UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

It is sad kwa mtu kujikita katika kukubaliana na thinking ya watu wasioitakia mema nchi hii.
To buy the UN view ati kwa vile wanafadhili miradi humu Tanzania, so we should dance to their whims is a radher absurd .
Sijui watanzania tutatoka lini kstika haya mawazo ya. Utegemezi kifikra, kwamba maendeleo yatakuja kwa ufadhili wa mzungu, na si vinginevyo.

So , If UNESCO or any UN affiliate so decides, umeme wa DOWANS, AGGREKO, IPTL, ni sawasawa llakini wa Steigkers Gorge, hapana.
My foot , watanzania tunasafari ndefu kujikomboa kifikra.
Ur ryt tuna safari ndefu sana
 
Kwahiyo unaamini kabisa kwamba ni hayo makampuni ndiyo yapo behind all this?! Btw, kama hoja ni kampuni zinazoikamua TANESCO, mbona hatukuwasikia hao UNESCO au taasisi yoyote ikipinga ujenzi wa bomba la gas ambalo serikali pia ilisema itakuwa ndio mwisho wa uhaba wa umeme?!

In addition, huo mradi wa Stigler ukishakuwa materialized unadhani utajengwa na wanani kama sio makampuni yenye asili ile ile? Mitambo toka nchi zile zile! Vipuri toka pande zile zile! Experts toka kule kule... and so much more!

So, do you really believe hayo makampuni hayautamani huu mradi ufanyike?!

Itoshe tu kusema kwamba Tanzania sio nchi ya kwanza na wala haitakuwa ya mwisho kwa UNESCO ku-criticise miradi iliyokuwa planned kwenye World Heritage Sites kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo! Selous Games Reserve ni moja ya World Heritage Sites ambazo UNESCO wana-finance protection yake!

So long as hizi World Heritage Sites zinakuwa under UNESCO, they will always criticize jambo lolote wanaloona litahatarisha wanachokilinda!

Kimsingi; hawakukatazi kufanya utakacho lakini watapinga kwa sababu ni wajibu wao!

Kama nchi imejitosheleza unaweza kuwavimbia cuz' all they can do ni ku-withdrawal site husika from among world heritage sites!

Kama ni nchi ya kutegemea misaada na external financing; wataenda kukusubiria huko... watafanya lobbying kuhakikisha you get no financing! Hili ndilo lilimfanya JK aufyate kwenye Stigler Gorge kwa sababu alitarajia financing from Brazil!

That said, acheni hizi porojo za eti cjui Dowans mara IPTL! UNESCO wanatimiza wajibu wao!

Na kama hamuwataki; Tanzania inaruhusiwa ku-withdrawal... hata Ronald Reagan, back 1983 aliitoa USA from UNESCO!
Bomba la gesi pia ulikua mradi mkubwa wa kifisadi...Mradi wa Stglers ilikua idea ya Nyerere ila wapiga deal waliokua nyuma ya makampuni ya kifsadi yanayoinyonya Tanesco hawakuuyaka cz baada ya Stglers Tanzania haitahitaji tena huu umeme wa wizi...Bu namuamini Rais wangu JPM hzo ni kelele za chura na vibaraka wao ila mradi utajengwa aliyajua haya ndio maana alisema hatajali mambo ya UNESCO
 
Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop! UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Hakuna uhujumu hapo Mkuu, acha kuwa dramatic. Ukweli ni kwamba siku moja miaka ya baadaye, ikiwa hatutatekeleza huu mradi, tutawashukuru UN na wadau wote wanaopinga huu mradi usijengwe.

Tanzania ina gesi nyingi sana ya kuzalisha umeme kwa ajili ya nchi zote za Afrika Mashariki na bado ukabaki. Sasa kiherehere cha Stiegler Gorge ni cha nini? Siku tukiwa tume-exhaust capacity yote ya kuzalisha umeme kwa gesi Songo Songo na Mtwara, na makaa ya mawe huko Liganga na Kiwira na bado tukawa na uhitaji zaidi wa umeme basi tuongee kujenga bwawa la umeme Stiegler Gorge. Lakini kwa sasa hakuna umuhimu. Hii Stiegler's Gorge ipewe kipao mbele kama world heritage site kwa faida na urithi wa vizazi vijavyo. Tuache ubishi usio na sababu. Magufuli anatudanganya tu hapa, anachotaka kuonyesha ni ubabe na ku-nurse ego yake kwenye hili jambo la Stiegler's Gorge.
 
Nzuri,
Patrice.
Niombe radhi kwanza kwa kutumia neno mjinga, nilikosea kwa kuwa sikulitolea ufafanuzi.
Nashukuru kwa kunipa mtiririko wa mifano hai kabisa, ya nchi zinazotumuia umeme wa maji.
Lakini ukiangalia nature ya hizo nchi zenye hayo mabwawa utakuta ni tofauti kabisa na sisi. Kwanza ukubwa wa nchi zenyewe, utayari, mipango na mikakati yao pamoja na utaalamu. Kwahiyo nafuu ya mradi kama huo kwa China na USA ni tofauti kabisa na nafuu yetu. Sijui kama unanielewa hapo.
Kwanza rasilimali pesa, watu, wataalamu na vifaa vyote wanatengeneza wenyewe, kwahiyo suala la nafuu zitoe hizo nchi.
Ukienda kwa Ethiopia nature yake ni milima na misitu mikubwa inayotunzwa kwa hali ya juu sana, kwa maana hiyo mvua kwao ni suala la lazima na bwawa lile litadumu sana.
Ukija kwetu Tanzania, linapotaka kujengwa hilo bawa hakuna misitu yoyote ya kupandwa, zaidi ya wenyewe kuona hill bonde eti ndio lizibwe ili ilijazwe na maji ya mvua, nakuambia hatujajiandaa na hatutafanikiwa, na ghalama zake zitazidi kuongezeka siku hadi siku.
Hayo mabwawa yanajengwa kwenye miinuko ya zaidi ya 1000 kutoka usawa wa bahari, lakini sio kwenye mabonde yaliyobondeni hapana nakuambia tena kwetu sio kipaumbele, muda utakuja kukuambia.
Mwisho wanataka kujenga ndani ya hifadhi ya wanyama, moja kwa moja itakuwa ni uharibifu wa mazingira.
Tuwe wa kweli tumeshindwa kuendeleza bwawa la Hale, Mtera na K
ihansi leo tuje tena na Rufiji?
Jamani kupanga ni kuchagua yetu macho.

HABARI,
"Gullam,
Hongera umefanya vema kuomba radhi najua Comrade atakuwa amesamehe.
Sasa hapo unapoongea nfuu na utayari kwa hizo Nchi wewe umesema umeme wa maji umupitwa na wakati mimi nataka unifafanulie umepitwa vipi na wakati ikiwa nchi hizo kubwa bado wanatumia,Unapozungumzia ukubwa hata sisi Tanzania ni kubwa na hilo bwana La Steiglers Gorge Litazalisha MW2100 ambazo mpaka sasa vituo vyote vinavyozalisha umeme vya maji,gesi,Mafuta nchi nzima havijafika mw1800 na hiyo mw2100 ilikuwa ni teknologia ya miaka hiyo ya 80 ninauhakika wanaweza kuongeza Uzalishaji kama wakitumia teknologia za kisasa,Na eneo hilo kama umesema swala la wingi wa maji ni maji ya mto rufiji ambao mito yote mikubwa inaingiza maji pale na mwaka mzima unamwaga maji baharini kwahiyo swala la wingi wa maji hilo sio tatizo ndio maaana mradi huo waliuona toka miaka 30 iliyopita na pia kunabwawa moa pia wanataka kulijenga morogoro linaitwa kidunda nalo litakuwa linahifadhi maji mengi kipindi ya mvua na linategemewa kuhudimia maji kwa mikoa ya morogoro na dar kwa miaka ya baadae pamoja na kuyaachia kumwagika kwenye hilo bwawa la rufiji.
Pia ukisema swala la utayari Tanzania tuko tayari mahitaji ya umeme ni makubwa sana swala la pesa.rasilimali watu vifaa hilo sio tatizo kuna mikopo na hata ukisema ishu ya Ethiopia wana milima hata sisi ruaha inatoka kwenye milima mbeya iringa ndio inamwaga maji rufiji panapotaka kujegwa mradi na pia unaambia eneo linapotakiwa kuengwa hilo bwawa haizidi asilimia 10 ya hifadhi yotena hao wamarekani hawataki tuenge hilo bwawa wao ndio wenye makampuni kama symbion ambayo tanesco yanawalipa hela nyingi kila mwaka hata kama hawajazalisha umeme hawataki tujitosheleze kwa umeme umoja wa mataifa ni kwa maslahi ya Mataifa makubwa sio nchi masikini comrade.

LUMUMBA
 
Wewe ulitaka fact gani kwa mfano.
The pros and cons of 2,100megawatts, hilo halihitaji mjadala.
Project hii ipo inapingwa na UN toka enzi za Mwalimu.
Tukumbuke ni watu hawahawa walipinga hata ujenzi wa TAZARA miaka ya mwanzoni mwa 1970s.

Tuliambiwa gesi ya Mtwara itazalisha umeme ambao tutaweza kuuza nje ya nchi. Hii stori imeishia wapi?
 
Tuliambiwa gesi ya Mtwara itazalisha umeme ambao tutaweza kuuza nje ya nchi. Hii stori imeishia wapi?
Tatizo viongozi wa Tanzania wanarukia mambo kama tumbili wanavyorukia matawi ya miti. Mara nyingine hawakai wakatulia kwenye tawi moja na kuangalia kinachoendelea kwanza kabla ya kurukia tawi jingine. Kama tumbili, ni rahisi kukuta umerukia kwenye tawi ambalo chui yupo anakungojea akutafune!
 
Kwako wewe kuwa m tanzania ni kulisupport lile jizi number moja linalotumia kivuli cha uzalendo kutuibia watanzania
Limeshathibitika kwamba ni jizi au unajiongela tu kwa sababu ya mlengo wa kisiasa? Angalia statement yako ndio inayothibitisha kwamba kauli yako ilifaa kutolewa na mtu ambaye sio mtanzania
 
Limeshathibitika kwamba ni jizi au unajiongela tu kwa sababu ya mlengo wa kisiasa? Angalia statement yako ndio inayothibitisha kwamba kauli yako ilifaa kutolewa na mtu ambaye sio mtanzania
Kwako wewe kuibua ufisadi wa jizi lenu hilo mnalolitetea ndo si utanzania
 
Kwa hili uncle Magu kaza buti mjomba,hapa nipo pamoja na wewe,yaani wakoloni wetu waendelee kututawala kifikra hata enzi hizi,hapana aiseee,kaza buti mjomba,chinga mimi nipo pamoja na wewe
 
Vipi kuhusu mkandarasi ,VP ashapatikana? Watu tunatakatu tutumie fursa zilizopo katika mradi huu
 
View attachment 701335

Nimesoma katika gazeti la The Guardian on sunday, tar 25 Feb 2018, ati UN(Umoja wa Mataifa), wanapinga kujengwa kwa kituo cha kuzalisha umeme kiasi cha 2,100MW ati kwa sababu za mazingira.

Huu ni uhujumu, full stop!

UN inatumiwa tu, ili ujumbe uonekane ati unatoka chombo ambacho ni fair, lakini ujumbe huo ni lazima unatoka nchi zinazofaidika na matatizo yetu ya nishati.

Kampuni za kimarekani kama AGGREKO, DOWANS na nyingine nyingi ni wazi zisingependa kuona mradi huu wa Stieglers Gorge ukifanikiwa, maana watakosa ulaji wanaofaidika nao leo.

Kama ingewapendeza UN, basi Three Gorges Dam ya China, Aswan Dam ya Misri, Akosombo Dam ya Ghana vyote visingejengwa kwa sababu za kimazingira.

Nampongeza sana Rais Magufuli na kumpa moyo kushika moyo ule ule , ili nchi ijitawale kinishati.
Tutajenga hata waseme nini wapumbavu hao. Kwanini watupangie maisha yetu?. Pumbavu zao
 
Back
Top Bottom