Jana niko zangu home nimetulia, nje namsikia jirani yangu ambaye anafanya kazi na mke wangu.(walimu) Alikuwa akimuita mke wangu aende amfuate alipo na jibu la wife lilikuwa njoo wewe, jirani akawa analazimisha wife aende na yeye anamuambia njoo ww huko siwezi kuja lkn jirani alikuwa anaendelea kusisitiza wf aende mara moja.
Ila wife alikaza kwa kumsisitizia huko siwezi kuja.
Mwisho jirani akaja mpka home na kuendelea kumsisitizia wf twende mara moja ila bado wf akakataa na kumuuliza kwani wanashida gn? Wewe twende ukawasikilize.....
Baada ya kuona ule msisitizo sio wakawaida ikanibidi nichungulie dirishani.
Kwa mbali kuna washikaji km watatu hivi ndio walikuwa na yule jirani yetu na wao ndio walikuwa wanamtumia kumuita wf pale akawasikilize na wf ni km alikuwa ananisikilizia mimi km nitamruhusu.
Ila binafsi baada ya kuona kuna msisitizo usio na maelezo ya wazi,nikamzuia wf asiende na kumuambia amuambie jirani awaambie wale wenye uhitaji wafike nyumbni km hawana ndhamira mbaya lkn jamaa hawakuja
Nilichoamua baada ya hili tukio ni kumuibukia jirani kumuonya kuheshimu familia za watu na kujua mipaka yake, kw mke wng sijaona cha kuzungumza nae zaidi sababu hakuomba hta ruhusa ya kutaka kwenda. Je! Kwa uamizi huu niko sahihi?