Una Walimu wengi hadi wa akiba bado vyuo vinaboreshwa na kudahiri Walimu Hapo malengo ya serikali nini?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Una Walimu wengi Hadi wa akiba bado vyuo vinaboreshwa na kudahiri Walimu Hapo malengo ya serikali nini? hao Walimu wakajiajiri vipi au wakajenge shule

Msaada, jamani Mimi sielewi naombeni mawazo yenu?
 
Kwa hiyo ma daktari wakiwa wengi basi vyuo vya udaktari vifungwe, au kwa vile wanasheria ni wengi na mahakama ni chache basi vyuo vya sheria vifungwe, 🤪🤪🤪 we kweli hamnazo..
 
Serikali hailazimishi mtu kusomea ualimu
 
ni biashara na hiari yako.kweli walimu wamekuwa wengi sana
 
Kwa hiyo ma daktari wakiwa wengi basi vyuo vya udaktari vifungwe, au kwa vile wanasheria ni wengi na mahakama ni chache basi vyuo vya sheria vifungwe, 🤪🤪🤪 we kweli hamnazo..
Sawa mkuu madaktari wanaweza kufungua maabara za Kati wakajiajiri pia wanasheria wanaweza kuwa mawakili wa kujitegemea Sasa Mwalimu ajenge shule? Mtaji anao?
 
Hii ndo inatakiwa

Sijasoma historia vizuri ila kipindi vita dunia inaisha wanajeshi walirudi manyumban na kusababisha baby boom na hapo ni kutokana na great economic depression kupita America wakaona wanaweza kuzaana

Wacha watu wasome
 
Una Walimu wengi Hadi wa akiba bado vyuo vinaboreshwa na kudahiri Walimu Hapo malengo ya serikali nini? hao Walimu wakajiajiri vipi au wakajenge shule

Msaada, jamani Mimi sielewi naombeni mawazo yenu?
Kwa wale waliosoma Bachelor of Art with Education, wanajifunza mambo mengi sana nje kabisa na kufundisha. Hii degree haikuandai kuwa mwalimu tu. Unaweza kufanya shughuli zingine kabisa nje ya kufundisha . Jambo la mwisho si kila mtu anaweza kupata ajira serikalini ,ipo pia sekta binafsi.

Jamabo la kufanya ni kuwa serikali iisadie sekta binafsi kukua bila vikwanzo ili iweze kuajiri vijana wengi. Moja ya strategy ya kuikuza sekta binafsi ni kuangalia mfumo wa kodi. Mfumo wetu si rafiki sana. Hauvutii sana uwekezaji wa ndani na nje.
 
Sawa mkuu madaktari wanaweza kufungua maabara za Kati wakajiajiri pia wanasheria wanaweza kuwa mawakili wa kujitegemea Sasa Mwalimu ajenge shule? Mtaji anao?
Si ndio maana kuna private schools
Na uzuri hulazimishwi kusomea ualimu unachagua mwenyewe

Ndio maana unaweza kusomea hadi international relations halafu utajua wewe utakapo enda kufanya kazi 🤪🤪🤪
 
Una Walimu wengi Hadi wa akiba bado vyuo vinaboreshwa na kudahiri Walimu Hapo malengo ya serikali nini? hao Walimu wakajiajiri vipi au wakajenge shule

Msaada, jamani Mimi sielewi naombeni mawazo yenu?
Ni sawa tu na serikali kutaka kila mtanzania awe na bima ya afya wakati huduma za afya ni mbovu! Ni biashara tu.
 
Una Walimu wengi Hadi wa akiba bado vyuo vinaboreshwa na kudahiri Walimu Hapo malengo ya serikali nini? hao Walimu wakajiajiri vipi au wakajenge shule

Msaada, jamani Mimi sielewi naombeni mawazo yenu?
Ili kuongeza majobless mtaani
 
Back
Top Bottom