UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Ur ryt tuna safari ndefu sana
 
Bomba la gesi pia ulikua mradi mkubwa wa kifisadi...Mradi wa Stglers ilikua idea ya Nyerere ila wapiga deal waliokua nyuma ya makampuni ya kifsadi yanayoinyonya Tanesco hawakuuyaka cz baada ya Stglers Tanzania haitahitaji tena huu umeme wa wizi...Bu namuamini Rais wangu JPM hzo ni kelele za chura na vibaraka wao ila mradi utajengwa aliyajua haya ndio maana alisema hatajali mambo ya UNESCO
 

Hakuna uhujumu hapo Mkuu, acha kuwa dramatic. Ukweli ni kwamba siku moja miaka ya baadaye, ikiwa hatutatekeleza huu mradi, tutawashukuru UN na wadau wote wanaopinga huu mradi usijengwe.

Tanzania ina gesi nyingi sana ya kuzalisha umeme kwa ajili ya nchi zote za Afrika Mashariki na bado ukabaki. Sasa kiherehere cha Stiegler Gorge ni cha nini? Siku tukiwa tume-exhaust capacity yote ya kuzalisha umeme kwa gesi Songo Songo na Mtwara, na makaa ya mawe huko Liganga na Kiwira na bado tukawa na uhitaji zaidi wa umeme basi tuongee kujenga bwawa la umeme Stiegler Gorge. Lakini kwa sasa hakuna umuhimu. Hii Stiegler's Gorge ipewe kipao mbele kama world heritage site kwa faida na urithi wa vizazi vijavyo. Tuache ubishi usio na sababu. Magufuli anatudanganya tu hapa, anachotaka kuonyesha ni ubabe na ku-nurse ego yake kwenye hili jambo la Stiegler's Gorge.
 

HABARI,
"Gullam,
Hongera umefanya vema kuomba radhi najua Comrade atakuwa amesamehe.
Sasa hapo unapoongea nfuu na utayari kwa hizo Nchi wewe umesema umeme wa maji umupitwa na wakati mimi nataka unifafanulie umepitwa vipi na wakati ikiwa nchi hizo kubwa bado wanatumia,Unapozungumzia ukubwa hata sisi Tanzania ni kubwa na hilo bwana La Steiglers Gorge Litazalisha MW2100 ambazo mpaka sasa vituo vyote vinavyozalisha umeme vya maji,gesi,Mafuta nchi nzima havijafika mw1800 na hiyo mw2100 ilikuwa ni teknologia ya miaka hiyo ya 80 ninauhakika wanaweza kuongeza Uzalishaji kama wakitumia teknologia za kisasa,Na eneo hilo kama umesema swala la wingi wa maji ni maji ya mto rufiji ambao mito yote mikubwa inaingiza maji pale na mwaka mzima unamwaga maji baharini kwahiyo swala la wingi wa maji hilo sio tatizo ndio maaana mradi huo waliuona toka miaka 30 iliyopita na pia kunabwawa moa pia wanataka kulijenga morogoro linaitwa kidunda nalo litakuwa linahifadhi maji mengi kipindi ya mvua na linategemewa kuhudimia maji kwa mikoa ya morogoro na dar kwa miaka ya baadae pamoja na kuyaachia kumwagika kwenye hilo bwawa la rufiji.
Pia ukisema swala la utayari Tanzania tuko tayari mahitaji ya umeme ni makubwa sana swala la pesa.rasilimali watu vifaa hilo sio tatizo kuna mikopo na hata ukisema ishu ya Ethiopia wana milima hata sisi ruaha inatoka kwenye milima mbeya iringa ndio inamwaga maji rufiji panapotaka kujegwa mradi na pia unaambia eneo linapotakiwa kuengwa hilo bwawa haizidi asilimia 10 ya hifadhi yotena hao wamarekani hawataki tuenge hilo bwawa wao ndio wenye makampuni kama symbion ambayo tanesco yanawalipa hela nyingi kila mwaka hata kama hawajazalisha umeme hawataki tujitosheleze kwa umeme umoja wa mataifa ni kwa maslahi ya Mataifa makubwa sio nchi masikini comrade.

LUMUMBA
 
Wewe ulitaka fact gani kwa mfano.
The pros and cons of 2,100megawatts, hilo halihitaji mjadala.
Project hii ipo inapingwa na UN toka enzi za Mwalimu.
Tukumbuke ni watu hawahawa walipinga hata ujenzi wa TAZARA miaka ya mwanzoni mwa 1970s.

Tuliambiwa gesi ya Mtwara itazalisha umeme ambao tutaweza kuuza nje ya nchi. Hii stori imeishia wapi?
 
Tuliambiwa gesi ya Mtwara itazalisha umeme ambao tutaweza kuuza nje ya nchi. Hii stori imeishia wapi?
Tatizo viongozi wa Tanzania wanarukia mambo kama tumbili wanavyorukia matawi ya miti. Mara nyingine hawakai wakatulia kwenye tawi moja na kuangalia kinachoendelea kwanza kabla ya kurukia tawi jingine. Kama tumbili, ni rahisi kukuta umerukia kwenye tawi ambalo chui yupo anakungojea akutafune!
 
Kwako wewe kuwa m tanzania ni kulisupport lile jizi number moja linalotumia kivuli cha uzalendo kutuibia watanzania
Limeshathibitika kwamba ni jizi au unajiongela tu kwa sababu ya mlengo wa kisiasa? Angalia statement yako ndio inayothibitisha kwamba kauli yako ilifaa kutolewa na mtu ambaye sio mtanzania
 
Limeshathibitika kwamba ni jizi au unajiongela tu kwa sababu ya mlengo wa kisiasa? Angalia statement yako ndio inayothibitisha kwamba kauli yako ilifaa kutolewa na mtu ambaye sio mtanzania
Kwako wewe kuibua ufisadi wa jizi lenu hilo mnalolitetea ndo si utanzania
 
Kwa hili uncle Magu kaza buti mjomba,hapa nipo pamoja na wewe,yaani wakoloni wetu waendelee kututawala kifikra hata enzi hizi,hapana aiseee,kaza buti mjomba,chinga mimi nipo pamoja na wewe
 
Vipi kuhusu mkandarasi ,VP ashapatikana? Watu tunatakatu tutumie fursa zilizopo katika mradi huu
 
Tutajenga hata waseme nini wapumbavu hao. Kwanini watupangie maisha yetu?. Pumbavu zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…