Una mipango gani kwa miaka 10-20 ijayo?

katika upuuzi ambao si huweki akilini ni huu....sijui nikifka miaka hii nifanye hiki , lazima niwe na hiki sijui kazi . naacha vitu vifanyike vile Mungu anapenda , muhimu naweka juhudi tu na nidhamu ya kile nachokifanya kwa wakati huo.
 
Kazi zangu nafanya masaa 8 kwa wiki, inategemea na project niliyonayo. Projects nyingi ni za malipo kwa hourly rate ($15 per hour) kwa sasa nafanya Brand & Identify Design kwahiyo process nzima naikamilisha kwa wiki moja ila kwa wastani wa kazi kufanyika 1 hour per day. Kwa mwezi nalenga kufanya projects 4 tu.

Muda unaobaki siyo kuwa hauna kazi. Muda mwingi natumia kujifunza Front-end Web Development.

Kwa siku nimegawa masaa 24 kwa 3. Masaa 8 ya kupumzika, masaa 8 ya kazi na kujifunza, masaa 8 yanayobaki itategemea na siku husika nina mambo gani yanayonitaka kuyafanikisha.

Gharama yangu ya milo 3 hailingani kila siku ila kwa wastani TZS 5,000 kwa siku.

Maisha ya "freestyle" nayo ni mazuri yanakufanya ufurahie zaidi kila siku unayoishi. Maisha ya kazi na kutimiza ndoto yamejaa stress za kutosha tu. Kimsingi hapa Duniani hakuna mapumziko. 😄
 
Unasumbuliwa na utoto tu sio jingine, ungejua maisha yenyewe wala usingeandika hayo, haya uhusiano wote na maisha halisi kabisa, determinants za maisha ya mtu nyingi ni external 20% ndo personality yako, sijui kama unalojua hilo?
Maisha ya mtu yako siku mimba imeingia mpaka siku ya kuzaliwa na jina lake,ni hivyo Ndivyo,namba pekee zinaongea
 
😂😂😂

Maisha yanabadilika fasta sana. Nadhani wahitimu wengi huwa wana picha zao kubwa kichani ambazo wakija mtaani ni tofauti. Kiukweli mimi mpaka namaliza sikuwahi kuwa na mawazo makubwa sana kwenye maisha yangu. Zaidi nilijua nikirudi mtaani mambo yatabadilika, na kweli ndiyo kilichotokea ila taratibu naanza kuendana na kasi ya Dunia na maisha kwa ujumla.
 
Ni kama tunafanana
 
katika upuuzi ambao si huweki akilini ni huu....sijui nikifka miaka hii nifanye hiki , lazima niwe na hiki sijui kazi . naacha vitu vifanyike vile Mungu anapenda , muhimu naweka juhudi tu na nidhamu ya kile nachokifanya kwa wakati huo.
Ni sawa kabisa kuwa na mitazamo tofauti ila naamini hata juhudi na nidhama ya kile unachofanya ni mpango kazi.
 
Una kitu utafika mbali ila hapo kwenye mlo inabidi uongeze.

Huwezi kutumia elfu tano kwa siku halafu ukasema unapata mlo kamili na kama hupati mlo kamili ni vigumu sana kufikia hayo malengo yako hasa kwa aina ya kazi unazofanya.

Nikutakie kila la heri.
 
pia ningekushauri focus zaidi kwenye stocks na sio crypto....
 
Kweli kabisa, lengo langu kubwa ni kupata mlo kamili. Mimi ni mmoja wa watu wanaotumia sana junk foods: vyakula vya viwandani, soda n.k. Nataka kupunguza au kuachana na hivi vitu kabisa.

Mlo kamili ni gharama ila nataka kuupata kila siku. Afya yangu kwa sasa imekuwa kipaumbele zaidi.

Asante sana kwa maoni yako.
 
Hizi ni project writting za wahitimu wa diploma vyuoni.......sina la kusema zaidi ya kukuambia kwamba "real life is complicated and uncertain" sio bookish
NAKAZIA.
 
pia ningekushauri focus zaidi kwenye stocks na sio crypto....
Soko la Crypto lilikuja na hype kubwa sana ikabidi nijifunze maana ni rahisi kuelewa kuliko Stocks.

Crypto haitabiriki naona kwa sasa hali mbaya ila natarajia kuipata elimu ya Stocks vizuri zaidi maana ina vitu vingi vya kujifunza kabla ya kuingia huko.

Asante sana kwa ushauri wako.
 
Sasa hivi wakati tupo JF kuna watu wanaweka mipango ya kuwa mabilionea wakiwa hawana hata TZS 100. Hiyo yote bado haimaanishi kuwa watafeli, wapo watakaoweza kufika mwisho na watakaoishia njiani.

Mimi najiona bado nina ndoto ndogo sana ukilinganisha na watu wengine. Kwenye maisha usipojiamini mwenyewe hakuna atakayekuamini.
 
baada ya kutoka migodini nilipigwa chini na my wife to be,...nikapambana sana, nikakaa sawa KISAIKILOJIA na kuanza kupata elimu mbalimbali katika nyanja za kidijitali,...nimejifunza zaidi kuhusu forex, crypto,na stocks... stocks ni the best, kwa kuwa na SHARES sio (kutrade).... cryptos zitapanda kwa baadae kwan zinazidi kutumiwa zaidi na watu kwenye black business and international exchanges,lakini ziko nyingi mno na zinazidi kuongezeka na ni very complicated kwenye kufahamu ni factors gani zitachochea kupanda kwa thaman ya crypto fulani tu na sio zinginezo ... kwenye stocks focus na NASDAQ, SP500, PEPSI and COCA-COLA.. different tech startups and wine companies.....soma hizo tu mdogo wangu naamini zitakusaidia zaidi hata ya unavyodhani....
 
Asante kwa muongozo.
 
Hamna tofauti na mtu anaesema atakuja kua mfanyabiashara mkubwa wa magari dunia nzima wakati hata pipi hajawahi uza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…