Una mtaji ila hauna pesa ya kodi ya fremu? Zijue biashara zisizohitaji fremu

ndio shida ya nyinyi wasomi, ndio maana huwa wengi wenu mnafeli sana katika biashara kwa sababu ya too much know
 
Ni good ideas ila hiyo ya mitungi ya gesi kwa kuanzia inahtaji mtaji kiasi gani
 
ifanye
+
ukiweka bidiii Hautojutia.
WW mwamba kiukweli ktk nyuzi zako za ujasiriamali huwa nakuelewaga sana aise..Katika dini yangu ya kiislam tunaamini mtu kama wewe una malipo makubwa sana kwa Mungu ,ima atakulipa hapa hapa duniani kupitia biashara zako au ukishakufa kama wewe ni Muumuni.Mkuu unafanya kazi kubwa sana japo huenda wewe mwenyewe usielewe ukubwa wa unachokifanya.Huwa nachunguza sana nyuzi zako na kiukweli hunaga roho kubwa yan unaeleza unachokijua na hufichi.
Mkuu haya unayoyaongea yanadumu daima na yanasomwa na wengi ila amini Mungu hatakuacha bure kwan anaona unachokifanya........Mungu akupe kila lililo zuri Mzee.
 
🙏 🙏 🙏

Na Mungu wangu atawapeni ninyi kila kitu mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake mtukufu katika Kristo Yesu.

Wafilipi 4:19

Ubarikiwe nawe pia SweetieLee
Nawaza kuhusu mobile games.. michezo ya watoto kwa shule mbali mbali ingawa fan yangu ni IT. Mawazo yako mkuu
 
Amen mkuu 🙏

Duniani si makazi yetu ya kudumu,kila tulichonacho tutakiacha hapa hapa

sina uwezo wa kugawa pesa kama walivyo wenye uwezo wengine,lakini

sitoshindwa saidia wengine kwakile ninachoona kwangu kilibadilisha maisha yangu

Tuzidi kubarikiwa sote mkuu,napokea yote uliyoniombea Asante na Mungu akubariki.
 
Mitungi ya gas hutakiwi kuuzia kwenye makazi ya watu kwa sababu ni hatari
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mitungi ya gas hutakiwi kuuzia kwenye makazi ya watu kwa sababu ni hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna biashara isiyo hatari,muuza duka haruhusiwi kuuza mafuta ya taa lakini ukienda kwa mangi utakuta mafuta ya taa anauza kupitia hayo faida anapata.

Huyo mangi angekua kasema afuta ya taa ni hatari kuuza leo hii wewe unaetafuta mafuta ya taa ukakoleze moto ungeyapata wapi? unatafuta mafuta ya taa ukachome takataka jalalani ungeyapata wapi?

Maji ya kandoro ni hatari kwa afya yako kwasababu yanawekwa kwenye vinailon bila usafi maji yanwekwa si mazuri lakini watu wananunua na muuzaji anapiga pesa,ila si kwamba yale maji ya kandoro ni mazuri kwa afya,ni hatari ten hatari kweli.

Mama ntilie anapika chakula,ushawahi ona mazingira anayopkia chakula? umeshawahi ona nyanya zinazopikiwa zile mboga zao? mkuuu n hatari tena hatari fire ila watu wanaishi kupitia u hatari huo huo.

Boda boda wanapakia mishkaki,unajua hatari za mishikaki? asee mkuu nataka tu kukwambia hakuna biashara isiyo na hatari na ukitafuta hizo biashara utazikuta kwenye shopping Mall tu,kule ndio kwenye usalama TU.

Huku madukani tunauziwa bidhaa fake na zilizo expire ila MUNGU tu ndio anatulinda, wewe ukikaa ukisema GESI ni hatari kwenye makazi ya watu kuna mwenzako upande wa pili anauza na anapiga pesa.
 
Uswahili sasa huu.. labda uuze bila vibali.. tatizo mtu unawekeza biashara ya kil 5 katika mazingira yasio faa, wakija siku wakakupora unaanza kulalamika.


Tumia kichwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Container zinapatikanaje ndugu? Nahitaji aisee
 
Contena za hiyo bei zipo kweli ? Manake bei zimesimama balaa,
kontena zinapatikana kwa hiyo pesa mzee coz mimi kuna jamaa yng amenunua kwa laki saba tuh na iko vizuri hadi aliligawanya vipande viwili
 
vipi kuhusu biashara ya chipsi mkuu, nipe mwongozo kidogo
 
Vipi Mkuu kuhusu kuuza Ubuyu kwa reja reja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi Mkuu kuhusu kuuza Ubuyu kwa reja reja?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubuyu sifahamu kabisa kuhusu hiyo biashara,ninachoamini katka biashara Hakuna biashara isiyo na Faida ubuyu unafaa sana kuuza reja reja ila si kwenye makazi yetu huku nyumbani.

Hiyo biashara naamini ina faida na haitaki frem lakini wateja wa hiyo biashara ni wanafunzi wa primary,hapo muuzaji anatakiwa akatege maeneo penye mikusanyiko ya watoto watoto n biashara nzuri naamini.

ila kuuza buyu kwa mtu wa nyumbani sidhani kwakweli na si ubuyu tu ila biashara zote za kula kula kama ubuyu,karanga,crips,nk simshauri mtu auzie nyumban hzo n biashara za kumfata mlaji direct na sio kumsubiri aje anunue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…