Una mipango gani kwa miaka 10-20 ijayo?

Una mipango gani kwa miaka 10-20 ijayo?

katika upuuzi ambao si huweki akilini ni huu....sijui nikifka miaka hii nifanye hiki , lazima niwe na hiki sijui kazi . naacha vitu vifanyike vile Mungu anapenda , muhimu naweka juhudi tu na nidhamu ya kile nachokifanya kwa wakati huo.
 
Kabla sijachangia naomba kufahamu
1. Unafanya kazi masaa mangapi kwa siku /wiki kulekea hizo ndoto zako.
2. Gharama ya mlo wako mmoja hua ni kiasi gani lets say lunch au breakfast.

Ndani ya mada . Sina mpango wowote ule hua naishi kwa kunata na beat, yaan freestyle life.
Kazi zangu nafanya masaa 8 kwa wiki, inategemea na project niliyonayo. Projects nyingi ni za malipo kwa hourly rate ($15 per hour) kwa sasa nafanya Brand & Identify Design kwahiyo process nzima naikamilisha kwa wiki moja ila kwa wastani wa kazi kufanyika 1 hour per day. Kwa mwezi nalenga kufanya projects 4 tu.

Muda unaobaki siyo kuwa hauna kazi. Muda mwingi natumia kujifunza Front-end Web Development.

Kwa siku nimegawa masaa 24 kwa 3. Masaa 8 ya kupumzika, masaa 8 ya kazi na kujifunza, masaa 8 yanayobaki itategemea na siku husika nina mambo gani yanayonitaka kuyafanikisha.

Gharama yangu ya milo 3 hailingani kila siku ila kwa wastani TZS 5,000 kwa siku.

Maisha ya "freestyle" nayo ni mazuri yanakufanya ufurahie zaidi kila siku unayoishi. Maisha ya kazi na kutimiza ndoto yamejaa stress za kutosha tu. Kimsingi hapa Duniani hakuna mapumziko. 😄
 
Unasumbuliwa na utoto tu sio jingine, ungejua maisha yenyewe wala usingeandika hayo, haya uhusiano wote na maisha halisi kabisa, determinants za maisha ya mtu nyingi ni external 20% ndo personality yako, sijui kama unalojua hilo?
Maisha ya mtu yako siku mimba imeingia mpaka siku ya kuzaliwa na jina lake,ni hivyo Ndivyo,namba pekee zinaongea
 
nikiwa sec.school niliapa kutoenda migodini kuchimba, no matter what will happen..hii ni baada ya kumuona jirani yetu kavunjika hovyo hovyo mguu wake,..na ukizingatia tena kwetu mzee na mama wote ni wasomi na wafanyakazi wa SERIKALI...miaka sita baadae nikajikuta niko migodini nikigonga nyundo balaaa😂😂, ..wachimbaji wenzangu walikuwa hawajui kuwa hata kitabu nimepiga, maana nilibadilika na kuamua tu sasa liwalo na liwe......so nakutakia safari njema bwana mdogo, ila fahamu changamoto za maisha halisi ni kubwa mno kuliko hizo za kwenye karatasi....
😂😂😂

Maisha yanabadilika fasta sana. Nadhani wahitimu wengi huwa wana picha zao kubwa kichani ambazo wakija mtaani ni tofauti. Kiukweli mimi mpaka namaliza sikuwahi kuwa na mawazo makubwa sana kwenye maisha yangu. Zaidi nilijua nikirudi mtaani mambo yatabadilika, na kweli ndiyo kilichotokea ila taratibu naanza kuendana na kasi ya Dunia na maisha kwa ujumla.
 
Habari wana-JF. Kama tunavyojua mpango kazi kwenye maisha ndiyo dira itakayokuongoza katika maisha yako na kufikia malengo yako.

Kwangu nahisi safari ndiyo kwanza inaanza na maamuzi yangu ya leo yatakuwa na mchango mkubwa kwa maisha ya baadaye.

Nikiwa kwenye early 20s (23) tayari nipo kwenye first phase ya mpango kazi wangu. Mimi shule nilikuwa siipendi kabisa kwa miaka 11 yote niliyosoma elimu ya msingi mpaka sekondari ila mtazamo wangu ulibadilika baada ya kujiunga chuo nikiwa na 18 na kuanza kusoma kile ninachokipenda.

Toka nikiwa mdogo nilikuwa ni mtu ninayependa kutumia teknolojia ya computer ni kwasababu ilikuwepo nyumbani na mzee wangu alinifundisha nilipokuwa mdogo sana. Nilipenda kucheza games na kufanya simple tasks mbalimbali. Mimi ni mmoja wa Gen Z niliyetumia Windows XP miaka hiyo.

So baada ya kumaliza sekondari nilijua nataka kusomea nini basi moja kwa moja nikainza safari yangu kwenye field ya Information Technology, miaka yote niliifurahia mpaka nilipohitimu kwa ngazi ya Diploma.

Sasa ukiachana na hiyo historia (intro) fupi mpango kazi wangu umegawanyika katika phase 2.

1st phase: 10 years
2nd phase: 10 years

So huu ni mpango kazi wa miaka 20 ijayo. Kwenye first phase ndiyo msingi unapoanzia, kitakachofanyika hapa ndiyo kitaleta picha ya kitakachotokea baada ya miaka 20.

1. Natumaini nitakuwa hai kwa miaka 20 ijayo.

2. Nataka niweze kufanya vitu ninavyovifanya kwenye early 20s kwa uwezo uleule au kwa ufanisi zaidi ya sasa. Hapa ni afya kuwa bora zaidi.

3. Nataka kuamua namna maisha yangu ya baadaye yatakuwa, na siyo magonjwa kuamua muda wangu wa kuishi duniani. Hapa ni kwa kuwa makini zaidi na afya yangu ya akili mpaka mwili.

4. Nataka kuishi kwa miaka 20 ijayo.

1st phase:

1. Career Building. Hapa nataka kujenga career yangu kwenye Web Development & Graphic Design (Freelancer) ndiyo kitu ninachifanya kwa sasa ila ninapotaka kufika ni safari ndefu ambayo siwezi kufika kwa usiku mmoja ndiyo maana ujenzi wa career yangu upo kwenye first phase. Malengo ni kuwa bora kwenye hizo field: bora kweli.

2. Education. Kwenye first phase ya mpango kazi wangu nataka kujiendeleza kielimu mpaka level ya Bachelor Degree. Hii naitaka ikiwa ni mwanzo wa safari nyingine kwenye second phase ya mpango kazi wangu.

3. Health. Afya ndiyo kila kitu, afya ndiyo uzima. Bila afya imara huu mpango kazi si kitu. Hivyo jambo la muhimu zaidi ni kulinda na kuimarisha afya yangu ya akili na mwili kwa miaka 20 ijayo. Hapa ni kwa kupata mlo kamili, mazoezi, kuwa na bima ya afya, kuupa mwili na akili mapumziko panapohitajika, kuyapa vipaumbele mambo yatakayonijenga na kunipa furaha zaidi.

4. Family & relationships. Nataka kuwa karibu zaidi na familia yangu: hao ndiyo watu wangu niliokuwa nao toka siku ya kwanza naletwa Duniani na ndiyo watakaokuwa na mimi katika safari ya maisha yangu. Mahusiano ni jambo la muhimu, hii ni safari nyingine kuelekea kujenga familia bora. Lakini sitaki mahusiano yaharibu mpango kazi wangu kabisa, hivyo ni kazi nyingine ya kutafuta mtu sahihi wa kuwa naye.

5. Personal development. Hapa nataka kuwa bora zaidi kwenye Technology na ndiyo njia ya kuijenga career yangu. Nataka kuachana na addiction zote zinazozuia mpango kazi wangu kufanyika kwa 100%.

6. Finance. Hili jambo la muhimu, mwanzo na mwisho wa mpango kazi huu. Nataka kujenga career itakayonipa fursa za kufanya Duniani popote na kunipa kipato kinachoendena na thamani ya kazi nitakayoifanya. Nataka kuweza zaidi kwenye Cryptocurrency & Stocks: elimu hapa ni muhimu zaidi. Nataka kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji wa kisasa, hii ndiyo back-up plan yangu japokuwa sitaki kuwa na back-up ni njia ya kwanza kujiona nimefeli kwenye mpango kazi wangu mkuu. Nataka kutafuta fursa nyingi zaidi za uwekezaji, sitaki kujipa limit, kujifunza zaidi ndiyo kufanikiwa zaidi.

7. Adventure. Malengo yangu kwa miaka 10 ijayo ni kusafiri zaidi, hasa nje ya nchi: kujifunza zaidi. Kupanda Mlima Kilimanjaro ni jambo lingine nataka kulufanya katika miaka 10, nilishatembelea Mbuga ya Wanyama ya Serengeti, hivyo kwa utalii Kilimanjaro ni my next target.

#: Kufurahia ujana ni jambo la muhimu zaidi kwasababu unakuja mara moja tu kwenye maisha. Kazi ni lazima ifanyike kwelikweli ila kufurahia maisha kila siku ni kushukuru kwa baraka hii tuliyonayo.

2nd Phase:

1. Education. Lengo kubwa kwenye second phase ya mpango kazi wangu itakuwa ni kujiendeleza kielimu kwa ngazi ya Masters. Hapa nataka kufuata nyayo za mzee wangu aliyehitimu masomo yake ya Masters nchini Netherlands. Nje ya nchi ndiyo lengo langu kuu kupata elimu huko, naamini fursa nyingi zaidi zitapatikana.

2. Family. Hapa sasa naamini ndiyo utakuwa wakati mzuri wa mimi kujenga familia bora baada ya msingi kutengenezwa kwenye first phase.

3. Work career. Hapa sasa ndiyo natarajia kazi kubwa zaidi itafanyika: kufanya kazi, uwekezaji kwa ajili ya kizazi changu.

4. Retirement. Baada ya miaka 20 ijayo natarajia kustaafu nikiwa na miaka 45-50. Ni muda ambao naamini ukifika napaswa kufurahia zaidi maisha na familia yangu bila kuwaza kufanya kazi tena. Lakini hili halitawezekana kama kazi bora na ya uhakika haitafanyika kwenye hii miaka 20 ya mpango kazi wangu.

5. Off-grid. Hapa naaminisha kuishi nje ya mji kabisa na familia yangu, mahali ambako nitafurahia maisha yangu baada ya kuikamilisha kazi kubwa iliyonileta Duniani. Kuwa na farm house ndiyo ndoto yangu kubwa. Kwa Tanzania tayari lipo eneo linalonivutia zaidi kuishi kwenye miaka 20 ijayo.

Yapo mengi ila hapa ni kwa kifupi tu. Ningependa kujua mipango yako kwa miaka 5, 10, 15 au 20 ijayo maana hapa tayari tunatofautiana umri, elimu, vipato.

Nataka kuishi kwa miaka 20 ijayo.
Ni kama tunafanana
 
katika upuuzi ambao si huweki akilini ni huu....sijui nikifka miaka hii nifanye hiki , lazima niwe na hiki sijui kazi . naacha vitu vifanyike vile Mungu anapenda , muhimu naweka juhudi tu na nidhamu ya kile nachokifanya kwa wakati huo.
Ni sawa kabisa kuwa na mitazamo tofauti ila naamini hata juhudi na nidhama ya kile unachofanya ni mpango kazi.
 
Kazi zangu nafanya masaa 8 kwa wiki, inategemea na project niliyonayo. Projects nyingi ni za malipo kwa hourly rate ($15 per hour) kwa sasa nafanya Brand & Identify Design kwahiyo process nzima naikamilisha kwa wiki moja ila kwa wastani wa kazi kufanyika 1 hour per day. Kwa mwezi nalenga kufanya projects 4 tu.

Muda unaobaki siyo kuwa hauna kazi. Muda mwingi natumia kujifunza Front-end Web Development.

Kwa siku nimegawa masaa 24 kwa 3. Masaa 8 ya kupumzika, masaa 8 ya kazi na kujifunza, masaa 8 yanayobaki itategemea na siku husika nina mambo gani yanayonitaka kuyafanikisha.

Gharama yangu ya milo 3 hailingani kila siku ila kwa wastani TZS 5,000 kwa siku.

Maisha ya "freestyle" nayo ni mazuri yanakufanya ufurahie zaidi kila siku unayoishi. Masiha ya kazi na kutimiza ndoto yamejaa stress za kutosha tu. Kimsingi hapa Duniani hakuna mapumziko. [emoji1]
Una kitu utafika mbali ila hapo kwenye mlo inabidi uongeze.

Huwezi kutumia elfu tano kwa siku halafu ukasema unapata mlo kamili na kama hupati mlo kamili ni vigumu sana kufikia hayo malengo yako hasa kwa aina ya kazi unazofanya.

Nikutakie kila la heri.
 
😂😂😂

Maisha yanabadilika fasta sana. Nadhani wahitimu wengi huwa wana picha zao kubwa kichani ambazo wakija mtaani ni tofauti. Kiukweli mimi mpaka namaliza sikuwahi kuwa na mawazo makubwa sana kwenye maisha yangu. Zaidi nilijua nikirudi mtaani mambo yatabadilika, na kweli ndiyo kilichotokea ila taratibu naanza kuendana na kasi ya Dunia na maisha kwa ujumla.
pia ningekushauri focus zaidi kwenye stocks na sio crypto....
 
Una kitu utafika mbali ila hapo kwenye mlo inabidi uongeze.

Huwezi kutumia elfu tano kwa siku halafu ukasema unapata mlo kamili na kama hupati mlo kamili ni vigumu sana kufikia hayo malengo yako hasa kwa aina ya kazi unazofanya.

Nikutakie kila la heri.
Kweli kabisa, lengo langu kubwa ni kupata mlo kamili. Mimi ni mmoja wa watu wanaotumia sana junk foods: vyakula vya viwandani, soda n.k. Nataka kupunguza au kuachana na hivi vitu kabisa.

Mlo kamili ni gharama ila nataka kuupata kila siku. Afya yangu kwa sasa imekuwa kipaumbele zaidi.

Asante sana kwa maoni yako.
 
pia ningekushauri focus zaidi kwenye stocks na sio crypto....
Soko la Crypto lilikuja na hype kubwa sana ikabidi nijifunze maana ni rahisi kuelewa kuliko Stocks.

Crypto haitabiriki naona kwa sasa hali mbaya ila natarajia kuipata elimu ya Stocks vizuri zaidi maana ina vitu vingi vya kujifunza kabla ya kuingia huko.

Asante sana kwa ushauri wako.
 
Sasa hivi wakati tupo JF kuna watu wanaweka mipango ya kuwa mabilionea wakiwa hawana hata TZS 100. Hiyo yote bado haimaanishi kuwa watafeli, wapo watakaoweza kufika mwisho na watakaoishia njiani.

Mimi najiona bado nina ndoto ndogo sana ukilinganisha na watu wengine. Kwenye maisha usipojiamini mwenyewe hakuna atakayekuamini.
 
Soko la Crypto lilikuja na hype kubwa sana ikabidi nijifunze maana ni rahisi kuelewa kuliko Stocks.

Crypto haitabiriki naona kwa sasa hali mbaya ila natarajia kuipata elimu ya Stocks vizuri zaidi maana ina vitu vingi vya kujifunza kabla ya kuingia huko.

Asante sana kwa ushauri wako.
baada ya kutoka migodini nilipigwa chini na my wife to be,...nikapambana sana, nikakaa sawa KISAIKILOJIA na kuanza kupata elimu mbalimbali katika nyanja za kidijitali,...nimejifunza zaidi kuhusu forex, crypto,na stocks... stocks ni the best, kwa kuwa na SHARES sio (kutrade).... cryptos zitapanda kwa baadae kwan zinazidi kutumiwa zaidi na watu kwenye black business and international exchanges,lakini ziko nyingi mno na zinazidi kuongezeka na ni very complicated kwenye kufahamu ni factors gani zitachochea kupanda kwa thaman ya crypto fulani tu na sio zinginezo ... kwenye stocks focus na NASDAQ, SP500, PEPSI and COCA-COLA.. different tech startups and wine companies.....soma hizo tu mdogo wangu naamini zitakusaidia zaidi hata ya unavyodhani....
 
Asante kwa muongozo.
 
Hamna tofauti na mtu anaesema atakuja kua mfanyabiashara mkubwa wa magari dunia nzima wakati hata pipi hajawahi uza
 
Back
Top Bottom