UN: Watoto 10,000 wameuawa katika vita ya muda mrefu ya Yemen

UN: Watoto 10,000 wameuawa katika vita ya muda mrefu ya Yemen

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Zaidi ya watoto 10,000 wameuawa au kujeruhiwa nchini Yemen katika vurugu zinazohusiana na vita vya muda mrefu katika taifa hilo masikini.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto, UNICEF, James Elder, amewaeleza waandishi wa habari kwamba takwimu zilizothibitishwa na Umoja wa Mataifa ni za chini kwa sababu vifo vingi vya watoto na majeruhi havirikodiwi. Kwa muda mrefu, Yemen imechukuliwa kuwa nchi yenye mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.

Vita vilizuka tena mwishoni mwa mwaka 2014 baada ya waasi kuuchukua mji mkuu, Sanaa. UNICEF inasema kuwa watoto wanne kati ya watano wanahitaji usaidizi wa kiutu, ambao ni sawa na karibu watoto milioni 11.

Jumla ya watoto 3,455 waliuwawa na wengine 6,000 kujeruhiwa katika mapigano ya Yemen baina ya machi 2015 hadi Septemba 30 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom