Una mshahara wa laki nane, kwanini uchukue mkopo na kuanza kukatwa karibu laki nne?

Una mshahara wa laki nane, kwanini uchukue mkopo na kuanza kukatwa karibu laki nne?

Tatizo hao UTT wenyewe hawajitangazi wako wapi! Unaweza kuta wako Dar tu je mtu wa Kigoma anawafikiaje? Unaweza kukuta wanasiasa wameelekeza pua zao hapo ukifika muda wa uchaguzi wanakomba kibuyu chote mwisho wa siku wanaleta kama zile za NSSF na the like
Toka lini soko la Kariakoo Huwa linajitangaza kwa wakulima. Tafuta soko ndugu mkulima
 
Wewe umeajiriwa lumumba unalipwa buku 7 ndio una akili? Watu wengi walioajiriwa wanaumia sana kwa hii mikopo wanachukua na kupoteza hizo pesa. Matokeo yake wanachukia kazi, wanapoteza ufanisi, kuwa wezi na hata kusumbua watu wawasaidie.

Mtu yeyote asiyeweza kudunduliza akafikisha kiasi fulani cha pesa bila kukitumia hawezi kufanikiwa hata apewe milioni 100. Pesa ina kanuni zake ndio maana masikini ni wengi.
Halafu mikopo inawafanya waajiriwa wengi kuwa na hasira hasira, kila mtu wanamuona mmbaya hapo ujue makato ya mkopo yamechanganya maisha yamekua magumu
 
Sio kweli, bank nyingi stable kubwa Tanzania wanatoa deposit rate kuanzia 10%+.

Pili why upelele pesa zako UTT wakati unaweza kununua hati Fungani za serikalini ambazo sasa zinatoa riba nzuri tu.

Kupeleka pesa zako UTT ni kama unakua unacheza kamari, una bet wakati kuna vyanzo vingine vya kuwekeza vya uhakika ambavyo unaweka pesa zako ukaa kunywa juice na kuku kwa mrija mpunga unaingia bila jasho.

Kuhusu waajiriwa, watu hawatoki kwenye same background, mtu mwingine ndio kichwa cha familia, wanategemewa kubadilisha hali za nyumbani kwao sasa aache kukopa kisa ni maamuzi ya hivyo sio kweli.

Acha watu wakope watatue matatizo yao, ya huko mbele hayajulikani.
Mkuu jiongezee maarifa kwenye uwekezaji wa UTT.Ikiwa hulijui jambo kaa kimya,hakuna mfuko UTT uliotoa faida chini ya 12% kwa mwaka wa fedha uliopita.UTT inalipa kuliko huko kwenye bond za serikali na benki.
 
Ona ulivyo mpumbavu kutoa majibu ya jumla jumla.

Siwezi kubishana na wewe hapa hujui chochote. Usilete uzoefu wako wa saccos huko eti consultancy kwenye corporate world. Hujui chochote.
Mkuu hujui chochote kuhusu UTT,achana na maarifa yanayopatikana kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Mimi ni kati ya watu waliokopa na wanalipwa kiasi kidogo cha pesa za mshahara na sijuitii hilo kwa nilichokifanya.
Kipindi nakopa eneo nililonunua kiwanja ilikuwa kama 5.5 M na kiwanja ni 15 *20 M sahv bei.yake ni zaidi ya 8-10 M

Kipindi naanza kujenga nondo ilikuwa elfu 20 ya 12 mm na mfuko wa cement ilikuwa elfu 14 mpaka 15 elfu ,sasa unaweza fikilia sahivi hizo bidhaa zimepanda kwa kiasi gani ? Lakini pia nashukuru nalala kwangu na sidaiwi kodi na mtu na nina amani ya moyo hilo tu inatosha na sijuitii kukopa na kukatwa hata siku moja

Kimsingi ningesema niweke savings ingekuwa ngumu sana kutoboa na ningekuja kufanya vitu kwa gharama kubwa zaidi
 
Wewe kwanza ni muongo, mimi nina 40m+ liquid fund na ninapata around 370k kwa mwezi, haiwezekani wewe na 30m upate 467k.

UTT ni uwekezaji, ukiona haufai nenda kafanye biashara.
Haujawekeza Bali umetunza pesa isipotee, umewekeza 40M na mwaka mzima return yako ni 3.7M yaani 370,000 kwa mwezi!! Haifiki hata 10%
Ukitoa inflation ,unabakiwa na bei gani?
 
Usitupangie Cha kufanya kwenye mishahara yetu
 
Back
Top Bottom