Nimekuita
mjinga kutokana na kitu ambacho umeandika ambacho kinaonesha kuwa wewe ni
shallow and professionally incompetent person with partial knowledge of election law kwa sababu zifuatazo;
(1)
Kwanza, haujui ulichoandika, umefanya rejea kwa
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambacho kinahusu Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais na Mbunge ambazo ni
Fomu Na. 21 A na
Fomu Na 21 B zinazotolewa na Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura (
Presiding Officer) na kutokana na ujinga wako wa sheria ukafanya rejea kwenye
Kanuni ya 67 (1) (b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 ambayo inahusu au ina deal na Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais pekee ngazi ya Jimbo la Uchaguzi zinazotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi (
Returning Officer) ambayo ni
Fomu Na 24 A, hapa umeandika kuhusu viwili tofauti ambayo hauvijui na badala yake ulipashwa kufanya rejea kwenye
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 ambayo inahusu
Fomu Na. 21 A na
Fomu Na. 21 B.
(2)
Pili, kutokana na maelezo yangu hapo kwenye Na. 1 hapo juu, ni wazi kabisa kuwa haujui tofauti kati ya Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura (Presiding Officer) kwa upande mmoja na Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer) ambaye ni msimamizi mkuu wa uchaguzi ngazi ya Jimbo la Uchaguzi.
(3)
Tatu, Kutokana na maelezo yangu hapo kwenye Na. 1 hapo juu, ni wazi kuwa wewe haujui tofauti ya kati ya
Fomu Na. 21 A na
Fomu Na. 21 B kwa upande mmoja na
Fomu Na. 24 A na
Fomu Na. 24 B kwa upande mwingine.
Nikuelimishe kidogo tu
Fomu Na. 21 A na
Fomu 21 B ni matokeo ya Rais na Mbunge mtawalia (respectively) ngazi ya kituo cha Kupiga Kura ambayo yanatolewa na Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura (Presiding Officer).
Wakati
Fomu Na. 24 A na
Fomu Na. 24 B ni nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais na Mbunge mtawalia (respectively) ngazi ya Jimbo la Uchaguzi ambazo zinatolewa na Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer).
(4)
Nne, maoni yako yanaoneshe wazi kuwa ama umetoa maoni yako bila kusoma makala yangu yote au kama umeisoma yote basi umesoma makala yangu bila kuielewa vizuri na kwa kina na kwa mapana na marefu kwa sababu katika
SEHEMU YA 2 ya makala yangu nimechambua kwa kina
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura 343 sanjari na
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 ambapo nimechambua kwa kina matumuzi ya neno
"SHALL" na matumizi ya neno
"MAY" na implications zake na athari zake kisheria na nimechambua matumizi ya neno
"IF" (iwapo) tena nikapigia mstari (underlining) neno
"IWAPO" (IF) kwenye sentensi.
(5)
Tano, Kwenye andiko lako umeshindwa kwa asilimia 100% kufanya rejea kwenye
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020
Mtu yoyote ambaye anachambua swala la nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura akishindwa kufanya rejea kwenye
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 basi bila shaka yoyote huyo ni kilaza na ni mjinga aliyekubuu wa sheria za Uchaguzi kwa sababu
Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu ndo inahusika na swala haki ya mawakala kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi na discretionary powers za Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura kutoa nakala hizo.
(6)
Sita, Kwenye andiko lako umeshindwa kwa asilimia 100% kufanya rejea kwenye
Aya ya 9 (19) Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020.
Mtu yoyote ambaye anachambua swala la nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura akishindwa kufanya rejea kwenye
Aya ya 9 (19) Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 basi bila shaka yoyote huyo mtu ni kilaza na ni mjinga aliyekubuu wa sheria za Uchaguzi kwa sababu
Aya ya 9 (19) tajwa hapo juu ndo inayotaja idadi ya nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani ambazo zinapashwa kuwepo katika kila kituo cha Kupiga Kura.
Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 inasema katika kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kuwepo na Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani na kila kitabu kitakuwa nakala 24 na kati ya hizo
nakala 24 sheria inaelekeza kwa lazima kuwa
Nakala 21 ni kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea katika Kituo cha Kupiga Kura kwa ajiri ya kuwapatia wagombea Urais na vyama vya siasa na
nakala 3 tu ndo za tume ya uchaguzi ambo nakala moja kati ya 3 ni kwa ajiri kubandikwa ukutani kwenye Kituo cha Kupiga Kura na nakala ya 2 kati ya 3 ni ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kwa ajiri ya kujumlishia kura na nakala ya 3 ni kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ngazi ya taifa . Kitabu cha Nakala za Fomu Matokeo ya Rais kitakuwa nakala 24, na cha mbunge kitakuwa na nakala 24 na cha Diwani kitakuwa na nakala 24.
NGOJA NIKUONESHE ENEO LA KWANZA AMBAPO UJINGA WAKO WA SHERIA MAHALI ULIOPO.
Soma
SEHEMU YA 4 ya makala yangu hapo chini.
😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛
SEHEMU 4: NI LAZIMA MAWAKALA KUPATIWA NAKALA YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS.
Kisheria ni lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Urais nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ambayo ni
Fomu Na. 21 A kwa sababu nne zifuatazo:
🔴 (1) Masharti ya
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 yanaelekeza kwa lazima kwamba
iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya Rais basi ni
"lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Urais nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ya Kituo cha Kupiga Kura.
View attachment 1575992 (2)
Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 inaelekeza kwa
lazima kuwa kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kiwe na Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais chenye
"nakala 24" za fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais (
Fomu Na. 21 A ) na kati ya
nakala 24 tajwa hapo juu,
nakala 21 ni kwa ajiri kuwapatia mawakala wa wagombea Urais ili wazipeleke kwa wagombea Urais na vyama vyao vya siasa ambavyo wanawakilisha katika Kituo cha Kupiga Kura.
🔴 (3) Kwa kuwa kisheria lazima ziwepo
nakala 21 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea Urais ili wazipeleke kwa wagombea Urais na vyama vyao vya siasa basi kutakuwepo na nakala za kutosha kuwapatia
mawakala 15 wa
wagombea Urais 15 ambao wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea nafasi ya Rais katika uchaguzi mkuu wa 2020.
🔴 (4) Kwa kuwa kutakuwepo na
nakala 21 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais ambazo zinatosha kuwapatia
mawakala 15 wa wagombea
Urais 15 basi Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura
lazima wawapatie nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais mawakala wote wa wagombea Urais kama inavyoelekezwa
kwa lazima na masharti ya
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 kwamba iwapo kuna nakala za kutosha
"lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura awapatie wakala wote wa wagombea Urais nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais.
Pia, Kisheria ni lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Ubunge na udiwani nakala ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge na diwani ambayo ni Fomu Na. 21 A na Fomu 21 C mtawalia (respectively) kwa sababu nne ambazo zimetajwa hapo juu kwa kufanya mabadiliko muhimu hapo juu (
mutatis mutandis).
NGOJA NIKUONESHE ENEO LA PILI AMBAPO UJINGA WAKO WA SHERIA MAHALI ULIOPO.
Somo
SEHEMU YA 2 ya makala yangu hapo chini.
😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛
SEHEMU 2: MSIMAMO SAHIHI WA SHERIA.
Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kila wakala wa mgombea Urais na ubunge alikuwa na haki ya kupatiwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais. Sheria
ilimtaka kwa lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ( Presiding Officer ) kumpatia kila wakala wa mgombea Urais na ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge kwa mujibu wa
Kanuni ya 60 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 307 la 2015).
Katika Kanuni za Uchaguzi Rais na Wabunge za mwaka 2015 haki ya wakala wa mgombea Urais na ubunge kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais nambunge
ilikuwa wazi na bayana sana bila utata wowote.
Lakini Katika Kanuni za Uchaguzi Rais na Wabunge za mwaka 2020 haki imepunguzwa makali kwa sababu kupewa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge imefanya kuwa
hisani (privilege) kwa mujibu wa
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 ( Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ambapo Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura
anaweza kumpatia au kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais na ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi iwapo atajisika kufanya hivyo kwa kuwa hashurutishwi na sheria kutoa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020, Msimamizi wa Kituo
"anaweza" kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge
"iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge", hii ni kwa mujibu wa masharti ya
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020).
Kutoka na matumizi ya neno
"anaweza" (
may) katika
Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu, kisheria inamaanisha kuwa Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ana hiyari (discretion) ya
kumpatia au
kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais au ubunge katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge.
Sababu ya hiyari (discretion) hii ya Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura inatokana na matumizi ya neno
"anaweza" (
may) katika sheria kwa msingi kwamba neno hili linapotumika katika sheria limaanisha kuwa mtu ana hiyari kufanya au hiyari ya kukataa kufanya kitu ambacho sheria inasema kifanyike (
discretionary power), hii ni kwa mujibu wa
Kifungu cha 52 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiriwa na Mahakama Kuu katika kesi ya
Laula Edmund Vs Barke Ahmed Said, PC Civil Appeal No. 1 of 2020.
Kwa maneno mengine, ni kwamba kwa mujibu wa
Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu, Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ana mamlaka ya hiyari (
discretionary power) ya kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge hata kama kuna nakala za kutosha za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.
Hatahivyo,
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020
inakinzana na masharti ya
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambacho kinaelekeza
kwa lazima kwa kutumia kitenzi kisaidizi
"ata" (
shall) kuwa iwapo kuna nakala za kutosha lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie wakala wa mgombea Urais au ubunge katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais.
Kwa maneno mengine, ni kwamba kwa mujibu wa
Kifungu cha 79 A (1) (e) tajwa hapo juu, Msimamizi wa Kituo cha kupiga
analazimishwa na sheria bila hiyari yake kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha kupiga kura nakala yafomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais
iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.
Kama kuna nakala za kutosha lazima Msimamizi wa Kituo cha kupiga ampatie wakala wa mgombea Urais au ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa sababu kitenzi kisaidizi
"ata" (
shall) kinapotumika katika sheria kinamaanisha kuwa mtu hana kabisa hiyari bali ni lazima afanye kama alivyoelekezwa na sheria (
mandatory duty), hii ni kwa mujibu wa
Kifungu cha 52 (2) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiriwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya
Shaaban Iddi Jololo and 3 others Vs Republic Criminal Appeal No. 200 of 2006.
Iwapo
Sheria Ndogo Ndogo (subsidiary legislation) iliyotungwa na mamlaka iliyokasimishwa (delegated) mamlaka ya kutunga sheria na bunge
"inakinzana" na
Sheria Kuu (principal legislation) iliyotungwa na bunge lenyewe basi Sheria Ndogo Ndogo inakuwa
batili tangia mwanzo (
null and void ab initio) kwa kiwango ambacho Sheria Ndogo Ndogo inakinzana na Sheria Kuu iliyotungwa na bunge, haya ndo matakwa ya masharti ya
Kifungu cha 36 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiri na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya
Morogoro Hunting Safaris Ltd. Vs Halima Mohamed Mamuya, Civil Appeal No. 117 of 2011 na pia huu msimamo wa sheria uliwekwa na Mahakama zaidi ya miaka 80 iliyopita katika kesi ya
Nanal Damodar Kanji Vs Tanga Township Authority [1940] 1 T.L.R. 239.
Kirai
"Sheria Ndogo Ndogo" (subsidiary legislation) kimetafsiri na
Kifungu cha 4 ya Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1, pamoja na mambo mengine kumaanisha A, Maelekezo,
Kanuni, Notisi na Tamko ambalo limetungwu chini ya mamlaka ya sheria iliyotungwa na bunge au mamlaka nyingine ya kisheria, hivyo, basi, kisheria
Kanuni ni sheria Sheria Ndogo Ndogo.
Tume ya Taifa Uchaguzi imekasimishwa (delegated) na bunge Mamlaka ya kutunga Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge chini ya
Kifungu cha 124 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambazo kisheria ni sheria ndogo ndogo.
Kwa msingi huu basi, iwapo Kanuni za Uchaguzi zilizotungwa na Tume ya Taifa Uchaguzi
zinakinzana na Sheria Kuu ya Uchaguzi iliyotungwa na bunge basi Kanuni za Uchaguzi ambazo zimetungwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
zinakuwa batili tangia mwanzo (
null and void ab initio) kwa kiwango ambacho zinakinzana na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, haya ndo matakwa ya masharti ya
Kifungu cha 36 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1.
Hivyo basi, msimamo sahihi wa sheria
sio ule ambao umeelekezwa kwenye
Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 kwa sababu msimamo wa sheria ambao umeelekezwa na
Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu ni batili tangia mwanzo kwa kukinzana na
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Hivyo basi, msimamo sahihi wa sheria (
correct position of law) ni kama ulivyoelekezwa kwenye masharti ya
Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 kwamba kama kuna nakala za kutosha
"lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie wakala wa mgombea Urais au mbunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.
Swali muhimu hapa ni je kutakuwepo nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge katika Kituo cha Kupiga Kura? Jibu la swali hili linapatikana sehemu inayofuatia hapo chini baada ya sehemu yaani Sehemu ya 3.
NGOJA NIKUONESHE ENEO LA TATU AMBAPO UJINGA WAKO MAHALI ULIOPO.
Soma
SEHEMU YA 3 ya makala yangu hapo chini.
😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛
SEHEMU 3: JE KUTAKUWEPO NA NAKALA ZA KUTOSHA ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KATIKA KITUO CHA KUPIGA KURA?
Jibu ni ndio.
Ndio kisheria lazima kuwepo na nakala za kutosha za matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Kituo cha Kupiga Kura kwa sababu ambazo nitazielezea hapa chini.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kutunga au kutengeneza
Maelekezo ya Uchaguzi (Election Directives) yenye nguvu ya kisheria chini ya
Kifungu cha 126 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 na chini ya
Kanuni ya 79 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitengeneza
Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 ambayo yanataja idadi ya nakala za matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge ambazo zinapashwa kuwepo katika Kituo cha Kupiga Kura.
🟧
A. UTOSHELEVU WA NAKALA ZA FOMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS.
Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 inaelekeza kwa lazima kuwa kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kiwe na
Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais chenye
"nakala 24" za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais (
Fomu 21 A ) ambazo zitagawiwa kama ifuatayo;
(1)
Nakala ya Kwanza ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko
ukrasa wa 1 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais atapewa Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer) ngazi ya jimbo. Nakala ya kwanza ni
nakala halisi (original copy).
(2)
Nakala ya Pili ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko
ukrasa wa 2 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais
itabandikwa ukutani na Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura katika Kituo cha Kupiga Kura husika kwa ajiri ya kuwajulisha wananchi au umma wa Watanzania matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika Kituo husika. Nakala ya Pili
sio nakala halisi bali ni
nakala rudufu (photocopy) ambayo inarudufiwa kutoka katika nakala halisi yaani nakala ya kwanza.
(3)
Nakala ya Kumi na Tatu (13) ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko
ukrasa wa 13 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais itapewa Tume Taifa ya Uchaguzi kwa ajiri ya matumizi yake ya kiofisi. Nakala ya 13 nayo ni
nakala halisi (original copy).
(4) Kuanzia
Nakala ya 3 na kuendelea (consecutively) mpaka
Nakala ya 24 katika Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambazo ziko kuanzia
ukrasa wa 3 na kuendelea mpaka
ukrasa wa 24 wa Kitabu tajwa hapo juu watapewa mawakala wa wagombea Urais kulingana na idadi yao
isipokuwa Nakala ya 13 ambayo itakuwa Nakala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa kuwa kuna
wagombea Urais 15, hivyo, basi mawakala wa wagombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura watapewa kuanzia
nakala ya 3 mpaka ya
nakala 18 isipokuwa nakala ya 13 ambayo itapewa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Pia, isipokuwa nakala ya 13, kuanzia Nakala ya 2 na kuendelea mpaka nakala ya 24 ni nakala zilizorudufiwa (photocopies) kutoka katika nakala halisi yaani nakala ya 1 na 13 na sio nakala halisi (original copy).
Nakala ya 3 kati ya nakala 24 ni kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maana ya Nakala ya 1, 2 na 13.
Fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais katika kituoni cha Kupiga Kura ambayo ni
Fomu Na. 21 A iko kwenye umbo la kitabu ambacho kitakuwa na kurasa
ishirini na nne (24) ambapo
nakala 12 za awali zimetenganishwa na
nakala 12 za mwisho kwa karatasi ngumu (
separator). Nakala 12 za mwisho zinaanzia ukrasa wa 13 mpaka ukrusa wa 24 yaani ni kuanzia nakala ya 13 na kuendelea mpaka nakala ya 24.
Karatasi za
Fomu Na. 21 A zimetayarishwa katika namna ambayo inawezesha kuandika na kutoa nakala rudufu (photocopies) bila kuweka
karatasi ya kaboni (Carbon Papers) yaani ni
"Self copying".
Hivyo basi, kila kituo cha kupiga kura kinatakiwa kuwa na nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais (
Form 21 A ) zisizopungua
Nakala 24 , basi kwa kuwa wagombea Urais ni
watu 15 ambao watapewa
nakala 15 za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapewa
nakala 3 za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais, hivyo, zitabaki
nakala 6 za fomu za matokea ya uchaguzi wa Rais za ziada ambazo hazitatumika.
Kutokana na uchambuzi wa hapo juu basi kisheria lazima zitakuwepo
nakala 24 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Kituo cha Kupiga Kura ambazo zinatosha kuwapatia mawakala wote 15 wa wagombea Urais 15 wote.
🟧
B. UTOSHELEVU WA NAKALA ZA FOMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MBUNGE NA DIWANI.
🔹
(a) Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge.
Utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa Rais kwa mawakala wa wagombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura unafanana karibu kwa kila kitu na utaratibu na masharti yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa wabunge kwa mawakala wa wagombea ubunge na sheria inayotumika ni moja.
Hivyo basi, kutakuwepo na nakala 24 za fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa mbunge kwenye kila Kituo cha Kupiga Kura. Kati ya nakala 24 za Matokeo ya Uchaguzi wa mbunge, nakala 21 zitakuwa kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea ubunge katika Jimbo la Uchaguzi husika. Na nakala 3 zitakuwa kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mojawapo ya nakala kati ya nakala 3 tajwa hapo juu itakuwemo nakala moja (1) ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge kwa ajiri ya kubandika katika ukuta wa Kituo cha Kupiga Kura kuutaarifu umma wa Watanzania na wapiga kura matokeo ya Uchaguzi wa mbunge katika Kituo husika.
Hatahivyo, nakala za matokeo ya uchaguzi wa mbunge katika Kituo cha Kupiga Kura zitakuwa kwenye
Fomu Na. 21 B.
🔹
(b) Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Diwani.
Kwenye uchaguzi wa diwani sheria zinazotumika katika mchakato wa kutoa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kituo cha Kupiga Kura kwa upande moja ni tofauti na sheria zinazotumika kwenye Uchaguzi Rais na mbunge kwa upande mwingine isipokuwa
Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 ambayo yatumika katika uchaguzi wa madiwani pamoja na Uchaguzi wa Rais na wabunge.
Sheria zinazotumika kwa upande wa uchaguzi wa udiwani katika kutoka nakala za matokeo ya uchaguzi wa diwani ni hizi zifuatazo;
(i) Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292
(ii) Kanuni ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020
(iii) Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020.
Hatahivyo, pamoja na utofauti wa sheria bado utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa diwani kwa mawakala katika Kituo cha Kupiga Kura kwa upande mmoja unafanana karibu kwa kila kitu na utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika kwa wagombea wa nafasi ya Rais na nafasi ya mbunge kwa upande mwingine.
Isipokuwa nakala za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kituo cha Kupiga Kura yanakuwa kwenye
Fomu 21 C.