Uchaguzi 2020 Umuhimu wa Mawakala wa Wagombea Urais, Ubunge na Udiwani kupatiwa nakala za matokeo ya uchaguzi katika vituo vya kupiga kura

Kwenye hii nchi kuna watu wameamua kuwapeleka wengine namna wanavyo taka wao tu kama vile nchi ni mali yao binafsi.
Yaani ukianzia katiba, sheria, kanuni na utaratibu vyote wamechakachua kwa maslahi yao badala ya nchi.
Nchi nyingi zilizo ingia kwenye mizozo sababu kuu ni kuharibu/kutofuata vitu muhimu kama hivi katika suala zima la kuiongoza nchi.
 
Mtoa mada kuhusu kutolewa kwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ameamua kwa makusudi kupotosha maana halisi ya kifungu cha 79A(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni ya 67(1)(b) ya kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020.

Nakushauri usome Sheria kwa ujumla wake na si kusoma in β€œisolation”. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu cha 79A (1) (e) inasomeka, 79(1) β€œupon conclusion of the counting of the votes in accordance with section 73, the Presiding Officer shall- (e) if available in sufficient number; give each polling agent a copy of the report of results;”
Maana yake ni kwamba Msimamizi wa Kituo (Presiding Officer) β€œata” (shall) atampatia kila wakala nakala ya fomu ya matokeo, β€œif” kama zipo za kutosha. Hii ni sheria mama. kwanini umeruka neno β€œif” makusudi ili apotoshe umma?? pasipo na sababu za msingi za kufanya hivyo??
 
Mapungufu ya uzi huu yako bayana
 

Sheria ndogo (kanuni za Uchaguzi) zimeelez,a kanuni ya 67(1)(b) -β€œ67(1) The Returning Officer shall after the addition of votes for Presidential election- (b) issue to every candidate or his agent a copy of Form No. 24A.

Kanuni inamtaka Msimamizi wa Uchaguzi kumpatia mgombea au wakala wake nakala ya fomu ya matokeo.
Mtoa mada anapotosha kwa makusudi. Hii inaonesha mambo mawili-
(i) Hana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu Sheria za Uchaguzi na kanuni zake; au
(ii) Hana nia njema na mchakato wa uchaguzi.

Namshauri akasome upya kifungu cha 79(A)(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kanuni ya 67(1)(b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, kwa utulivu ili aelewe.
Kwa taaluma yake ya kama sheria, naamini mtoa mada ameenda kwa mwendokasi kuzidi lengo la Sheria na kanuni husika.
 
Mapungufu ya uzi huu yako bayana

Pia Sheria ndogo (kanuni za Uchaguzi) zimeelez,a kanuni ya 67(1)(b) -β€œ67(1) The Returning Officer shall after the addition of votes for Presidential election- (b) issue to every candidate or his agent a copy of Form No. 24A.

Kanuni inamtaka Msimamizi wa Uchaguzi kumpatia mgombea au wakala wake nakala ya fomu ya matokeo.
Mtoa mada anapotosha kwa makusudi. Hii inaonesha mambo mawili-
(i) Hana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu Sheria za Uchaguzi na kanuni zake; au
(ii) Hana nia njema na mchakato wa uchaguzi.

Namshauri akasome upya kifungu cha 79(A)(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kanuni ya 67(1)(b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, kwa utulivu ili aelewe.
Kwa taaluma yake ya kama sheria, naamini mtoa mada ameenda kwa mwendokasi kuzidi lengo la Sheria na kanuni husika.
 

Huu utopolo ulioandika ni ushahidi wa wazi kwa Mwanasheria yoyote anayejua kwa kina sheria uchaguzi kujua kwa haraka sana kuwa uelewa wako kuhusu maswala ya sheria za Uchaguzi ni mdogo sana.

Kwa sasa niko busy lakini baadae nitakujibu mpaka wewe mwenye utajiona mjinga sana wa swala hili.
 


Wewe ndo hauna ufahamu ndo maana umeshindwa kutofautisha kati ya Returning Officer na Presiding Officer, hivi ni vyeo viwili tofauti kabisa kwenye sheria.

Baade nikipata muda nitakujibu nikioneshe jinsi ulivyo mjinga wa sheria za Uchaguzi.
 
Kenge kabisa wewe. Ulamwambia mtu uelewa wake ni mdogo. Halafu huna JUSTIFICATION za kukosoa hoja zake?
Bure kabisa Wewe!!
 

Nimesoma makala yote mwanzo mwisho....

Asante sana kwa elimu murua kuhusu sheria na kanuni za uchahuzi mkuu huu wa 2020...

SWALI KUBWA LA KUJIULIZA NI HILI....

Kwamba, iweje NEC watunge kanuni inayopingana na sheria kuhusu mgombea Udiwani ama Ubunge ama Urais yeye mwenyewe ama kupitia wakala wake kuanzia ngazi ya kituo cha kupigia na kuhesabia kura wawe na "uhiari" badala ya "ulazima" kumpatia kila mgombea yeye mwenyewe ama wakala wake nakala ya matokeo ya kura??

Lengo la TUME lilikuwa ni nini hasa? Je, siyo kwamba wanatengeneza chanzo cha vurugu kwa makusudi kabisa?

Ni matumaini yangu kuwa hawataendelea na mchezo wao huu hatari kwa sababu hakuna maana wala sababu yoyote kuhatarisha AMANI ya nchi hii kwa sababu ya fomu za matokeo ya kura kwenye vituo...!

Na kwa upande mwingine ni kuwa, kumbe ni wazi kabisa kuwa, kwa NEC kufanya mambo kinyume cha sheria, huwa ni jitihada za makusudi kabisa kutaka kumsaidia mgombea fulani kushinda uchaguzi kwa kuchakachua matokeo ya kura halali kwa kila mgombea....!

Hili halikubaliki....
 
Kenge kabisa wewe. Ulamwambia mtu uelewa wake ni mdogo. Halafu huna JUSTIFICATION za kukosoa hoja zake?
Bure kabisa Wewe!!

Wewe unafikiri Kenge ni nani hapa kama siyo wewe maana hata wewe huna "justification" ya unachokikosoa....!!

Na kingine kukuhusu wewe ni hiki;

"Anayejua" au mtu mwenye "ufahamu" wa jambo fulani na kutaka kushea na wengine huwa hatumii lugha ya matusi na isiyo ya kistaarabu kutaka kurekebisha ama kukosoa hoja ya mtu mwingine kama vile mlevi wa bar za pombe za kienyeji hususanj chang'aa au gongo...!

Hivi ndivyo ulivyo wewe. Wewe ni mlevi wa vilabu vya pombe ya chang'aa tu, huna lolote unalolijua. Ushahidi ni maandishi yako...!!

Ndo kusema, lugha yako na uandishi wako tu ni "justification" tosha kuwa huna ulijualo zaidi ya "mapenzi kipofu" uliyonayo juu mambo haya....!!

Pole na usiku mwema...
 
ni kweli wote tunajua hilo, ila bila kusisitiza hili, uhuni ni lazima utafanyika vituoni. Mkuu CCM hii unafikiri inaogopa sheria? angalia tu namna wagombea walivyoenguliwa kuhuni huni wakati sheria zipo wazi kabisa.
Dah! Uko vizuri bro. Umemwaga nondo za kutosha.
 

Mheshimiwa, hawa ni walewale wakati mwingine ni wa kuwapuuza tu maana wanakuwa hawana nia ya kuelewa ama kujifunza..

Makala yako inafumbua ufahamu watu wengi sana...

Hili CCM na Allies wao (kama huyu hapo chini πŸ‘‡ πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡huyo hapo chini uliyemkwoti), hawataki watu watambue na kuujua ukweli huu ambao ndio moja ya mbinu ya NEC katika chaguzi zote zilizopita ya kuchakachulia matokeo ya kura za uchaguzi kwa kumpa ushindi mgombea ambaye hakushinda wala kustahili kuwa mshindi...

Kwao watu wakijua udhaifu huu wa NEC, aliyewafanya wajue ni MCHOCHEZI...!!

Fikra za namna hii ni za kijinga na za kipumbavu sana tena ule upumbavu uliovuka mipaka ya ustaarabu wa binadamu. Huyu hapa πŸ‘‡ πŸ‘‡msomeni..
Elimu iliyoambatana na uchochezi wa chuki dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sawa rudi kwa huyo aliyekutuma mwambie umeshafanya kazi uliyotumwa.
 
Asante sana mkuu Kitaturu.
 
Kenge kabisa wewe. Ulamwambia mtu uelewa wake ni mdogo. Halafu huna JUSTIFICATION za kukosoa hoja zake?
Bure kabisa Wewe!!

Kuitetea CCM yataka ujasiri na kujitoa akili...
Sasa hayo matusi Ni ya nn? Ukishindwa kujibu hoja kaa kimya.
 
NEC ya CCM inasema si LAZIMA wakala kumpatia nakala....anaweza kupatiwa tu kama nakala zitatosha!!

Mmeona janja hiyo ....hapo kuna gepu la wizi... kwamba hata ujumlishaji wa kichama wa kura hauwezi kufanyika.
Kifupi sana wanajambo lao
 
Mbona hukubali kufundishwa?... Yaani wewe ndio mjuzi na mtaalamu wa kila kitu ama sivyo?

Mimi ninakubali kufundishwa na kuelimishwa tena kwa roho safi, hatahivyo, siwezi kufundishwa na professionally incompetent person anayefanya makosa ya kisheria ambayo yako wazi sana, mtu ambaye hana hata uwezo wa kutofautisha kati ya Returning Officer na Presiding Officer.

Mimi haya mambo ya sheria za Uchaguzi nimeyachimba kwa kina sana, hivyo, mtu ukija kichwa kichwa bila maandalizi ya kina, bila kusoma kwa kina na bila kuelewa kwa mapana, kwa kina na kwa marefu utakwama sana kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…