiutawala itatuchukua miaka 100 kukaribia tunapopataka.
Point nyingine ya kuongezea bado elimu yetu haijakidhi viwango vya kufanya ushindani katika soko la kimataifa.
Mtu aliyeishia form 4 Ghana/Zambia/Kenya/Nigeria ana confidence kubwa ya kujiingiza kwenye soko la ajira la kimataifa mara 10 kumzidi Graduate wa Tanzania.
Hili nimelishuhudia kwa macho yangu baada ya kusafiri kwenye nchi kadhaa.
wasomi wa Tanzania wanawaza wakishamaliza degree wapate kazi Halmashauri wakishapata wamemaliza kazi hakuna challenge mpya tena.
Madini muhimu sana, asante sana kwa maoni yako, ni kweli tunahitaji mfumo endelevu kwa ajili ya mipango ya maendeleo na utekelezaji wake ndio maana nikasema ni lazima dira yetu isimamiwe kikamilifu ili tuwe na muunganiko kutoka awamu moja kwenda awamu nyingine, umetoa mifano mizuri ambayo ni halisi

Kuhusu elimu, kuna mapungufu mengi kama ulivyoeleza na tunahitaji marekebisho katika mfumo mzima wa elimu yetu pamoja na mitaala itakayoendana na dunia ya sasa
 
Tuko sambamba mkuu...tupige kazi, vinginevyo tozo zinatutoa kwenye reli. Niluvyosikia kuna mabadiliko kwenye baraza nikafurahia kwa kujipa moyo waasisi wa tozo wanatolewa nje ya mchezo, baada ya mkeka kuwekwa hadharani nimejikuta nauacha urojo wangu bila hata kuchukua chenji....

Kimsingi haitakaa itokee serikali ikagawa mpunga kwa raia wake, lazima tufanye kazi. Na kuna wakati mtu anailaumu serikali wakati kuna vitu amvavyo vipo kwenye uwezo wake hafanyi.

Hapo namtania serikali ni kama unavyoiendesha familia yako ila katika kiwango kikubwa, sasa kama unapeleka mambo yako namna hii ungekua serikali si ingekua hatari?

Bila shaka kura / vote yako imeenda kwa huu uzi mkuu.
Usinikumbushe ya mkeka wa leo mkuu, watu ni walewale, circle ile ile, mawazo na fikra zile zile hakuna damu mpya
 
Ni sawa nakubaliana na wewe 100%. Nilichotaka kukemea ni ile tabia ya watu kukaa wakilalamika na kutumia mapungufu yaliyopo kama excuse.

Haitatokea mazingira yawe wezeshi na kumridhisha kila mtu. Tuendelee kuwabana wanaohusika waboreshe mazingira huku tukipiga kazi.
Absolutely
 
Jambo la msingi kwenye utawala wa sheria ulio na malengo ya kuwafikishia wananchi wake maendeleo ni pamoja na viongozi kutii viapo vyao vya kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na siyo kutii maigizo ya vyama vyao vya siasa kiasi cha kuathiri uchumi wa nchi na usalama wa Taifa kwa sababu za kisiasa.Mfano awamu iliyopita imefanya mambo mengi kinyume na kiapo,pia awamu hii ilianza vizuri lakini kutokana na maagizo ya chama tawala tayari Serikali inajikanyaga yenyewe.
Amani na umoja huu tunaojivunia uliasisiwa kitambo na Nyerere pamoja na Karume ambayo ilidumu hadi awamu ya nne.Kwa sasa inalazimishwa na vyombo vya ulinzi na usalama wala si kwa mapenzi ya raia wake kama ilivyokua nyuma.Athari yake ni kuwa pale raia watakapokuwa sugu kama tulivyoona kwa Hamza itatuchukua muda kutibu majerha hayo yatakayojitokeza kwa sababu asilimia kubwa ya raia watakuwa sugu na hawatopenda/hawatojali ushauri.
Mungu ibariki Afrika pamoja na viongozi wao wote,Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote bila kujali chama,dini,kabila,kanda,upande fulani wa Muungano,jinsia,rangi,imani,umri,fedha na hali ya maisha.
Nimekupata vizuri mkuu, shukrani kwa mchango mzuri
 
Kwanza nitoe pongezi kwa uzi uliobeba maudhui yenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
Hizi ndio mada zinazofaa kutiliwa mkazo na vijana ili kuleta mapinduzi ya kisiasa,kiutawala na kiuchumi pia.
Kwa kifupi Nchi yetu ilikuwa ni Taifa lililofeli kiuchumi japokuwa tuna utajiri wa rasilimali ambazo zingesimamiwa ipasavyo tungefika mbali.
Katika miaka mitano iliyopita chini ya utawala wa JPM niwapongeze kwa kuipandisha uchumi wa kiujumla wa nchi na kuingia katika uchumi wa kati na najivunia nchi yangu sasa iko katika kumi bora ya nchi tajiri Afrika tofauti na miaka ya nyuma ilikuwa ni nchi maskini duniani ikikaribiana na Burundi.
Lakini mbali na kupanda kwa uchumi wa kiujumla wa nchi yetu bado uchumi wa mtu mmoja mmoja ni tatizo raia bado ni maskini.
Tatizo na chanzo cha hili tatizo ni kukosekana kwa muendelezo wa mikakati kutoka awamu moja kwenda awamu nyingine.
Kwa mfano nikitolea mfano katika sekta ya Elimu na Sekta ya Afya awamu mbili zilizopita walijitahidi kuongeza shule na hospitali lakini hazina walimu na madaktari wa kutosha.
Sasa ilitakiwa awamu inayofuatia waendeleze kwa kuwaandaa wataalamu katika hayo majengo yaliyojengwa katika awamu iliyopita lakini badala yake awamu inayofuata hawalioni hilo na wanaanza upya kwa vipaumbele vyao vipya bila kurekebisha makosa ya awamu iliyopita.
Kwa huu utaratibu wa kiutawala itatuchukua miaka 100 kukaribia tunapopataka.
Point nyingine ya kuongezea bado elimu yetu haijakidhi viwango vya kufanya ushindani katika soko la kimataifa.
Mtu aliyeishia form 4 Ghana/Zambia/Kenya/Nigeria ana confidence kubwa ya kujiingiza kwenye soko la ajira la kimataifa mara 10 kumzidi Graduate wa Tanzania.
Hili nimelishuhudia kwa macho yangu baada ya kusafiri kwenye nchi kadhaa.
wasomi wa Tanzania wanawaza wakishamaliza degree wapate kazi Halmashauri wakishapata wamemaliza kazi hakuna challenge mpya tena.
Mawazo mazuri,Dira ni muhimu sana ili kuwa na muendelezo wa shughuli za maendeleo kutoka awamu moja kwenda awamu nyingine, pointi yako ya serikali kujikita zaidi kwenye miundombinu kuliko kuboresha rasilimali watu pia ni ya msingi sana maana tunaweza kuwa na shule nyingi lakini wataalamu kama ni wachache ni sawa na hatujafanya kitu chochote.
 
Exactly,shida ya viongozi wetu wako shallow kwenye future forecasts hao wanaangalia current activities tu.
 
Badala ya kutengeneza mfumo ujiendeshe wenyewe tunatengeneza mtu wa kuendesha kila kitu

Hilo tatizo la kwanza, lakini baya zaidi hapo kwenye mtu kuendesha kila kitu kwa matakwa yake tunapoteza muda na rasirimali. Hatuelewi vipaumbele vyetu hasa ni vipi.

Dira ya mpango wa maendeleo inayotekelezeka ikiwepo hata wahisani wakija au tukipewa mkopo, tunajua kabisa pesa zielekezwe wapi.

Vinginevyo tutajikuta watu wanatupangia kutupa msaada na matumizi wanayotaka wao hata kama kwetu sio jambo tunalihitaji kwa sasa.
Nchi inaendelea kuelemewa na madeni wakati hatupigi hatua inayoendana na pesa tunazopoteza.
 
Back
Top Bottom