Safi sana KenyaView attachment 3422979
Umoja wa Mataifa unatarajia kuhamishia ofisi zake za kimataifa za UNICEF, UNFPA na UN Women jijini Nairobi kufikia mwaka 2026, hatua itakayoiweka mji mkuu wa Kenya katika hadhi sawa na New York, Geneva, na Vienna kama miongoni mwa miji minne pekee duniani inayohifadhi makao makuu ya mashirika mengi ya UN.
Tayari Nairobi inahifadhi mashirika 23 ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo mashirika makuu kama UNEP na UN-Habitat.
Pia kuna mipango ya Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) kuhamishia shughuli zake Afrika, jambo litakaloongeza zaidi nafasi ya bara hilo katika majukumu ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu.
Hatua hii ni sehemu ya ajenda ya mageuzi ya UN iitwayo “UN@80”, ambapo Katibu Mkuu António Guterres ametaja ufanisi wa gharama kama sababu kuu ya mabadiliko hayo.
Gharama za uendeshaji katika miji kama New York na Geneva – kutoka kwa nafasi za ofisi hadi wafanyakazi na vifaa – ni kubwa zaidi ikilinganishwa na Nairobi.
Zaidi ya gharama, uhamisho huu pia unaonekana kama mkakati wa kuelekeza nguvu zaidi barani Afrika, ambalo linahusika na zaidi ya asilimia 60 ya shughuli za kibinadamu za Umoja wa Mataifa.
Mabadiliko haya yanachukuliwa kama ishara kubwa ya kuaminiwa kwa Nairobi kama kitovu cha kidiplomasia duniani.
=======================
Nairobi joins New York, Geneva and Vienna as only cities globally hosting multiple UN headquarters
The United Nations is set to relocate theglobal offices of UNICEF, UNFPA, and UN Women to Nairobi by 2026, elevating the Kenyan capital to the ranks of New York, Geneva, and Vienna as one of only four cities globally hosting multiple UN headquarters.
Nairobi already hosts 23 UN agencies, including flagship bodies like UNEP and UN-Habitat.There are also plans for the Office for the Coordination of Humanitarian Affairs (OCHA) to move its operations to Africa, further strengthening the region's role in global humanitarian response.
The move is part of the UN's wider "UN@80" reform agenda, with Secretary-General António Guterres citing cost efficiency as a key driver.(AD)Operating costs in New York and Geneva, from office space to staffing and logistics, are significantly higher compared to Nairobi.Beyond cost, the relocation is also seen as a strategic realignment toward Africa, which accounts for over 60% of the UN's humanitarian work.This shift is being viewed as a major vote of confidence in Nairobi as a global diplomatic hub.
Source: Developmentaid
Dawa yake hiyo ni ndogo sana, kama weye ni mgeni Marekani na Ulaya kitu cha kwanza pigania kitabu chao ndo salama yako kwenye masuala mengi, ukaazi, ajira na elimu.Hahaha ila Trump kabana hadi wenye green card hawako Salama. Unaambiwa wenye green card wanaogopa hata kusafiri nje ya marekani. Immigration lawyers wanawashauri green card holder wasisafir nje marekani hadi hali itulie.
Trump Ana deport hadi raia wa ulaya.
Jamaa kaona kutumia illegal immigrants card kujipatia umaarufu kwasababu uchumi kashindwa.
Ndio ajabu kwamba majirani hadi Burundi wana internet ya Starlink halafu wadanganyika wao wanasema ili wawaruhusu lazima wajenge ofisi Dar es Salaam.Figisu za kibongo mara vikao sijui vinafanyila baada ya miezi 6 pale BOT upumbavu mtupu hata ungekuwa wewe jirani anakwambia njoo upewe huduma za haraka unasepa tu
Benjamin anasema alipouliza muda na mchakato Tanzania na Kenya akaona Kenya ni muda mfupi kuprocess vibali factor ya pili ilikuwa lugha akaona product yake itauzika sana akitumia Kenya na sio Tanzania.Jibu rahisi, urasimu.
Minnesota kuna sehemu ukifika unaweza kudhani Kisii imehamia US.Kenya kwenye position ya jukwaa la kimataifa wametuzidi kidogo hilo tukubali.
Kwa mfano wapo maprofesa wa Kenya hapa Marekani na wafundisha vyuo vikuu hapa.
Yupo profesa Eric Otenyo afundisha afundisha sayansi ya jamii chuo kikuu cha Arizona, yupo profesa David Kimori ambae afundisha chuo kikuu cha Mankato katika jiji la Minesota, na yupo profesa mwingine kama Ruben Marwanga ambae ni mratibu wa Diaspora yote kwa wakenya kama sikosei.
Isitoshe, wakenya wana kanisa kubwa kabisa walolijenga kwa fedha zao linonifanya nishangae meli kuelea liko kwenye mji wa Massachusetts laitwa ACK mtakatifu Stephen.
Na pia wapo wakenya wengine wengi tu wenye kuweza kukupa connection ukapiga hatua mbele.
Kwenye hili nipo 100% uhakika ila sijaona watanzania huku nje tukiwa na level hizo.
Mimi naipenda nchi yangu Tanzania ila kinoendela kwa sasa chakatisha tamaa.
South Africa je? Ahahahahaha!!Uingereza ipo wapi?
Nafikiri serikali ilikwishatenga eneo Dodoma wakati wa utawala wa hayati Magufuli na balozi zikapewa viwanja bure.
Kenya wao tiyari wana maeneo maalum kwa shughuli za kibalozi kama Gigiri, Runda na Muthaiga ingawa tiyari kuna ongezeko la mahitaji na mfumuko wa bei.
Utawala bora umepigiwa kelele kwa miongo 10 sasa, huku wengine wakijipigia humohumo kwenye utawala bora.Tatizo siyo kukosekana kwa ardhi ya kutosha au Viwanja vya kujenga Ofisi za Balozi za Nchi za nje, tatizo lipo kwenye kukosekana kwa Utawala Bora wa Sheria, kukosekana kwa Demokrasia na kukosekana kwa Usalama wa umma. Siyo Siri hata kidogo, Tz kuna Utawala wa kidikteta ambao kimsingi hauvutii Wageni kutoka nje ya nchi hii kuja kuwekeza au kuja kujenga Ofisi zao hapa Tanzania. Masuala haya ya Utekaji Watu yana madhara mabaya Sana kwa nchi kimataifa.
Je, nani anataka kutekwa kama walivyotekwa Watu mbalimbali hapa Tanzania mfano wa alivyotekwa mfanyabiashara Mo Dewji?
Endapo kama Mo Dewji angekuwa siyo raia wa Nchi hii na angekuwa Mwekezaji wa kigeni hapa Tanzania kama ilivyo kwa Mfanyabiashara Aliko Dangote, Basi naamini mpaka Sasa hivi tayari angekuwa keshafunga biashara zake zote kabisa hapa Tanzania na kisha kuhama nchi.
Jiulize swali hili: Je, wewe binafsi unaweza kwenda kuanzisha biashara zako katika Nchi ya HAITI hata kama utapewa ardhi bure huko kwa ajili ya biashara zako? Je, unaweza?
Ni sawa. Dar ed salaam kuna chawa 'binsdamu' hawawezi kuishi.View attachment 3422979
Umoja wa Mataifa unatarajia kuhamishia ofisi zake za kimataifa za UNICEF, UNFPA na UN Women jijini Nairobi kufikia mwaka 2026, hatua itakayoiweka mji mkuu wa Kenya katika hadhi sawa na New York, Geneva, na Vienna kama miongoni mwa miji minne pekee duniani inayohifadhi makao makuu ya mashirika mengi ya UN.
Tayari Nairobi inahifadhi mashirika 23 ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo mashirika makuu kama UNEP na UN-Habitat.
Pia kuna mipango ya Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) kuhamishia shughuli zake Afrika, jambo litakaloongeza zaidi nafasi ya bara hilo katika majukumu ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu.
Hatua hii ni sehemu ya ajenda ya mageuzi ya UN iitwayo “UN@80”, ambapo Katibu Mkuu António Guterres ametaja ufanisi wa gharama kama sababu kuu ya mabadiliko hayo.
Gharama za uendeshaji katika miji kama New York na Geneva – kutoka kwa nafasi za ofisi hadi wafanyakazi na vifaa – ni kubwa zaidi ikilinganishwa na Nairobi.
Zaidi ya gharama, uhamisho huu pia unaonekana kama mkakati wa kuelekeza nguvu zaidi barani Afrika, ambalo linahusika na zaidi ya asilimia 60 ya shughuli za kibinadamu za Umoja wa Mataifa.
Mabadiliko haya yanachukuliwa kama ishara kubwa ya kuaminiwa kwa Nairobi kama kitovu cha kidiplomasia duniani.
=======================
Nairobi joins New York, Geneva and Vienna as only cities globally hosting multiple UN headquarters
The United Nations is set to relocate theglobal offices of UNICEF, UNFPA, and UN Women to Nairobi by 2026, elevating the Kenyan capital to the ranks of New York, Geneva, and Vienna as one of only four cities globally hosting multiple UN headquarters.
Nairobi already hosts 23 UN agencies, including flagship bodies like UNEP and UN-Habitat.There are also plans for the Office for the Coordination of Humanitarian Affairs (OCHA) to move its operations to Africa, further strengthening the region's role in global humanitarian response.
The move is part of the UN's wider "UN@80" reform agenda, with Secretary-General António Guterres citing cost efficiency as a key driver.(AD)Operating costs in New York and Geneva, from office space to staffing and logistics, are significantly higher compared to Nairobi.Beyond cost, the relocation is also seen as a strategic realignment toward Africa, which accounts for over 60% of the UN's humanitarian work.This shift is being viewed as a major vote of confidence in Nairobi as a global diplomatic hub.
Source: Developmentaid
Wakenya wamejitahidi sana.Minnesota kuna sehemu ukifika unaweza kudhani Kisii imehamia US.
We jamaa Kila siku kiwango chako cha akili kinazidi kushuka,sijui umepatwa na nini,ndugu.Kwani duniani kuna miji mitatu tu ya dar es salaam,new York na Nairobi!?..mbona hamuulizi kigali au kampala vipi?
Lengo ni kuokoa fedha na kwa hilo watakuwa na uwezo wa kuwa na kiba ya kutosha kuendesha shughuli zao kutokea Kenya yaani kuokoa operating costs na pia kuwa karibu zaidi na maeneo wanoyasaidia barani Afrika.Kama lengo ni kuokoa Hela hamna haja ya kusambaza makao makuu huku na kule.
Wamefanya vyema.
Ningeshangaa Sana endapo kama wangepanga kuhamishia Makao Makuu ya Taasisi hizo nchini Tanzania.
Licha ya mapungufu yao madogo madogo waliyonayo, bado Kenya ni nchi ya Kidemokrasia na yenye Katiba Bora ukilinganisha na nchi nyingi sana za kiAfrika na duniani kote kwa ujumla.