SoC01 Umuhimu wa mazoezi na faida zake kwa watoto wenye changamoto ya ulemavu wa akili

SoC01 Umuhimu wa mazoezi na faida zake kwa watoto wenye changamoto ya ulemavu wa akili

Stories of Change - 2021 Competition

JOSIA PATRICK

New Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
4
Reaction score
2
Ulemavu wa akili: Ni ile hali ya mtu kushindwa kutumia viungo vyake sawasawa na kushindwa kutumia akili yake sawasawa kutokana na athari ya ubongo wake.Sababu za ulemavu zinaweza kutokea katika nyakati kuu tatu ambazo ni.
(a)Kabla ya Kuzaliwa.
(b) Wakati wa kuzaliwa.
(c) Baada ya kuzaliwa.

(A) KABLA YA KUZALIWA:Kabla ya kuzaliwa ni ule wakati mtoto ametungwa na kuwa mimba na anadumu kwenye tumbo la mama yake mpaka atimize umri wa kuzaliwa ambao ni miezi tisa.Sababu izo ni kama zifuatazo,Kurithi,Lishe Duni,Ajali,Ulevi,Madawa,Magonjwa.

(B)WAKATI WA KUZALIWA:Hii inatokea pale ambapo mama amefikisha miezi tisa na ni wakati kujifungua.Sababu hizi ni kama ifuatavyo,Uchungu wa muda mrefu,Kuzaliwa kabla ya muda,Ajali,Kutanguliza damu wakati wa kujifungua.

(C) BAADA YA KUZALIWA:Mtoto anapozaliwa anatakiwa kulia au kwa maana nyingine ni lazima alie kwa nguvu ili kuruhusu hewa ya oxygen kuingia kwenye mapafu hivyo kuzunguka mwili kupitia mishipa ya damu hadi kwenye ubongo.

UMUHIMU WA MAZOEZI
Kwanini Tunasema ni muhimu kwa mtoto mwenye changamoto ya ulemavu kufanyiwa mazoezi kwa sababu kwanza kabisa tunatambua kwamba mtoto akishakuwa na ulemavu ni vyema apate haki yake ya msingi ambayo ni mazoezi kwa sababu tunaamini kwamba mtoto akishakuwa na ulemavu wa akili tiba ambayo itakuwa imebaki kwake ni mazoezi na sio.Kitu kingine ambapo anatakiwa kwenda kwa wataalamu wa physiotherapty kwa ajili ya kupatiwa mazoezi hayo.Jamii nyingi sana zimekuwa na mtazamo ambao ni tofauti kulingana na hali ambayo wanapita watoto hawa ambao inapelekea wazazi had walezi kukata tamaa na kuanza kuwa na mawazo ambayo sio mazuri na ambayo hayapendezi.Na mtoto hupatiwa mazoezi kulingana na tatizo lake alilokuwa nalo sio kila changamoto ambayo anayo mtoto huyu basi ndo apewe mazoezi ya mtoto mwimgine .Kila mtoto hupangiwa kitu cha kufanya kulingana na changamoto yake ambayo anayo hivyo ni vyema kwa wazazi kuanza kuamka sasa baada ya kutambua changamoto ambayo anapitia mtoto wake.

IMANI POTOFU
Kumekuwa na imani potofu kwa baadhi ya wazazi kwamba baada ya mtoto kupata hitilafu wengi wamekuwa wakikimbilia kwa waganga kwa kuamini kwamba wanaweza wakafanyiwa kitu na kupata maendeleo kwa watoto wao jambo ambalo limekuwa halina ukweli wowote ule.Sote tunaamini kwamba mtu akishapata ulemavu wa akili kwamba tib a yake iliyobaki ni mazoezi na elimu maalumu kulingana na hali ambayo anaipitia mtoto .Kulingana na hali ya wazazi kukata tamaa hupelekea wazazi pamoja na walezi kwenda kwa waganga kulingana na kukata kwao tamaaa ni vyema kwa wao sasa kuamka na kujua kwamba wanaweza wakapata msaada kupitia mazoezi kwa ajili ya kuwafanyia watoto wao .

JAMII:
Kulingana na jamii zetu kuwa na mtazamo tofauti kuhusu suala la ulemavu ni vyema sasa kwa wao kuanza kubadilika na kuanza kuelemisha wao kwa wao kuhusu suala hili kwan tunaamini kwamba katika jamii zetu wako watu ambao wanaweza sana kubadilisha watu kutokana na ushawishi ambao wanao katika maeneo yao wanayoishi.Hivyo basi kwa wazazi pamoja na walezi ambao wamahudumia watoto hawa ni vyema sasa kwa wao kuachana na imani potofu na kuanza kuwafanyia watoto wao mazoezi baada ya kujua kwamba wana changamoto ya ulemavu wa akili.Ni muda sasa wa sisi jamii kuacha kuwatenga walemavu katika jamiii zetu na kuanza kuwapa haki zao za msingi.

ASANTE NAPENDA KUWASILISHA.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom