Kichwa Ndio Mtu
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 3,079
- 1,711
Kimaubile mwanamke ndie anaekaa na watoto kwa muda mrefu na ndie mlezi kwa asilimia 80 hivyo unaweza kuuona huo ukaribu
Wanawake wanakuwa wagumu sana kwasababu za wivu yaani kila akimuona yule mtoto anakuwa anamuona kama mumewe amemsaliti na inasababisha amuone mtoto nae ni mkosaji sana na kuanza kumsumbua na kumtesa
Kwa upande wa wanaume ni wachache sana wanajali kuhusiana na watoto na mara nyingi baba yeye wala hashindi nyumbani hivyo inakuwa ngumu sana kujali kuhusiana na hilo
Wanaume wengi sana wameoa wanawake wenye watoto lakini wanawake wachache sana wameolewa na wanaume wenye watoto na hao wachache kunakuwa na sababu kama nilizozisema hapo juu
Mimi ni mmojawapo wa wanaume ambao wala sitajali sana kuhusiana na mwanamke kama akiwa na mtoto,tutalizungumza hilo na wala hicho sio kitu ambacho kitanifanya nisimuoe au kuanzisha mahusiano na mwanamke!
Dah!umenijibu kwa buusara ya hali ya juu sana, umenisababisha nijione mwenye makosa kwa kuwachukulia wanawake wenye watoto wakosefu,nareview mtazamo wangu juu ya wanawake wenye watoto