UN kuhamishia makao makuu ya UNICEF, UNFPA na UN Women jijini Nairobi, Tanzania tuko wapi?

Tanzania haishindani na Kenya bali na shida zake,ushabiki wenu wa mitandaoni unageuza dira ya taifa?
 
Walimletea zengwe Starlink Tanzania waligoma tupate internet bei ya chini Upigaji
 
Sie, tupo bize na gori la mama, ngome ya mama,
 
Wakenya wamejitahidi sana.

Na KA yaenda US nafikiri zaidi ya 2X a week sina uhakika.

Na ndege yatua New York City.

KA pia yashirikiana na British Airways, KLM na sasa hivi waweza kuruka kwenda New York kutokea Nairobi, Kisumu na Mombasa.
KQ tu sio ndege ya abiria hadi cargo plane walikuwa nayo direct kutoka NRB ilikuwa inafanya huduma kila baada ya siku 2 .
 
KQ tu sio ndege ya abiria hadi cargo plane walikuwa nayo direct kutoka NRB ilikuwa inafanya huduma kila baada ya siku 2 .
Yes, yapeleka bidhaa kama matunda na flowers wanazolima wazungu na wakenya matajiri.

Pia mizigo mingine ya maana.
 
Swali la kijinga na la kipuuzi kabisa kama kweli wewe ni Mtanzania. Siyo kila analofanyiwa Kenya na sisi Tanzania tufanyiwe.Mashirika haya yana uhuru wa Kwenda popote duniani na usije ukadhani Nairobi ni nzuri kuliko Pretoria au Jo'berg.Wenzenu hawa wapo huru lakini uhuru wa kushikiliwa,Bado yale mataifa makubwa sina haja ya kuyataja hapa wanaona kwamba Kenya bado ni mali yao.Na kwa ujinga wetu sisi tunaona hiyo ni sifa.Wakija kuweka kambi za kijeshi kwako,basi hapo wale ambao bado hawajakombolewa kifikra wanaona sifa kabisa kabisa kwamba wao ni sehemu yao kuanzia mavazi mpaka lugha.Wakiambiwa kwenda kuwa Polisi kule Haiti basi hapa baadhi yetu weusi tunaona kana kwamba wenzetu wameokota Dodo kwenye mchanga.Watu weusi tunatumiwa ,tunaleweshwa sifa za kijinga . Badilikeni.
 
Kwa kiingereza twasema "you are missing a point".

Kenya hawafanyiwi chochote bali wizara yao ya mambo ya nje iko active.

Pili hata raisi wao Ruto alipokwenda Washington alikuwa katika mkakati wa kukaribisha wageni na wawekezaji wengine na alikutana na Guterez SG.

Na hawa wawezekezji au wageni mara nyingi hufanya kitu chaitwa PESTLE analysis, sifahamu kama una uelewa wa hii formular.

Kwa Tanzania hadi sasa ukiifanyia PESTLE analysis yafeli (kwa mtazamo wao) kwenye maeneo kama political instability, environmental (miundombinu isokamilika) na hata kwenye economy yaani utaratibu wa kodi na teknolojia ni ndo kabisa Internet yasumbua kidogo upatikanaji wake.

Kwenye legal au masuala ya sheria na mahakama usiwaone wageni waja pale mahakamani kumuangalia tu Tundu Lissu bali pia wasoma mfumo wenu wa sheria waendeshwaje na je ni safe kwao kwao endapo kuna shida.

Sasa kwa wachambuzi (analysts) na majasusi hufanya hii PESTLE na kutoa report kisha huwapa wakubwa wasome na kinofuata na kuangalia wapi pafaa zaidi.
 
Bi kizimkazi tupo busy kuteka na kupoteza watu
 
KENYA NI SEHEMU YENYE GHASIA NA FUJO SANA,ARUSHA ILISTAHILI SANA.
 
Lugha Lugha Mifumo ya Nairobi ni supportive sana na hakuna Ujinga wa politicians kupiga simu mahakamani kama ilivo kisutu apo
 
Wengi mmeandika malalamiko badala ya sababu halisi, hii Ina reflect hata IQ zetu ni ndogo tu.

Settlers bado wapo pale, hivyo maslahi ya wazungu hayajaguswa.

Kambi za jeshi za Marekani na Mwingereza, nje ya usalama duni ila uwepo wa hao jamaa unahakikisha usalama wao.

Zipo makao makuu ya taasisi nyingine za UN na balozi mbali mbali

Transportation hub ya east Africa

Siasa zetu zinazobadilika bila uelekeo
 
Viongozi wetu akili yao ni kwenye kuiba tu mali za kwetu sote,
Wangekuwa na visions haswa tanzania ingekuwa mbali mnooo.

Mtu mwenye akili yake haweza leta hivyo vitu tanzania yetu hii.
Kwani kenya viongizi wao hawaibi?
 
Mwanzo ilikuwa wahamie Dar es salaam lakini waliacha na sababu waliyoitoa ni kuhusu usalama mdogo maana wapinzani wanatekwa sana,Hivyo,waliepusha watumisha wao wasitekwe maana serikali hii haiaminiki
 
Haya mashirika bwana yule nzilankende aliwazungua sana mpaka UN women walifunga ofisi zao bongo wakabakiza staff kadhaa tu. Hii haiwezi kurudisha imani zao kwetu kwa haraka taking into consideration of the current socio-political circumstances happening in our country.

Rais aliyeingia angehakikisha anarudisha imani yao kwetu but ndio hivyo tena.

Waafrika hatuaminiki.
 
Kwani duniani kuna miji mitatu tu ya dar es salaam,new York na Nairobi!?..mbona hamuulizi kigali au kampala vipi?
Baadhi ya balozi kuhamishia huduma zake jirani hapa nchini zikibaki kama balozi ndogo unaona ni sawa tu siasa zinakufanya uwaze kila kitu na sawa ?​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…