UN kuhamishia makao makuu ya UNICEF, UNFPA na UN Women jijini Nairobi, Tanzania tuko wapi?

UN kuhamishia makao makuu ya UNICEF, UNFPA na UN Women jijini Nairobi, Tanzania tuko wapi?

Bora hawajaleta hata ofc moja hapa bongo, kipindi hiki cha propaganda za kuupiga mwingi mbona tungekoma!
 
Wamefanya vyema.

Ningeshangaa Sana endapo kama wangepanga kuhamishia Makao Makuu ya Taasisi hizo nchini Tanzania.

Licha ya mapungufu yao madogo madogo waliyonayo, bado Kenya ni nchi ya Kidemokrasia na yenye Katiba Bora ukilinganisha na nchi nyingi sana za kiAfrika na duniani kote kwa ujumla.


Hawawezi kuhamishia Tanzania, wanaogopa maafisa wao ama kutekwa ama kuuawa na watawala. Kunaweza kutokea matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu, kama ilivyo kawaida kwa Tanzania, afisa wa UN, akakemea, unadhani watawala watamwacha?
 
Wasiojulikana Wasijekuwavizia Na Kuwapiga Nyundo Visogo Kama Padre Kitine Wakatoliki.
Tumalizane Sisi Kwa Sisi Tu Sio Watu Wa Ng'ambo.
sio sababu kwasababu vifo vya foreigners kenya vimetokea ving recently compared to Tz. Juzi tu yule muandishi habari wa Pakistan aliuliwa kenya. Sababu zinaweza zikawa uendeleaji wa kimiundombinu wa jiji la Nairobi, Itikadi ya kibepari, agglomeration effects whereby there are many other multinational offices in Nairobi, presence ya military base ya USA and others. Kwa tz, ofisi za multinational zipo chache kwamfano kuna ya UNDP pia kuna UN house pale PSSF tower etc
 
Tuko bize kupambana na Lisu
Kenya kwenye position ya jukwaa la kimataifa wametuzidi kidogo hilo tukubali.

Kwa mfano wapo maprofesa wa Kenya hapa Marekani na wafundisha vyuo vikuu hapa.

Yupo profesa Eric Otenyo afundisha sayansi ya jamii chuo kikuu cha Arizona, yupo profesa David Kimori ambae afundisha chuo kikuu cha Mankato katika jiji la Minesota, na yupo profesa mwingine kama Ruben Marwanga ambae ni mratibu wa Diaspora yote kwa wakenya kama sikosei.

Isitoshe, wakenya wana kanisa kubwa kabisa walolijenga kwa fedha zao linonifanya nishangae meli kuelea liko kwenye mji wa Massachusetts laitwa ACK mtakatifu Stephen.

Na pia wapo wakenya wengine wengi tu wenye kuweza kukupa connection ukapiga hatua mbele.

Kwenye hili nipo 100% uhakika ila sijaona watanzania huku nje tukiwa na level hizo.

Mimi naipenda nchi yangu Tanzania ila kinoendela kwa sasa chakatisha tamaa.
 
Ukiona watz wengi tunafurahia hii habari basi ujue tumeishaichoka hii nchi
 
Nairobi Kenya kuna Balozi nyingi sana za nchi za nje ukilinganisha na Tz. Nairobi ni kama HUB ya Kidiplomasia ya Kimataifa katika nchi za Ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita tulilazimika kusafiri hadi Nairobi kwa ajili ya kupata huduma ya Viza za kuzuru kwenye Mataifa fulani fulani ya Ulaya na Amerika ya Kusini kama vile Hungary, Latvia, Austria, Australia, New Zealand, n.k.
Lakini nimesikia pia Uingereza visa zinatoka Nai kwahiyo hapa ni kama ubalozi mdogo tu pia nchi za Scandnavia nazo zilikuwa kwenye mchakato wa kufunga balozi zao hapa kuhamia Nai sijui watu wa mambo ya nje wanachukuliaje hili maana kidiplomasia sidhani kama ni sawa.​
 
Sisi tunapiga siasa zisizoeleweka haki na kuonekana imetendeka sio kipaumbele cha watawala hawajali hilo kwao chama na maslahi yao wachache halafu nchi inafata. Kwa mwendo huo huwezi ukaona mashirika ya kimataifa yakaweka makao makuu yao makuu. Uongo uongo uliokubuhu kwa viongozi wengi nayo inaweza kuwa sababu nyingine maneno lukuki vitendo/utekelezaji hakuna​
Kwani duniani kuna miji mitatu tu ya dar es salaam,new York na Nairobi!?..mbona hamuulizi kigali au kampala vipi?
 
Figisu za kibongo mara vikao sijui vinafanyila baada ya miezi 6 pale BOT upumbavu mtupu hata ungekuwa wewe jirani anakwambia njoo upewe huduma za haraka unasepa tu​
Siku hizi hata ukiwa na "business plan" yakupasa kuilinda kwelikweli kama hujulikani (HUNA CONNECTION) waweza kuporwa na kupotezwa kisha mtu akaitumia.
 
Hahaha hohoho nyie bado mnaomba visa kuingia marekani hahaha kwikwi. Wakati mimi naingia at will tena na private jet gulfstream 900 na kupokelewa na limo hahaha hahaha kwikwi umaskini bana 😆😆😆😆😆😆😆
min -me mshamba_hachekwi
Waingia at will wapi?

Wadhani Marekani ya sasa chini ya Donald Trump waingia tu kama waenda Magomeni Mapipa kumsalimia Sheikh Kundecha?

Baki hapohapo Magomeni mkuu.

Jokes😉
 
Tunahitaji kutenga eneo Dodoma kwenye mji wa kiserikali hili eneo liitwe international street, tujenge maofisi na mashirika yapewe nafasi kwa discounted rates, eneo hili liwe na ofisi na makazi. sasa hivi dar unakuta nyumba anaishi balozi jirani yake kuna danguro linaitwa lounge, usiku kucha wanapiga mziki na kusaula hovyo, na hizi spika za ahuja ndo usiseme ukiwa ndani utadhani nje kuna shetani anafanya tafrija.
 
Waingia at will wapi?

Wadhani Marekani ya sasa chini ya Donald Trump waingia tu kama waenda Magomeni Mapipa kumsalimia Sheikh Kundecha?

Baki hapohapo Magomeni mkuu.

Jokes😉
Hahaha ila Trump kabana hadi wenye green card hawako Salama. Unaambiwa wenye green card wanaogopa hata kusafiri nje ya marekani. Immigration lawyers wanawashauri green card holder wasisafir nje marekani hadi hali itulie.

Trump Ana deport hadi raia wa ulaya.

Jamaa kaona kutumia illegal immigrants card kujipatia umaarufu kwasababu uchumi kashindwa.
 
Back
Top Bottom