Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imesema ina wasiwasi kuhusu taarifa za vifo, majeruhi, watu kupotea na kukamatwa katika muktadha wa uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba nchini Tanzania.
Hayo ni kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo, Volker Turk, ambaye ametoa wito wa familia kupata taarifa kuhusu wapendwa wao, pamoja na kuheshimiwa kwa haki za msingi kama uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani, na uwajibikaji.
Taarifa ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imeeleza kutambua kuwa Serikali ya Tanzania imeanzisha uchunguzi kuhusu matukio ya baada ya uchaguzi, na kusisitizia kuwa uchunguzi huo uzingatie viwango vya Kimataifa, ikiwemo uhuru, kutopendelea upande wowote, uwazi na ulinzi kwa wanaotoa ushirikiano.
Aidha, Ofisi hiyo imesema tangu katikati ya Novemba, 2025 kumekuwapo pia taarifa za kukamatwa kwa wasomi, viongozi wa kisiasa na watendaji wa asasi za kiraia, hivyo kutoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa wote waliokamatwa kiholela.