Brayan_Jk
JF-Expert Member
- Mar 28, 2025
- 210
- 250
Nimefuga kwa miaka kadhaa ,kwa mtu ambaye anataka kuanza serious ufugaji wa kuku 2026 ,ningemshauri azingatie haya
Habari ya mwaka mpya wafugaji wenzangu,
Kila mwaka kuna watu wengi wanaanza ufugaji wa kuku kwa matumaini makubwa, lakini wengi wao wanakata tamaa njiani kutokana na hasara ambazo zingeweza kuepukika.
Binafsi, kama ningekuwa naanza ufugaji wa kuku mwaka 2026, haya ndiyo mambo 4 muhimu sana ningeanza nayo kabla hata ya kununua vifaranga.
1.Wateja wako au soko unalolenga
Hili watu wengi hulipuuza sana.
Kabla hujaanza kufuga, jiulize:
Unalenga kuuza kwa migahawa?
Taasisi kama shule na hospitali?
Au unauza kwa mtu mmoja mmoja mtaani?
Ni kuuza kwa jumla au rejareja?
Kumuelewa mteja wako mapema kunakusaidia kujua:Ufuge kuku wa aina gani (mayai, nyama au mchanganyiko),Ufuge kuku wangapi,Na hata bei yako itakuwaje
Usianze kufuga kwanza halafu ndipo uanze kutafuta au kujifunza kuhusu soko mara nyingi hii ndiyo chanzo cha hasara.
2.Bajeti yako halisi
Ufugaji wa kuku si kuanza tu, bali ni kuhimili hadi uanze kuuza.Ni muhimu sana kujiuliza:Hela niliyonayo inatosha kufuga kuku wangapi?
Inatosha hadi lini kabla ya kuku kuanza kuingiza kipato?
Je, nitaweza kumudu chakula, chanjo na gharama nyingine bila pesa kukatika?
Wafugaji wengi huanguka hapa kwa sababu wanaanza bila makadirio ya gharama.
Kwa sasa kuna apps kama Fuga App zenye kipengele cha makadirio kinachokusaidia kuona:
Unahitaji pesa kiasi gani
Ni vitu gani muhimu kuanzia mwanzo
Hii inakusaidia kuanza kwa uhalisia, si kwa kubahatisha.
3.Utunzaji wa rekodi
Wahenga walisema😂😂: “Mali bila daftari hupotea,bila habari” na hili ni kweli sana kwenye ufugaji.
Changamoto kubwa kwa wafugaji wengi ni:Hawajui gharama halisi ya kuku mmoja,Hawajui kama wanapata faida au hasara,Wanakadiria tu kwa hisia. Kutunza rekodi ya Chakula,Chanjo
,Vifo na Mauzo kunakupa picha halisi ya biashara yako.
Kwa njia za kisasa kama Fuga App, unarekodi kila kitu kwa urahisi na unaona:Gharama ya kuku mmoja na Faida au hasara baada ya kuuza
4.Usafi na kinga dhidi ya magonjwa
Hasara kubwa kwa wafugaji wengi haitokani na soko tu, bali magonjwa.
Usafi mzuri bandani + kufuata ratiba sahihi ya chanjo,Hupunguza vifo,Hupunguza gharama za madawa,Hukuza uzalishaji bora
Ni muhimu kwako mfugaji Kuwa na ratiba ya usafi Kushirikiana na maafisa mifugo,Kufanya chanjo kwa wakati, si baada ya dalili kuonekana
Kinga ni nafuu kuliko tiba hasa kwenye ufugaji wa kuku.
Kwa wanaopenda njia za kisasa, apps kama Fuga App zinarahisisha usimamizi wa kuku kwa urahisi zaidi. Pakua playstore kupitia link hii[ Fuga - Apps on Google Play]
Nawatakia kila la heri wote wenye mipango ya kuanza ufugaji wa kuku 2026✨
Karibuni tushirikishane uzoefu