Umuhimu wa mawakili wa shetani kwenye makongamano ya siku ya Nyerere.

Umuhimu wa mawakili wa shetani kwenye makongamano ya siku ya Nyerere.

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Zamani kanisa katoliki kama linataka kumfanya mtu kuwa mtakatifu lilikuwa linaajiri mtu fulani wa kuitwa Advocate Dei(wakili wa shetani). Kazi yake ilikuwa ni kuchambua mabaya ya mtu huyo na kujenga hoja kuwa hafai kuwa mtakatifu.

Kwahiyo, huyu mtu anayepewa utakatifu alikuwa ni bora sana, lakini ilionekana kuna umuhimu mkubwa wa kuangalia upande wake wa pili. Sasa basi, Nyerere alikuwa ni moja ya viongozi bora kuwahi kutokea. Lakini ni muhimu sana kujua upande wake wa pili. Kuna mengi ya kujifunza kutokana na makosa ya mtu, pengine hata kuliko mazuri yake.

Ni vyema haya makongamano ya Nyerere yaalike na watu wa upande wa pili ili tupate kumfahamu zaidi.

Tuanze hapa kwenye huu uzi. Tujadili makosa ya Nyerere, pengine tunaweza kujifunza zaidi.
 
1. Aliingia vita vya kagera kichwa kichwa
2. hakupenda kukosolewa ndio maana alifuta vyama vya upinzani




Bongo Hapo Zamani:

- Miaka 22 Ya Kifo Cha Mwalimu:

Kisa Cha Nyerere Alipomshikisha Adabu Giriki Aliyetamba Kuitia Serikali Mfukoni..!

Ndugu zangu,

Julius Nyerere alikuwa kiongozi wa kanuni. Alikuwa na misimamo na hakupenda mambo ya hovyo hovyo.

Kuna kisa cha mfanyabiashara raia wa Kigiriki aliyepita akitamba kuwa Serikali yote ameiweka mfukoni. Aliitwa George Paparus. Ni kwa kuwahonga watendaji wa Serikali.

Jambo hilo lilimkera sana Nyerere, kwamba mtu huyo anadai Serikali yote kaiweka mfukoni. Ni dharau kubwa sana kwa Jamhuri na Rais mwenyewe. Julius Nyerere akaamuru Giriki huyo aswekwe ndani.

Mzee Jommo Kenyatta alijaribu kumwomba Nyerere amwachie bepari yule. Nyerere alikataa.

Ni pale tu Baba Askofu Makarios alipomtumia mjumbe maalum. Mjumbe huyo aende kwa Julius Nyerere na kumwomba radhi Nyerere kwa kilichofanywa na Giriki huyo.

Ndipo Nyerere akaamuru atolewe ndani. Kwa sharti moja, kuwa asikanyage tena kwenye ardhi ya Tanzania na Afrika Mashariki.

Naam, Julius Nyerere alikuwa kiongozi wa kanuni na hakuwa na mzaha na wenye kudhani fedha zao zingewapa jeuri ya kuichezea Jamhuri.

credit to Maggid Mjengwa.. Mwenyekiti wa wenyeviti
 
Muulize malikia elizabeth alivyo pewa kifimbo na baba wa taifa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom