Ni mgeni gani anaefurahishwa huko Ololosokwan?
Je unao uelewa kwamba kelele za Loliondo sio kuhamishwa bali ni kutengewa eneo rasmi la malisho.
Serikali imewaachia
2500sq km na sasa inaweka Beacon kwenye eneo liliotengwa kwa uhifadhi kama Buffer zone.
Nyinyi huku mmekazana kupiga tararira oooh Loliondo kuna Genocide...
Mnaijua maana ya Genocide?
Mnaelewa Loliondo na sheria zake kuhusu uhifadhi?
Mnaropoka sana kwenye keyboard mpaka mnachafua screen kwa mapovu bila uelewa.
Kule Ngorongoro NCAA nako ni kwamba watu wanahama ili kupisha shughuli za uhifadhi.
Tena kwa hiari yao wenyewe
Nyinyi huku mnapayuka ovyo utadhani huwa mbawasaidia chochote kwenye maisha yao ya kila siku.
Kwa hiyo hapa wewe umejipachika ujuaji,; ulijuaje kama hukuambiwa? Na iweje serikali isiwe na uwezo wa kueleza inachonuia kufanya watu wakakielewa, bali iweke kama siri kwa watu wachache kama wewe, kwa manufaa ya nani?
Huoni hilo pekee ni udhaifu mkubwa kwa seriakali..., au wewe ndiyo muhusika uliyepewa wajibu wa kutoa taarifa sahihi halafu ukaamua kutoa upotoshaji kwa lengo la kuleta sintofahamu katika jamii husika na nchi nzima?
Sasa angalia, hiyo "genocide" imeingiaje hapo, au mambo kama hayo ndiyo yako ndotoni mwako?
Kule Ngorongoro NCAA nako ni kwamba watu wanahama ili kupisha shughuli za uhifadhi.
Tena kwa hiari yao wenyewe
Kama ni kwa "hiari yao" kelele zingetoka wapi, hivi unayo akili timamu au unajiandikia tu yanayoingia kichwani bila ya tafakari juu yake?
'Bottomline', ni hii, endapo kama serikali inafanya mambo yaonekane yana chembechembe za ubabaishaji na usiri usiokuwa na maana yoyote, hapo watu watauliza maswali mengi, hata kama baadhi ya maswali hayo si sahihi.
Serikali yoyote haiwezi kuvuruga wananchi wake kwa lengo la kuweka wageni wafaidike kwa maumivu ya wananchi wake.
Iwe kweli au isiwe kweli, ni wajibu wa serikali kutoa taarifa sahihi juu ya malengo yanayokusudiwa wakati wananchi wanahamishwa.
Zaidi ya yote, ni wajibu wa serikali kuwa wakweli kabisa kwa wananchi wanaohamishwa, na kuwapa taarifa zilizo sahihi bila ya ubabaishaji na uongo mwingi ndani yake.
Hiyo kazi ya kuwaelimisha wananchi kwa miezi minne na kuwahamisha katika wakati huohuo, wewe hapo huoni ubovu wake?