Unabii wa nyerere utabiri wa shehe Yahaya anguko la CCM na udhaifu wa Samia katika utimilifu wa nyakati

Unabii wa nyerere utabiri wa shehe Yahaya anguko la CCM na udhaifu wa Samia katika utimilifu wa nyakati

ANGUKO la ccm liko karibu sana kuliko tudhanivyo ila namuomba Mungu wasije wakasababisha bloodshed. Maana ndivyo watawala wa afrika walivyo.
 
Nyerere alitoa UNABII huu Kwa usahihi kabisa namnukuu. Chama kisichosikiliza maoni ya wananchi kitalia machozi kisipate mtu wa kuyafuta. UNABII umetimia. Haya yanayoendelea ni matokeo ya ccm kutosikiliza maoni ya wananchi watu walitekwa nchi nzima tulipiga kelele sana humu mkashupaza shingo. Rais akajibu fyongo malalamiko ya utekaji. Spika akazuia mijadala ya utekaji na mahakama zikawafunga kina LISSU kiuonevu. Mdude akapotezwa spika akajibu ujinga mbele ya TV watu wakasema hewalaaa.

Shehe YAHAYA mtabiri maarufu aliyasema mapema kabla ya umauti wake namnukuu. Atatokea rais mchekeshaji atatawala KIPINDI kimoja halafu atakuja rais mwanamke baada ya hapo ccm itaanguka na wapinzani watachukua nchi. UTABIRI huu ukiangalia Kwa jicho la mbali unaenda kutumia au umeshatimia Kwa sehemu.*

Samia ni Rais mbaya kuwahi kutokea katika historia ya Taifa letu. Na historia itamwandika hivyo kuna ujinga mwingi anaufanya ambao hata yeye hajui kwanini anaufanya ila yote haya ni ili UNABII utimie fikiria Kwa mfano hotuba yake ya kuuwa taasisi kisa undugu nepotism alisema Kwa mdomo wake Cha ajabu yeye muda mfupi baadae akafanya nepotism ya hali ya juu kitu ambacho hakijawahi fanywa na rais yeyote yule Nyerere hakuteuwa wanae walikuja kuteuliwa na Marais wengine (refer makongoro) Mwingi hakumteuwa mwanae aliteuliwa na mkapa (refer Dr Mwinyi)

Kikwete hakumteuwa mwanae Ridhiwani aliteuliwa na MAGUFULI (refer Ridhiwani) Mkapa ndio kabisaaa watoto wake hata hawajulikani yule aliyekuwa karibu mkuu aliteuliwa na MAGUFULI. Sasa Samia kuingia tu madarakani tena Kwa wizi wa kura kamteuwa mtoto waziri mkwe waziri shemeji mshenga nk Sasa jiulize ile kauli yake ya nepotism na alichofanya je hawa ni Samia wawili tofauti au ni Samia mmoja? Jibu ni rahisi UNABII WA ANGUKO LA CCM UMETIMIA NA CCM INAANGUKA MWAKA HUU. UZI HUU UTABAKI KAMA ALAMA YA MKUSANYIKO WA NABII NA TABIRI ZINAZOENDA KUIPELEKA CCM KABURINI KAMA KANU. TUKUTANE D9.
RUBBISH
 
"Tusiseme hatuna matatizo kwa kuyaficha matatizo yetu wenyewe. Ujasiri wa taifa hauko katika kuficha kasoro zake, bali katika kuzikubali na kuzitatua." Mwalimu J K Nyerere.
 
Back
Top Bottom