Umuhimu wa Shirika Kuwa na Ufadhili Kutoka kwa Mtu Mmoja Mmoja (Individual Donor)

Umuhimu wa Shirika Kuwa na Ufadhili Kutoka kwa Mtu Mmoja Mmoja (Individual Donor)

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60
1727262083349.png

Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yaani, “Non-Governmnetal Organizations” yanapokea ruzuku kutoka kwenye vyanzo vikuu vitatu, ambavyo ni; 1) Taasisi za ufadhili yaani “funding organizations/foundations” 2) Makampuni ya kibiashara yaani “corporations” na 3) Mtu mmoja mmoja yaani “individual Donors”. Kitaalamu; ufadhili unaotoka kwa mtu mmoja mmoja hujulikana kama “Individual Giving”

Takwimu zinaonyesha kwamba ufadhili kutoka kwa mtu mmoja mmoja kwenda kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ndio chanzo kikubwa cha ufadhili ukilinganisha na ufadhili unaotoka kwenye Taasisi za Ufadhili na Makampuni ya kibiashara. Kwa mujibu wa Giving USA, kwa mwaka 2019 tu, ufadhili wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 309.66 sawa na asilimia 69 kati ya bilioni 449.64 ulioenda kwa Mashirika yasiyo ya kiserikali ulitokana na ufadhili wa mtu mmoja mmoja yaani “Individual Giving”. Kwa takwimu hizi unaona ni kwakiasi gani ufadhili kutoka kwa mtu mmoja mmoja ni mkubwa ukilinganisha na ule unaotoka kwenye Taasisi za ufadhili na makampuni ya kibiashara.

Mfadhili Mmoja Mmoja au “Indivividual Donor” ni nani ?
Huyu ni mtu anaelichangia shirika kiasi kidogo cha fedha kwa muda mrefu. Anaweza akawa anachangia kila mwezi au kila mwaka kiasi ambacho wamekubaliano na Taasisi husika kulingana na uwezo wake. Baadhi ya mashirika yana utaratibu wa kuwaweka hawa wafadhili kwa makundi, mfano wa makundi hayo ni;​
  • Kundi la Chini hawa wanachangia kiasi kidogo kwa shirika mfano; Tsh 5,000 mpaka Tsh 20,000 kila mwezi au Tsh 100,000 mpaka Tsh 150,000 kila mwaka.​
  • Kundi la Kati hawa wanachangia kiasi cha juu zaidi ukilinganisha na uchangiaji wa kundi la chini.​
  • Kundi la Juu hawa wanachangia kiasi cha juu zaidi ukilinganisha na uchangiaji wa kundi la kati.​
Hakuna kiasi maalum ambacho kinatumika kama kipimo kuonyesha hiki ni kiasi kwa kundi la chini au kwa kundi la kati na la juu. Mashirika yanatofautiana, Tsh 100,000 kwa shirika moja inaweza ikawa ni kiasi kwa kundi la chini, na kiasi hicho hicho kwa shirika lingine ikawa ni kiasi kwa kundi la juu.

Kwanini ni muhimu kwa shirika kuwa na msingi mkubwa wa ufadhili wa mtu mmoja mmoja (Individual Giving)
  • Mashirika yasiyo ya kiserikali japo hayatengenezi faida, ila yana mahitaji muhimu kwa ajili ya shughuli za uendeshaji, kama vile ulipaji wa mishahara, ulipaji wa kodi, kufanya utafiti, mawasiliano n.k. Ufadhili unaotoka kwa Taasisi za ufadhili au makampuni ya kibiashara, unatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi maalum na si vinginevyo, hivyo inakuwa ngumu kwa shirika kujihudumia kwenye mahitaji ya uendeshaji wa ofisi. Ufadhili kutoka kwa mtu mmoja mmoja hauna uhusiano na mradi fulani, ila unahusiana na shuighuli za shirika kiujumla, hivyo shirika linakuwa na uhuru wa kutumia fedha hizi kwa mahitaji mengine muhimu ya ofisi.
  • Shirika linapokuwa na msingi mkubwa wa ufadhili wa mtu mmoja mmoja, ni rahisi kupata wafadhili wachache miongoni mwao ambao watatoa ufadhili wa juu kabisa kama vile wakfu n.k
  • Kuwa na msingi mkubwa wa ufadhili wa mtu mmoja mmoja unaliwezesha shirika kukabiliana na ushindani mkubwa wa ufadhili kutoka kwenye Taasisi za ufadhili.
Shirika lifanye nini ili kuvutia mfadhili mmoja mmoja (Individual Donor)
Shirika linapaswa kuwa na mpango maalum ambao unajumuisha ufadhili wa mtu mmoja mmoja yaani “Annual fundraising Plan”. Ili kuhakikisha mpango huu unafanikiwa, shirika linapaswa kuzingatia yafuatayo;
  • Kujenga mahusiano ya muda mrefu na mfadhili. Mahusiano haya yatajengwa kwa kuweka wazi fursa ambazo mfadhili atazipata kwa shirika. Pia shirika linapaswa kuchagua njia ya mawasiliano ambayo itapendekezwa na mfadhili husika.
  • Kutoa shukrani za mara kwa mara kwa mfadhili pindi anapotoa mchango wake. Kama kuna uwezekano mualike mfadhili kwenye matukio muhimu ya shirika ili apate nafasi ya kujionea namna ambavyo shirika linafanya shughuli zake.
  • Kutumia teknolojia. Shirika linapaswa kutumia fursa ya mitandao ya kijamii ili kumjulisha mfadhili namna ambavyo mchango wake unaleta mabadiliko kwa jamii na kwa ajili ya kufanya mawasiliano/kupokea maoni na mawazo ya wafadhili kuhusiana na shughuli za shirika. Tovuti ya shirika inapaswa iwe na muundo mzuri ambao utamuwezesha mfadhili kufanya uchangiaji kwa urahisi.

Article By
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Back
Top Bottom