Una mshahara wa laki nane, kwanini uchukue mkopo na kuanza kukatwa karibu laki nne?

Una mshahara wa laki nane, kwanini uchukue mkopo na kuanza kukatwa karibu laki nne?

Kwanini wewe usihifadhi hata UTT shilingi laki 3 kwa mwezi? Kwa mwaka utakuwa na 3.6m na miaka mitano itakuwa 18m, tena hapo bila kuweka faida yake.
Tatizo hao UTT wenyewe hawajitangazi wako wapi! Unaweza kuta wako Dar tu je mtu wa Kigoma anawafikiaje? Unaweza kukuta wanasiasa wameelekeza pua zao hapo ukifika muda wa uchaguzi wanakomba kibuyu chote mwisho wa siku wanaleta kama zile za NSSF na the like
 
Okay, wala sina sababu ya kujibishana na wewe, na wala hatushindani, we endelea kuweka 40m upate 300,000.
Uungwana ni kukubali kwamba ulidanganya.

Mimi UTT naweka kama savings. Hiyo 40m nimeplan ifike 100m mwisho wa 2024 kwa kuendelea kuwekeza. Sina muda wa kufanya biashara na sitaki hela ikae benki.
 
Uungwana ni kukubali kwamba ulidanganya.

Mimi UTT naweka kama savings. Hiyo 40m nimeplan ifike 100m mwisho wa 2024 kwa kuendelea kuwekeza. Sina muda wa kufanya biashara na sitaki hela ikae benki.

Ni sawa nimedanganya, maana form yangu ulinijazia wewe, na plan yangu na yako zinafanana!!!!
 
Tatizo hao UTT wenyewe hawajitangazi wako wapi! Unaweza kuta wako Dar tu je mtu wa Kigoma anawafikiaje? Unaweza kukuta wanasiasa wameelekeza pua zao hapo ukifika muda wa uchaguzi wanakomba kibuyu chote mwisho wa siku wanaleta kama zile za NSSF na the like
UTT wana ofisi mikoani, cheki kwenye website yao. Huku hamna serikali itakayogusa kwasababu ni kitu cha hiari na hela yako unaweza kuichukua muda wowote.
 
Mkuu ukifuatilia hawa waajiriwa ni kichekesho, hizo hela huwa zinaisha bila maelezo halafu wanaishia kuteseka.

Mimi namuona mtu kuwa mpumbavu kwa kujishushia kipato. Bora asevu hata miezi minne, apate 1.2m halafu hiyo aitumie kufungua biashara ya kumpa 10k mpaka 30k kwa siku.

Hapo atakuwa ameongeza kipato lakini sio upuuzi wa kutoka kwenye laki 8 hadi laki 4 kwa mwezi.
Kikubwa hapa ni mipango ya mtu, kukopa na kujemga au kununua gari ni kuzika hela chini..

Kuna baadhi ya pesa kuzifikia kwa kudunduliza, haswa kwa hizi familia zetu za kimaskini, we mwenye mshahara wa laki 8 ndio umetoboa, mjomba, mamkubwa, bibi, sijui mtoto wa nani, bado ukweni wote wanakutizama wewe ni ngumu saana kufikisha, hapo ndipo mkopo unakuwa fresh, lakini uhakikishe unachoenda kufanya kuna 90% ya kutoboa, sio unaenda kubahatisha, itakula kwako
 
Interest ni % ngapi kwa mwaka na makato mengine yapoje
Kwenye liquid fund ambako mimi nimeweka hela hamna makato yoyote. Faida ipo kati ya asilimia 12 na 14 kwa mwaka kutegemeana na performance ya bond za serikali, gawio la makampuni mbalimbali na pia bond za makampuni mbalimbali.
 
Sasa hapo kwenye misamiati mingi ndipo mnatuchanya na huenda ndipo tunapoibiwa "liquid, bond"
 
Uzi mzuri,yani jamaa wanavyozidi kupambana sie wengine tusiojua tunajifunza,endeleeni tu...
 
Unaanza mkopo upya
Si bora hata kuanza mkopo upya, "top up" inamaana kuna mkopo ulikuwa unaendelea kukatwa benki lakini ukataka kuchukua mkopo mwingine/mpya ila hauna namna ya kumaliza deni inabidi benki hiyo hiyo iliyokua inakukata inunue deni unalodaiwa ili kumaliza deni na ikupatie mkopo upya, ni zaidi ya majanga [emoji1745][emoji2].

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom